Barua hiyo ya wito kutoka ofisi ya DCI inamtaka Dkt. Nshala kufika kwa ajili ya mahojiano
Ofisi hii inafanya uchunguzi kuhusiana na kauli ulizotoa tarehe 03 Julai 2023 na kisha kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam
Ili tuwe kukamilisha uchunguzi wetu, ofisi hii inakutaka ufike ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Kanda Maalum Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2023 saa 09:00 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya mahojiano.
Nikadhani wanamuita atoe taarifa kuhusu kutishiwa uhai wake, kumbe wanamuita akatoe maelezo kwanini alitoa maoni yake, kwani DCI hajawahi kuisoma Katiba ya JMT 1977 kuhusu uhuru wa kutoa maoni?
Kwa hii taarifa, hapa ndio unapata picha kabisa, ni wakina nani waliomtishia maisha Dr. Nshalla, hivi vitisho vyao vimepitwa na wakati, werevu hawawezi kuona uozo mahali halafu waufumbie macho kizembe, hiyo ni dhambi.
Wakili inawezekana alikuwa na nia njema ya kufikisha ujumbe ila uchaguzi wake wa maneno haukuwa mzuri, aliongea akiwa emotional akapoteza rationality. Uhuru wa kutoa maoni una misingi na mipaka yake sio kufyatuka tu