Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Huduma za bandari zikija kuboreshwa msiwe wa kwanza kulete unafiki wa kuanza kusifia. Ndio tulivyo watanzania.

Hakuna kitu kizuri kinachokubalika moja kwa moja mbele ya jamii. Huu ni ulimwengu wa kibiashara, wa kukamata fursa za kiuchumi zinazoibuka.

Huu ujinga wa utanganyika na utanzania unaibuka muda huu eti kisingizio ni suala la bandari, that is stupid argument,

Tuache Malawi na Zambia eti wahamie kule Angola wakati bandari ya kisasa yenye ufanisi wa kisayansi ipo Dar.

Hata kama tunatumiwa na watu basi na tuanza kujivua huu ujinga na kuanza kuiona dunia ya ushindani unaotukabili katika mtazamo halisi.
Mkuu watu hawapingi uboreshaji wa bandari wala uwekezaji.
Wanapinga kupewa mwarabu bandari bure kwa mkataba wenye vipengele vibovu na vinavyotuondolea uhuru wetu km Taifa.
Hii ni dharau!
 
Punda haendagi Ila Kwa marungu na mabom ya muwasho. Songa Wakili msomi
 
Mpumbavu sana huyu Mwabukusi. Nyakati za JPM asingethubutu kufungua mdomo wake kama anavyofanya muda huu.

Siku nyingi tu tungekuwa tumesaini mikataba ya uwekezaji pale ikulu na media zote zingeimba mapambio. Leo anaongea kwa sauti ya juu ni kwa sababu mamlaka za juu zimempa uhuru wa kufanya hivyo.
Wapi uliona Magu kasaini mkataba usioeleweka?
 
Bahati mbaya HUWA TUNASHABIKIA kauli zenye kutugawa na KUCHOCHEA chuki lakini tukiulizana wangapi wana uraia pacha sina hakika kama watakuwa aa kutosha!!!

Huu UJINGA tunaouendekeza tutakuja kulia siku moja....

Nashauri MAMLAKA zifanye kazi zake!!! Wakitokea wajanja wachache wakatuchochea HIZO BANDARI, MADINI NA MBUGA ZA WALIMA vitakuwa shamba la BIBI kama vya KONGO!!! Bahati mbaya wasomi NDIYO WAMEKUWA SABABU YA KUHARIBIKA MAMBO....

Kuna haja gani ya kukosoa kwa MATUSI NA LUGHA ZA KEBEHI? LUGHA ZA KIFEDHULI NA KIBAGUZI???

TUKICHOCHEA HAYA TUTAMBUE tunaigawa nchi pamoja na damu zetu...

Watu waandike PETITION, WAANDAMANE AU KUANDAA MAKONGAMANO lakini kwanza TUILINDE NCHI YETU YA TANZANIA...

Wenzetu akiba lisu, nsala, na wengineo WANAWEZA KUPOKELEWA ULAYA NA KWINGINEKO!! Tujiulize sisi MASSES tukiivunja nchi tutakuwa na pakwenda???

HaTUONI MFANO WA WASOMALI NA WAETHOPIA KILA KUKICHA WANAFIA KWENYE MAKONTENA WAKISAFIRISHWA KWENDA AFRIKA KUSINI???

Watanzania tusiwe wajinga kiasi hiki!!!

these are coordinated attacks and whoever is behind these, I strongly believe has a handsome share benefiting for putting the country into chaos
Sasa hivi ni shamba la nani kama sio la bib
 
Wapi uliona Magu kasaini mkataba usioeleweka?
Magu ndio alijenga SGR ili ichukue mzigo wa Rwanda. Na Kagame Rais wa Rwanda kafungua dry port ya kuweka mzigo unaokusanywa ili uweze kusafirishwa kuja huku Dar kupitia SGR.

Samia anaposema kazi iendelee huwa haeleweki anamaanisha nini, ni muendelezo wa biashara iliyoanza kufikiriwa kufanyika tangu miaka ya 2014-15. Hawa kina Mwabukusi wanapotosha lengo nzima la mradi wa muda mrefu kwa kutumia siasa za chuki, huyo mwanasheria kwa sasa kawekwa kiporo kwanza ili masuala mazito yaweze kufanyika.

Awe mwangalifu kwani anapigana na serikali isiyoonekana kwa macho yetu haya mawili.
 
Mkuu watu hawapingi uboreshaji wa bandari wala uwekezaji.
Wanapinga kupewa mwarabu bandari bure kwa mkataba wenye vipengele vibovu na vinavyotuondolea uhuru wetu km Taifa.
Hii ni dharau!
Huyo mwarabu kwa taarifa yako kaajiri wazungu na weusi wenzetu wenye uzoefu wa kazi na elimu. Usitegemee kuja kumuona mwarabu na kanzu yake akisimamia upakiaji au upakuaji wa makontena, ni wataalam wa mataifa mengine wanaofanya kazi.

Ni sawa na Pep Guardiola na wataalam wenzake pale Man City, wao ndio wapo kazini kuipandisha kiwango timu mpaka imebeba makombe matatu makubwa.

Mwarabu kaja kuonekana siku Guardiola alipopeleka makombe kule Arabuni kwa mmiliki mwenyewe.
 
anachokitafta atakipata. soon atajua maana ya amri jeshi mkuu inamaana gani. ngoja aendelee kufurahisha genge. his days are numbered.
Acheni upumbavu wa kutisha watu, anachokisema wakili yuko sawa maana si sawa kuliacha taifa liteketee kwasababu ya upumbavu wa viongozi wachache walioko madarakani.

Mimi nadhani ifike wakati hata jeshi au majeshi yetu yasipokee order ya kushughulikia kikatili wanaowasema viongozi kwani hili ni taifa letu sote si mali ya viongozi walioko madarakani.
 
Huyo mwarabu kwa taarifa yako kaajiri wazungu na weusi wenzetu wenye uzoefu wa kazi na elimu. Usitegemee kuja kumuona mwarabu na kanzu yake akisimamia upakiaji au upakuaji wa makontena, ni wataalam wa mataifa mengine wanaofanya kazi.

Ni sawa na Pep Guardiola na wataalam wenzake pale Man City, wao ndio wapo kazini kuipandisha kiwango timu mpaka imebeba makombe matatu makubwa.

Mwarabu kaja kuonekana siku Guardiola alipopeleka makombe kule Arabuni kwa mmiliki mwenyewe.
Duuh....
Safi kwa kuanza kuelewa kinachopigiwa kelele.
Serikali imeshindwa vipi kuajiri hao wataalamu wa mataifa mengine yenyewe?
Huoni kuwa serikali imeshindwa kutuongoza nayo pia inapaswa ibinafishwe?
 
WAKILI BONIFACE MWABUKUSI;KAMA HAMTATUSIKILIZA,TUTAZUNGUMZA LUGHA MTAKAYOTUSIKILIZA,HATUTARUHUSU MZANZIBARI KUFANYA MAMBO YA HOVYO KWENYE MALI ZA TANGANYIKA.

"Wazee wangu wa Mbeya nipo hapa kuwahakikishia Tanganyika hailiwi tena,tutafuatilia hatua kwa hatua kwenye mikataba ya Mali zote za Tanganyika" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba unatakiwa ujisimamie na ujitetee,ila watu wanautetea bila "baseline" za data na facts kwenye mkataba huo,hakuna research wala data, mkataba hauna data ambazo ni measured kisayansi watu wanacheza na maneno tu ambayo hayapo kwenye mkataba" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba wa bandari ni batili, chochote kilichofanywa nje ya sheria na nje ya katiba kirekebishwe" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar,hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Tanganyika,kama ambavyo Mtanganyika hawezi kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Ndoa ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ndoa ya utotoni sasa tumekua tunataka tuongee tukubaliane Mali za Tanganyika ziwe chini ya Mtanganyika na Mali za Zanzibar ziwe chini ya Mzanzibari" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu alitudanganya kuhusu kifo cha Hayati Rais John Pombe Magufuli na hajawahi kuomba radhi,na leo anatudanganya kuhusu mkataba wa bandari,akae pembeni kumsaidia Rais" Wakili Boniface Mwabukusi

"Waziri Mkuu atujibu,sheria sura 449 na sheria sura 450 kuhusu Ulinzi wa rasilimali za nchi na kuhusu ushughulikiwaji wa vifungu vyenye utata walizifuata,je vipengele vya mkataba wa bandari vinaoana na vipengele hivi vya sheria yetu" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu atujibu,kwa nini bunge linataka kubadili sheria sasa hivi ziendane na mkataba huu wa bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tuliibinafsisha Tanesco kwa Net Solution tulipata faida gani na leo Tanesco ya nani? Tulileta watu TRL wakaishia kubeba vichwa vya treni kurudi navyo India,tulifanya hivyo hivyo kwa NBC kuuzwa bei ya kutupwa,na leo mnatuambia mna muujiza kwenye kuibinafsisha bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Kama mkataba ni sahihi,Waziri Mkuu anatuambiaje tukusanye maoni,nani anakusanya maoni,yaende wapi,ya nini? kama mkataba tayari umeshapita" Wakili Boniface Mwabukusi

"Wakati nchi yetu ina Kiongozi mwenye element za Uzalendo watu fulani hawakuonekana kabisa,sasa hivi wamerudi wanatukana hadi Mahakama, Watanzania angalieni walioko nyuma ya huu mkataba"Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kila uovu juu ya Tanganyika tutaukabili kwa jina lake na kila muovu tutamkabili kwa jinsi anavyokuja,hii ni nchi yetu hatutamuchia mtu mwingine aitetee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mabadiliko ya sheria yanayokwenda kufanyika ni matusi kwa Tanganyika,narudia tena Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tunatoa onyo kwa Kiongozi mwingine kudhani anaweza kuingia mikataba ya kuuza nchi akabaki salama,wasituchezee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tunawaomba Watanzania wa dini zote,Waislamu, Wakristo,Wachungaji na Mashehe na WA jadi,tufunge tarehe 14,15,16 kuomba mapenzi ya Mungu yakafanyike kwa Tanganyika na Tanzania,ahsanteni sana"Wakili Boniface Mwabukusi
Hawa jamaa wako backed na system hawa.. si kwa guts hizo
 
Back
Top Bottom