Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Mkuu watu hawapingi uboreshaji wa bandari wala uwekezaji.
Wanapinga kupewa mwarabu bandari bure kwa mkataba wenye vipengele vibovu na vinavyotuondolea uhuru wetu km Taifa.
Hii ni dharau!
 
Punda haendagi Ila Kwa marungu na mabom ya muwasho. Songa Wakili msomi
 
Wapi uliona Magu kasaini mkataba usioeleweka?
 
Sasa hivi ni shamba la nani kama sio la bib
 
Wapi uliona Magu kasaini mkataba usioeleweka?
Magu ndio alijenga SGR ili ichukue mzigo wa Rwanda. Na Kagame Rais wa Rwanda kafungua dry port ya kuweka mzigo unaokusanywa ili uweze kusafirishwa kuja huku Dar kupitia SGR.

Samia anaposema kazi iendelee huwa haeleweki anamaanisha nini, ni muendelezo wa biashara iliyoanza kufikiriwa kufanyika tangu miaka ya 2014-15. Hawa kina Mwabukusi wanapotosha lengo nzima la mradi wa muda mrefu kwa kutumia siasa za chuki, huyo mwanasheria kwa sasa kawekwa kiporo kwanza ili masuala mazito yaweze kufanyika.

Awe mwangalifu kwani anapigana na serikali isiyoonekana kwa macho yetu haya mawili.
 
Mkuu watu hawapingi uboreshaji wa bandari wala uwekezaji.
Wanapinga kupewa mwarabu bandari bure kwa mkataba wenye vipengele vibovu na vinavyotuondolea uhuru wetu km Taifa.
Hii ni dharau!
Huyo mwarabu kwa taarifa yako kaajiri wazungu na weusi wenzetu wenye uzoefu wa kazi na elimu. Usitegemee kuja kumuona mwarabu na kanzu yake akisimamia upakiaji au upakuaji wa makontena, ni wataalam wa mataifa mengine wanaofanya kazi.

Ni sawa na Pep Guardiola na wataalam wenzake pale Man City, wao ndio wapo kazini kuipandisha kiwango timu mpaka imebeba makombe matatu makubwa.

Mwarabu kaja kuonekana siku Guardiola alipopeleka makombe kule Arabuni kwa mmiliki mwenyewe.
 
anachokitafta atakipata. soon atajua maana ya amri jeshi mkuu inamaana gani. ngoja aendelee kufurahisha genge. his days are numbered.
Acheni upumbavu wa kutisha watu, anachokisema wakili yuko sawa maana si sawa kuliacha taifa liteketee kwasababu ya upumbavu wa viongozi wachache walioko madarakani.

Mimi nadhani ifike wakati hata jeshi au majeshi yetu yasipokee order ya kushughulikia kikatili wanaowasema viongozi kwani hili ni taifa letu sote si mali ya viongozi walioko madarakani.
 
Duuh....
Safi kwa kuanza kuelewa kinachopigiwa kelele.
Serikali imeshindwa vipi kuajiri hao wataalamu wa mataifa mengine yenyewe?
Huoni kuwa serikali imeshindwa kutuongoza nayo pia inapaswa ibinafishwe?
 
Hawa jamaa wako backed na system hawa.. si kwa guts hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…