PreGE2025 Wakili Addo November: CHADEMA bado wanayo nafasi kutia saini kanuni za maadili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
No Reforms No Election

Yule dingi wao wa Msoga amekuwa na ufala mwingi sana nowadays ,jana amezingua sana ,mastory mengi then pointless
Yule mzee sijui kwa nini hauwawi hana faida yoyote kwa nchi hii zaidi ya ukuda tu na kumtengenezea mwanawe nafasi ya kuja kuwa Rais baada ya Samia.
 
labda wakasaini kwenye tume ya Uchaguzi isiyo huru ambayo haina taratib zake huru za kusimamia wajibu na majukumu yake kwa uhuru.

But Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi makini kama hii inayojiandaa kusimamia uchaguzi mkuu wa October mwaka huu 2025, hiyo nafasi ya kila chama kuamua kitakavyo kwa wakati wake hawatakua nayo abadan 🐒
 
Your browser is not able to display this video.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeelezwa kuwa bado kina nafasi ya kutia saini kanuni za maadili ya uchaguzi ili kipate fursa ya kushiriki uchaguzi.

Chama hicho kilisusia kusaini kanuni hizo Aprili 12, 2025, huku vyama vingine 18 vikisaini.

Akizungumza jana Juni 21 katika Kongamano la Sheria lililofanyika jijini Dar esSalaam, Ado November kutoka Chama cha Wanasheria wa Serikali alisema chama hicho kinayo fursa hiyo.

“Leo CHADEMA wakija wakitaka kushiriki nafasi wanayo ‘as long as’ hatujafikia hatua ya kuanza mchakato wa uchaguzi,” amesema Ado
 
No Reforms No Election

Yule dingi wao wa Msoga amekuwa na ufala mwingi sana nowadays ,jana amezingua sana ,mastory mengi then pointless
Tangu lini mswahili akawa na akili.
 
Watu wazima wamekutana kujadili ujinga ujinga tu.
 
Hakuna nafasi nyingine ya kutia saini.
 
Hata behind closed doors wanaruhusiwa kusaini.
Unaposikia mtu kama huyo Ado anazungumzia swala la "CHADEMA kusaini", ujue kuna joto kali huko jikoni.

CHADEMA hawana sababu yoyote ya kusaini chochote bila ya mabadiliko ya kanuni za uchaguzi kuruhusu uchaguzi HURU na wa HAKI
Hiyo ndiyo maana ya "NO REFORM, NO ELECTION"...,; vinginevyo watajieleza vipi kwa waTanzania?

Wataeleza kwamba wamepata njia mbadala wa kuhakikisha kura za waTanzania hazichezewi, hata katika mazingira mabovu yaliyopo; ni njia zipi hizo? Itabidi wajieleze vizuri sana ili wananchi wawaelewe.

Kwa mfano: wanaweza kueleza ni namna gani watazuia Samia Suluhu Hassan asitangazwe kuwa mshindi na Mwenyekiti wa Tume, hata kama atakuwa kashindwa uchaguzi? Watatumia mbinu zipi kufanya hivyo!

Na je, CHADEMA wapo tayari kuweka sahihi, wakati Mwenyekiti wao akiwa Jela?
Watakubali kutia sahihi wakati kesi za kuwazuia wasijishughulishe na siasa zikiendelea mahakamani?

Wataweka sahihi wakati Mtungi hatambui viongozi wateuliwa wa chama hicho?

Wakati joto likizidi kupanda, ni sahihi kuwahimiza CHADEMA kwa ujumla wao, siyo viongozi wa juu pekee, waongeze kuni kwenye hii kampeni ya NORNOE; kwani inaonyesha wazi kwamba inaeleweka vizuri sana kwa wananchi kwa wakati huu.
 
John Heche, makamu Mwenyekiti CHADEMA ameshawajibu tayari. Sikiliza majibu hapa👇👇

View: https://youtu.be/s7wfACK12Uo?si=t5McK8ym6A5JUOXR
 
Watakuwa wapumbavu sana kushiriki uhuni wa uchaguzi...kete sahihi ni kuto kushiriki bila ya kupepesa macho ...faida ni nyingi kwenye hiyo kete ...mfano kama chadema wangetia saini basi kungekuwa na fujo kutoka genge la wapumbavu wa mbowe ila kugomea kutia saini na kushiriki uchaguzi, umewafanya wahuni wa "ccm ya mbowe" kukimbia chadema kwa kujitoa...pia itasahidia chadema kuwa chama pekee kwa upinzani na kufanya vyama vingine vyote kutokubalika tena milele daima
 
Wameona maji ya shingo sasa wanatapatapa wamekua vigeugeu. Ina maana walivyotangaza na kutoa tamko kuwa CDM haitaruhusiwa kushiriki uchaguzi kwa kuwa hawakutia sign hawakua ni wao?...Mbona hawakusema kuwa bado wana nafasi ya kutia saini toka mwanzo?

NO REFORMS NO ELECTION
 
Mbona form za C-19, walisaini wasiojulikana na huko wakasaini tu! Baada semeni tu wamesaini CDM! Kwisha.
 
Ndio huyo , jamaa mpuuzi sana huyu. Ana tamaa sana na ni mpigaji mzuri kupitia mgongo dini
Sasa hapo amepiga wapi mjinga wewe mnajiita wanademokrasia ila mawazo ti ya mtu hamtaki kusikia

USSR
 
Sasa unafikiri Addo atapoteza nini ikiwa chadema itafel

USSR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…