El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 297
- 537
Maandamano yanayoendelea nchini Kenya, binafsi hayajanivutia kwa sababu hayana lengo linaloeleweka.
Uharibifu unaofanywa na waandamanaji kama kuiba na kupora Mali za watu hii inaonyesha maandamano hayo hayana lengo.
Ilianza na kutaka budget irekebishwe kwa kile walichodai maisha magumu,. Serikali ikakubali kufanya mabadiliko( amendment) bado wakaandamana.
Jana Rais Ruto akakubali kwamba budget nzima irudishwe bungeni kwa amendment nyingine, bado Leo watu wameandamana.
Hii tabia haionyeshi kabisa lengo la maandamano. Na nahisi hata siyo suala la uchumi Bali chuki za kisiasa dhidi ya Rais aliyeko madarakani.
Hao Gen Z hawana hata Uongozi, jambo ambalo linaonyesha hii ni movement holela unayotaka kuifanya nchi isitawalike.
Ukiacha Sasa hayo mengine, bado naona Kuna jambo chanya la viongozi wa Tanzania kujifunza kabla haijaja hapa pia.
1) Tamaa ya madaraka
2) ukwasi uliopitiliza wa viongozi.
3) kuwasahau vijana katika nafasi mbalimbali za ujenzi wa Taifa Leo.
4) Dharau ya tabaka tawala ( hapa namaanisha hasa chama tawala kama hapa CCM) . Kudhani kwamba nchi ni yao tu. Kumbukeni Kenyata na wenzake ( Tabaka tawala, na watoto waliokua wazazi wao wakiwa madarakani) wanamdharau Ruto ambaye anatokea kwenye familia masikini, na hivyo ni rahisi kuchochea watu kwa jina la kutaka mabadiliko ya kuichumi kwa ajili ya wananchi.
Siku za hapa mbele nitakuja kufafanua hasa sababu za hayo maandamano kama nilivyoziorodhesha hapo juu, Sasa nakimbia mahala.
Usiku mwema.