Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala(PhD) aitwa Polisi kutokana na maoni yake kuhusu bandari

Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala(PhD) aitwa Polisi kutokana na maoni yake kuhusu bandari

tatizo la Nshala anaongea kwa jazba sana jambo linalo poteza uwezo wake wa kufikiria kwa kina.
kwa mtu mwenye taaluma kama yake hapaswi kupayuka kwa mihemko ya kisiasa.

kila raia anao uhuru wa kutoa maoni lakini kumbuka mipaka iliyo wekwa, ukivuka mipaka uhuru wako unapotea na hivyo utashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

tatizo watu wanatumia uhuru wao vibaya kwa kuvunja uhuru wa wengine au mamlaka
 
Dk Nshalla hamtamuweza, wala ccm police haita wasaidia, kitu bora zaidi ni kuchukua maoni ya wananchi na kurekebisha mkataba, kama kuna nia ya dhati ya uwekezaji kurekebisha mkataba kwa kuondoa vipengele tata lina ugumu gani? mkiishiwa hoja mnaomba msaada wa police?, maoni ya wananchi na watalaam mbalimbali ni kwa ajiri ya kuboresha, ukiwa mgeni Tanzania ndo unaweza shabibikia hizi mikataba, lakini kama upo Tanzania miaka yote, mikataba ya uwekezaji imeleta majanga makubwa.
 
1689065410757.png
=
Mkurugenzi wa upelelezi makosa ya jinai (DCI), ametoa wito wa polisi kwa Dkt. Rugemeleza Nshala kufika ofisi za ZCO (Dar es Salaam) kwa mahojiano kwa kauli alizotoa kuhusu mkataba wa uuzwaji wa bandari Kwa DP WORLD.

==
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA

Dr Rugemeieza Albert Nshaja.
Lawyers Environmental Action Team (LEAT).
Mazingira House — Mazingira street.
S.LP 12605,
DAR ES SALAAM.

Yah. WITO WA POLISI JAI-ADA; CID/HQ/PE 57/2023

Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu.

2. Ofisi hii inafanya uchunguzi kuhusiana na kauli ulizotoa tarehe 03 Julai 2023 na kisha kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na mkataba wa uwekezali katika bandarl ya Dar es Salaam,

3. Ili tuweze kukamilisha uchunguzi wetu, ofisi hii inakutaka ufike ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2023 saa 09.00 asubuhi bila kukosa kwa ajlli ya mahojiano.

4. Nawasilisha kwa utekelezaji.
 
Kwa moves hizi. Hii Serikali itaondoka 2025. Uchaguzi utakuwa wa moto. Hamna serikali Afrika imewahi kupambana na Wanasheria, Wanaharakati na Viongozi wa dini wakashinda. Haya mapambano siyo ya kisiasa. Hii ni civil movement.
 
Watu wanaosifia na kutetea mkataba ni sawa,wanaokosoa na kusema mkataba mbovu wanatishiwa maisha na kushtakiwa.

Rais Samia huu ni udikteta,watu wasilazimishwe kusifia na kupongeza,kazi hiyo waachie chawa wa Mama na chawa wa CCM.

Raisi hivi punde ulionekana ukikosoa utendaji wa serikali kuhusu malipo ya ndege hadi ukatamaka maneno "stupid" je nawe utaitwa Polisi?!!

Mbona nyinyi mumetuvamia na kuichukuwa nchi yetu Zanzibar na kuwa ngawira yenu ?? Hilo hamlioni au mkuki kwaa nguruwe tu na mlikuwa mnasema wanaohoji muungano washughulikiwe ?+
 
Taifa letu lipo ktk mtihani mgumu sana..tutavuka si Kwa akiri wala nguvu, Wala siasa Bali neema kubwa na upendo wa Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na rehema.

Msamaha Kwa watukoseao ni utii Kwa Mwenyezi Mungu..

Nawaombea viongozi wetu wajaariwe unyenyekevu na kujishusha Kwa faida ya Taifa..

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Barua hiyo ya wito kutoka ofisi ya DCI inamtaka Dkt. Nshala kufika kwa ajili ya mahojiano


Ofisi hii inafanya uchunguzi kuhusiana na kauli ulizotoa tarehe 03 Julai 2023 na kisha kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam

Ili tuwe kukamilisha uchunguzi wetu, ofisi hii inakutaka ufike ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Kanda Maalum Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2023 saa 09:00 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya mahojiano.




Pia soma:
Rugemeleza Nshala: Tutafungua Kesi kupinga Mkataba wa DP World na Tanzania
Dkt. Rugemeleza Nshala: Nimetishiwa maisha baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World
Saa 09:00 Asubuhi
 
Back
Top Bottom