Wakili aliyeitwa Ofisini kwa DCI Kunyamaza ni Makosa

Wakili aliyeitwa Ofisini kwa DCI Kunyamaza ni Makosa

Mwenzako kishatapika huko mpaka wanaomlipa. Kuna cha kuongea tena hapo.

Wewe subiri leo au kesho anatangazwa mshindi wa zabuni rasmi, habari zilizovuja ni DP World. na siku wanayotangazwa wanaanza kazi rasmi.

Hapo sasa!

Hiyo zabuni imetangazwa wapi?
 
Hata wewe unaweza kuitisha wanahabari ukawaambia unatishiwa maisha baada ya hapo utaitwa kuhojiwa na ukirudi utatupa mrejesho . Wabongo mnapenda kuwatumia wenzenu kwenye matatizo nyie mmetulia majumbani mwenu kimya.
Wewe unanufaika na nini?

"Unawatumia" akina nani katika kunufaika kwako huko?

Usidhani kunyamazisha watu ndiyo suluhu ya kuondoa matatizo, na hili litawagharimu sana.
 
Mkuu 'denooJ', hicho Kibibi kielewe vizuri.

Ukisoma maandishi yake yote humu ndani ya JF, na hasa kwenye hili sakata la DP World, utaelewa vizuri kazi anayofanya.
Tatizo hiyo kazi anaifanya kwa akili ndogo sana, atadharauliwa mpaka na watoto wadogo, naona sasa anajiropokea tu baada ya kuishiwa maneno ya uongo.
 
Sasa nawe utasema unajua unacho andika juu yake, au ni kujivimbisha tu na jambo usilolifahamu kabisa?

Kwanza uandishi tu unaonyesha kiwango cha chini kabisa cha uwezo ulio nao katika eneo hili. Kwa hiyo huna lolote unaloweza kuchangia hapa linaloweza kufikirisha wasomaji.
Nia yako ni kuweka vitisho tu, ukidhani enzi hizi bado watu wanatishwa kama enzi za ukoloni..
Sio kuvimba huo ndio ukweli kila jamii ina misingi yake katika kila nyanja za maisha yanayotuzunguka. Tunapotofautina kimawazo sio sehemu ya kupanda chuki na kejeli dhidi ya mamlaka. Hapa hakuna ujuaji wala kitu chochote isipokuwa hekima na busara vinapaswa kutangulia mbele. Mbona prof shiv hakuitwa wala kutushiwa kwanini yeye. Mamlaka za nchi lazima zieshimiwe sio unaweza kuargue against na sio kumdhalilisha raisi na kauli zenye utata utanyooshwa tu. Ukitaka kujua mamlaka ziko active fanya ujinga uone ndio maana magufuri alikuwa mkali kwenye ujinga unaoitwa Uhuru wa kujieleza.
 
Mwenzako kishatapika huko mpaka wanaomlipa. Kuna cha kuongea tena hapo.

Wewe subiri leo au kesho anatangazwa mshindi wa zabuni rasmi, habari zilizovuja ni DP World. na siku wanayotangazwa wanaanza kazi rasmi.

Hapo sasa!
Huna taarifa yoyote wew Ni mganga tu Mara dp anafunga mashine zake ,Mara wako wanajindaa kutua nchini yaani wee huna tofauti na popoma
 
Mkuu 'denooJ', hicho Kibibi kielewe vizuri.

Ukisoma maandishi yake yote humu ndani ya JF, na hasa kwenye hili sakata la DP World, utaelewa vizuri kazi anayofanya.
Usihangaike sana, wewe na wezako niulizeni mtakacho kukifahamu, nimeweka uzi wa watu kuuliza chochote wapemdacho, bofya chini hapo ukaulize"

Dr Rugemeleza Nshala aliitwa polisi kwenda kuhojiwa, siyo kwa uchunguzi wa kutishiwa kwake, bali kwa yale aliyoyasema kuhusu suala la Bandari.

Sasa wala haieleweki kama alikwenda kuhojiwa, na kama alipewa masharti asiseme chochote kuhusu mahojiano hayo?

Katika hali ya kawaida, ilitegemewa vyombo vya habari vimfuate na kumuuliza maswali kuhusu alichoitiwa huko osisini kwa DCI; lakini hata waandishi wa habari na wao hawana hamu ya kupata tarifa wanayoweza kuwafikishia wananchi.

Kama wakili alipewa masharti ya kutozungumzia chochote baada ya mahojiano hayo, maana yake ni kwamba wakili huyo katishwa na kutishika, kiasi kwamba hata haki yake ya kupasha na kupata habari imeingiliwa.

Ni vigumu sana kuamini kuwa wakili msomi kama huyu anaweza kutishika kirahisi namna hiyo.

Kunyamazishwa kwake, kuna maana kwamba ameshughulikiwa na kukubali kusalimu amri katika jambo ambalo wengi waliamini kuwa katika nafasi yake, aliyoyazungumzia yalikuwa ya kweli na umuhimu mkubwa kwa jamii.
Sasa ananyamaza jamii imuelewe vipi?

Hata kama kasalimu amri, si ajitokeze na kusema kuwa hana hamu tena ya kuendelea na yale aliyokuwa ameyasema?

Kunyamaza kwake kunawafurahisha sana aliokuwa kawatupia lawama kuhusika na yanayoendelea na makubaliano hayo ya Bandari.
Je kama aliwekwa ndani?
 
Mwenzako kishatapika huko mpaka wanaomlipa. Kuna cha kuongea tena hapo.

Wewe subiri leo au kesho anatangazwa mshindi wa zabuni rasmi, habari zilizovuja ni DP World. na siku wanayotangazwa wanaanza kazi rasmi.

Hapo sasa!
Wewe FaizaFoxy wewe..!! Unazungumzia zabuni ipi? Ilitangazwa lini na wapi? Hao wazabuni wengine (kama wapo) nao watasaini mnayoyaita makubaliano..??

BTW, umesema habari zilizovuja i za DPW..!! Hivi kuita kuwa zimevuja, inamaanisha hazikutakiwa kuwafikia wananchi..!!??
 
Wewe Bi. Kizee ni mchawi.

Kuendelea kujibishana nawe ni kujishushia heshima; hii imedhihirika kuwa sifa ya ziada uliyo nayo mbali ya ule ulevi wako wa siku zote.

Sasa kwa mfano, tazama uliyoandika hapo juu, mtu mwenye akili timamu ataandika vile na kutegemea majadiliano juu yake?

Inabidi nikuitie mkuu' Mshana jr', anayejulikana kuwa kinara wa wachawi wote hapa JF.

Tokea sasa nakupuuza kama majuha wengi waliomo humu.
Huyo ajuza ni mshirikina balaa
 
Tundu Lisu ameitwa polisi mara ngapi, na aliwahi kutishika?? Mpaka wakamvizia kwa njia za aibu, mwisho Mungu amewaibisha, leo yupo hai na hajabadlika.
Mkae mkijua issue ya bandari ni ya watanganyika wote, hata hao polisi waliomuita wako ambao wako upande wake na pengine ni wengi sana,
Wanajua hawawezi kuwa mapolisi milele, na wanawaona wenzao wengi hasa wastaafu wanavyoteseka mitaani , na wanajua na wao itafika zamu yao.
Ni punguani pekee anayeweza kubeza mchango wa hawa mashujaa waliojitolea kina Nshala, Lisu, Mwambukusi, Dr. Slaa Mbowe na wengine wengi katika kutetea maslahi ya nchi yetu haswa Tanganyika. Hata wakiwatisha wamesaidia wengi kujua kile ambacho wengi tusingekijua tena kwa muda mfupi,na kwa weredi mkubwa.
Labda niulize,kwani
kutozungumza alichoitiwa,aliahidi atasimulia?
 
Wewe FaizaFoxy wewe..!! Unazungumzia zabuni ipi? Ilitangazwa lini na wapi? Hao wazabuni wengine (kama wapo) nao watasaini mnayoyaita makubaliano..??

BTW, umesema habari zilizovuja i za DPW..!! Hivi kuita kuwa zimevuja, inamaanisha hazikutakiwa kuwafikia wananchi..!!??
wewe huelewi hata unachokiongea, rudi ukasomeshwe halafu uje kubishana kiakili.
 
Mwenzako kishatapika huko mpaka wanaomlipa. Kuna cha kuongea tena hapo.

Wewe subiri leo au kesho anatangazwa mshindi wa zabuni rasmi, habari zilizovuja ni DP World. na siku wanayotangazwa wanaanza kazi rasmi.

Hapo sasa!
Mkuu pole sana mwaka huu lazima ujifungue mkataba wa bandari 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Dr Rugemeleza Nshala aliitwa polisi kwenda kuhojiwa, siyo kwa uchunguzi wa kutishiwa kwake, bali kwa yale aliyoyasema kuhusu suala la Bandari.

Sasa wala haieleweki kama alikwenda kuhojiwa, na kama alipewa masharti asiseme chochote kuhusu mahojiano hayo?

Katika hali ya kawaida, ilitegemewa vyombo vya habari vimfuate na kumuuliza maswali kuhusu alichoitiwa huko osisini kwa DCI; lakini hata waandishi wa habari na wao hawana hamu ya kupata tarifa wanayoweza kuwafikishia wananchi.

Kama wakili alipewa masharti ya kutozungumzia chochote baada ya mahojiano hayo, maana yake ni kwamba wakili huyo katishwa na kutishika, kiasi kwamba hata haki yake ya kupasha na kupata habari imeingiliwa.

Ni vigumu sana kuamini kuwa wakili msomi kama huyu anaweza kutishika kirahisi namna hiyo.

Kunyamazishwa kwake, kuna maana kwamba ameshughulikiwa na kukubali kusalimu amri katika jambo ambalo wengi waliamini kuwa katika nafasi yake, aliyoyazungumzia yalikuwa ya kweli na umuhimu mkubwa kwa jamii.
Sasa ananyamaza jamii imuelewe vipi?

Hata kama kasalimu amri, si ajitokeze na kusema kuwa hana hamu tena ya kuendelea na yale aliyokuwa ameyasema?

Kunyamaza kwake kunawafurahisha sana aliokuwa kawatupia lawama kuhusika na yanayoendelea na makubaliano hayo ya Bandari.
Nshalla alifanya makosa ya kumtukana Rais aliomba radhi na kuahidi kuufyata.
 
Usihangaike sana, wewe na wezako niulizeni mtakacho kukifahamu, nimeweka uzi wa watu kuuliza chochote wapemdacho, bofya chini hapo ukaulize"
Ngoja nikutaarifu kama hujui.
Ni hivi, ukinifuatafuata, huku nikishakudharau na kukufahamisha uhayawani wako, maana yake ni kwamba bado unataka nipoteze muda na upumbavu wako humu.

Hiyo ina maana unataka nami niwe chizi kama wewe, na uwezo wa kuwa na hali hiyo ninao sana.

Kwa hiyo hii ni taarifa kwako, ukiendelea kunizongazonga, nitakupa muda huo maalum tuyamalize.
Usiniite tena.
 
Back
Top Bottom