Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala(PhD) aitwa Polisi kutokana na maoni yake kuhusu bandari

Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala(PhD) aitwa Polisi kutokana na maoni yake kuhusu bandari

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Barua hiyo ya wito kutoka ofisi ya DCI inamtaka Dkt. Nshala kufika kwa ajili ya mahojiano


Ofisi hii inafanya uchunguzi kuhusiana na kauli ulizotoa tarehe 03 Julai 2023 na kisha kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam

Ili tuwe kukamilisha uchunguzi wetu, ofisi hii inakutaka ufike ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Kanda Maalum Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2023 saa 09:00 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya mahojiano.


Nshala.jpg



Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
  2. Rugemeleza Nshala: Tutafungua Kesi kupinga Mkataba wa DP World na Tanzania
  3. Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World
 
Watu wanaosifia na kutetea mkataba ni sawa,wanaokosoa na kusema mkataba mbovu wanatishiwa maisha na kushtakiwa.

Rais Samia huu ni udikteta,watu wasilazimishwe kusifia na kupongeza,kazi hiyo waachie chawa wa Mama na chawa wa CCM.

Raisi hivi punde ulionekana ukikosoa utendaji wa serikali kuhusu malipo ya ndege hadi ukatamaka maneno "stupid" je nawe utaitwa Polisi?!!
 
Rais mstaafu wa TLS amepokea wito wa polisi kanda maalumu Dar es Salam kwa mohojiano kufuatia maoni yake naamna mkataba wa kitapeli dhidi ya waarabu

Sisi Watanganyika tukae tujiulize kosa la Dr.nshala ni lipi?

Kosa lake kuhoji bandari kutaka kuuzwa kwa waarabu?


Watanganyika tuamke wanalenga kutuziba mdomo midomo


Tujitokeze barabarani kupinga dr nshala kuhojiwa hii inatoa inshara mbaya sana

Km viongozi wamekula pesa za waarabu wawajibike wao sio kutesa wananchi wasio na hatia

Jamani watanganyika tujitokeze kupinga huu uonevu wa dola kupitia police
 
Nikadhani wanamuita atoe taarifa kuhusu kutishiwa uhai wake, kumbe wanamuita akatoe maelezo kwanini alitoa maoni yake, kwani DCI hajawahi kuisoma Katiba ya JMT 1977 kuhusu uhuru wa kutoa maoni?

Kwa hii taarifa, hapa ndio unapata picha kabisa, ni wakina nani waliomtishia maisha Dr. Nshalla, hivi vitisho vyao vimepitwa na wakati, werevu hawawezi kuona uozo mahali halafu waufumbie macho kizembe, hiyo ni dhambi.
 
Karamagi lazima ka sponsor hizo movements zote
Karamagi ndio architect aliekuwa nyuma ya Tibaijuka, Dr Nshala and god knows who else. Mtu ambae $5m hela ya chai kwake ashindwi kuandaa cinema yake.

Hila JF kiboko story yote unaipata hapa hapa ukiwa unasoma comments za wengine kwa makini tu na kuuanganisha dots.
 
Back
Top Bottom