Marekani, nchi ya makazi yangu, nchi iliyoendelea kiuchumi kwa kupitia figisu nyingi sana na kuweka misingi ya sheria, imejiwekea sheria hivi.
Mimi Kiranga, raia, nikitaka kuchukua picha yako Nyani Ngabu, raia mwenzangu usiye na cheo, halafu niiweke picha ike kwenye T-Shirt. Labda tuseme wewe Nyani Ngabu ni firefighter uneokoa watu, nikiweka picha yako kwenye T-Shirt, ama kwa kuuza ama kwa kuvaa mimi mwenyewe, ama kwa kukusifu, ama kwa kukutukana, wewe una uhuru wa kunishitaki na kunishinda mahakamani nisiweke picha yako. Ukashinda kesi, mimi nifungwe au nilipe faini, na nikatazwe kutumia picha yako.
Kwa nini? Kwa sababu wewe ni private citizen. Una privacy rights kubwa sana.
On the same token.
Nikiamua kuchukua picha ya Donald Trump. Niziweke kwenye T-Shirt. Ama kwa kumsifu, ama kwa kumtukana. Donald Trump na serikali yake hawana haki ya kisheria ya kunukataza.
Nina ruhusa za kuchapisha T-Shirt za kumtukana Donald Trump, nikaweka picha yake na maneno "Donald J. Trump is a douchebag".
Kisheria, hiyo ni sehemu ya free speech tu. Hakuna sheria itakayonikataza.
Raia wa kawaida anatetewa na sheria kuliko rais katika hili.
Kwa sababu, rais alikuwa na uchaguzi, awe raia wa kawaida aachiwe maisha yake yawe private bila figisu na maneno mengi, au atake uongozi, kwa kujua "ukubwa gunia la chawa", pamoja na figisu zote zinazokuja na uongozi.
Akachagua figisu. Hakuchagua privacy.
Sasa keo watu wamemcheka suti msulupwete tu?
Sasa akitukanwa kikwelikweli serikali itaweza kuvumilia?
Tuna umasikini kwa sababu nyingi sana.
Na serikali yenyewe ina ji undermine. Haijui kula na kipofu usimshike mkono.
Sasa wanaendesha serikali kisiri na kujuwekea mazingira ya kuiba mabilioni, watu hawahoji.
Unapoanza kukamata watu wanaomcheka rais kwa sababu ya suti msulupwete, hapo ndipi unaanza kumgusa mkono kipofu unayekula naye.
Wanaiba kura, wanaiba hela, hata kuwaachia uhuru wa msingi tu watu wacheke wasahau machungu wanashindwa?
Sent from my typewriter using Tapatalk