Mc Tilly Chizenga
JF-Expert Member
- Feb 7, 2012
- 4,641
- 3,680
Unacheka , unaendelea na maisha yako, kujirekodi ukiwa unacheka na kuisambaza hapo itabidi dhamira yako ya kufanya hayo mawili yaani kujirekodi na kuisambaza aingaliwe , je Ni dhamira ovu?Lione jioga! Ukiona kitu kinakuchekesha unafanyaje?
Ukweli kwamba watu wengi sana wana support ujinga huu, hata hapa JF, na watu tukieleza huu ni ujinga tunapingwa kwa cognitive dissonance za kila aina, unaeleza mengi kuhusu kwa nini sisi kama nchi bado tunaelea katika wimbi wa umasikini wa kutupwa.Ujinga na umasikini. Ukijitambua huwezi kuwa na akili za kishamba hivo.
Yaani kumcheka kiongozi ni kosa. Wallahi tunapo elekea ni shimoni
Sent using Jamii Forums mobile app
vichekesho mnavyoviona mitandaoni vna tofauti gani na hiyo picha. Sema mmeshakubali kuwa watumwa wa Jwe. Slaves, umekubali kuwa mtumwa!Unacheka , unaendelea na maisha yako, kujirekodi ukiwa unacheka na kuisambaza hapo itabidi dhamira yako ya kufanya hayo mawili yaani kujirekodi na kuisambaza aingaliwe , je Ni dhamira ovu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Marekani, nchi ya makazi yangu, nchi iliyoendelea kiuchumi kwa kupitia figisu nyingi sana na kuweka misingi ya sheria, imejiwekea sheria hivi.
Mimi Kiranga, raia, nikitaka kuchukua picha yako Nyani Ngabu, raia mwenzangu usiye na cheo, halafu niiweke picha ike kwenye T-Shirt. Labda tuseme wewe Nyani Ngabu ni firefighter uneokoa watu, nikiweka picha yako kwenye T-Shirt, ama kwa kuuza ama kwa kuvaa mimi mwenyewe, ama kwa kukusifu, ama kwa kukutukana, wewe una uhuru wa kunishitaki na kunishinda mahakamani nisiweke picha yako. Ukashinda kesi, mimi nifungwe au nilipe faini, na nikatazwe kutumia picha yako.
Kwa nini? Kwa sababu wewe ni private citizen. Una privacy rights kubwa sana.
On the same token.
Nikiamua kuchukua picha ya Donald Trump. Niziweke kwenye T-Shirt. Ama kwa kumsifu, ama kwa kumtukana. Donald Trump na serikali yake hawana haki ya kisheria ya kunukataza.
Nina ruhusa za kuchapisha T-Shirt za kumtukana Donald Trump, nikaweka picha yake na maneno "Donald J. Trump is a douchebag".
Kisheria, hiyo ni sehemu ya free speech tu. Hakuna sheria itakayonikataza.
Raia wa kawaida anatetewa na sheria kuliko rais katika hili.
Kwa sababu, rais alikuwa na uchaguzi, awe raia wa kawaida aachiwe maisha yake yawe private bila figisu na maneno mengi, au atake uongozi, kwa kujua "ukubwa gunia la chawa", pamoja na figisu zote zinazokuja na uongozi.
Akachagua figisu. Hakuchagua privacy.
Sasa keo watu wamemcheka suti msulupwete tu?
Sasa akitukanwa kikwelikweli serikali itaweza kuvumilia?
Tuna umasikini kwa sababu nyingi sana.
Na serikali yenyewe ina ji undermine. Haijui kula na kipofu usimshike mkono.
Sasa wanaendesha serikali kisiri na kujuwekea mazingira ya kuiba mabilioni, watu hawahoji.
Unapoanza kukamata watu wanaomcheka rais kwa sababu ya suti msulupwete, hapo ndipi unaanza kumgusa mkono kipofu unayekula naye.
Wanaiba kura, wanaiba hela, hata kuwaachia uhuru wa msingi tu watu wacheke wasahau machungu wanashindwa?
Sent from my typewriter using Tapatalk
Kusambaza habari ni haki ya kikatiba.Unacheka , unaendelea na maisha yako, kujirekodi ukiwa unacheka na kuisambaza hapo itabidi dhamira yako ya kufanya hayo mawili yaani kujirekodi na kuisambaza aingaliwe , je Ni dhamira ovu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ulimbukeni ni kutaka kumfunga mtu kwa sababu kamcheka rais.Ulimbukeni wa mitandao ya kijamii ili kupata likes na views ndio kinapelekea watu ku-share kila kitu.
Inatosha ukicheka na kufurahi binafsi, alichofanya Idris asingeweza fanya kwa baba yake au ndugu.
HOPE>fear
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kusambaza habari ni haki ya kikatiba.
Kama kitu kinachekesha unatakiwa kuwasambazia wenzako.
Usiwe mchoyo mpaka wa vichekesho.
Sent from my typewriter using Tapatalk
Hivi comedians wa Tanzania wakiamua kufanya Magufuli Roast itakuwaje?
Sent from my typewriter using Tapatalk
Haha, eti roast beef.Hahahaaa mazee....seriously?
Wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kutaka kumuua Rais na kui roast nyama yake [kama roast beef] sitoshangaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Maana jamaa ni washamba sana aisee.
Na wewe kuwa mwangalifu usijepews ban humu kwa sababu ya kuzungumzia kum-roast Magufuli.
Waweza shitakiwa for conspiracy to aid and abet in the attempted murder of one JPM and cooking him thereafter in order to consume him for a meal....
Magufuli angeweza kumaliza hili sakata kwa urahisi sana.
Angemwita Idris Ikulu, akaongea naye, kisha akatoa statement kwenye TV akiwa anacheka na Idris, akiwaambia Watanzania ukweli tu kwamba, kwa mfano, yeye Magufuli ni mtoto wa wakulima ambaye hakuwa na suti za anasa, hiyo suti aliazima last minute kwa kufanya kazi tu nandiyo maana imempwaya hivyo.
I am sure hiyo suti ina explanation iliyo very interesting. Labda kairithi. Labda alioeea bula kupimwa. Hiyo suti si ya kushonesha kwa vipimo.
Angesema tu kwamba yeye alikuwa anajali kazi kuliko mavazi.
Hilo linge resonate na zaidi ya 90% ya Watanzania, wangemuelewa.
Uhuru wa watu kujieleza ungelindwa, na rais angepangua utani kwa kujichekesha na "mtesi" wake.
Sasa hivi rais kukaa kimya inaonekana kama anafurahia yanayotokea, au yeye ndiye kaagiza.
Sent from my typewriter using Tapatalk
Nyerere alivyotoka Scotland alikuwa anavaa vikaptula vyake ambavyo kwa wazee wa pwani vilikuwa culturally inappropriate. Mpaka leo nikienda Zanzibar huku nimevaa cargo shorts wenyeji wangu wananisema navaa kama mtalii.Sawa kabisa.
Or he can just self-deprecate. He can say that was the shit back then...he looked fly and Janeth fell for him [emoji23].
More importantly, they can let Idris go [if they haven’t already] and let him be.
No crime was committed there.
And honestly, many of us have photos from way back when that we can look at today and be somewhat embarrassed about or laugh at.
Wewe ni nani mpaka umpe into wakati ni boya fokonyolewaji team praise.Washauri wa Idriss sijui ni akina nani! Ile video tokea nilipoiona nilijua itamletea shida, kwa jinsi picha zile za ‘TBT’ za Rais zilivyoenea mitandaoni huku wengi wakifanya dhihaka haikufaa yeye kujifunga kibwebwe kuchekelea waziwazi.
Kwa hili umelivagaa Idriss, umepatikana...
Ni wazi Rais hakupendezwa na dhihaka zile, utayabeba machungu yake wewe mwenyewe!
Ukiponea hili uache kiherehere cha kurukia mambo, cheap stunts zitakuponza!
Sent from my iPhone using JamiiForums
Kuna hoja nzito zaidi ya Idris na Magufuli.Washauri wa Idriss sijui ni akina nani! Ile video tokea nilipoiona nilijua itamletea shida, kwa jinsi picha zile za ‘TBT’ za Rais zilivyoenea mitandaoni huku wengi wakifanya dhihaka haikufaa yeye kujifunga kibwebwe kuchekelea waziwazi.
Kwa hili umelivagaa Idriss, umepatikana...
Ni wazi Rais hakupendezwa na dhihaka zile, utayabeba machungu yake wewe mwenyewe!
Ukiponea hili uache kiherehere cha kurukia mambo, cheap stunts zitakuponza!
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hawa ndiyo wale niliokuambia kuwa wanagandamizwa ila bado wanaunga mkono juhudi za ugandamizaji za wanaowagandamiza!Kuna hoja nzito zaidi ya Idris na Magufuli.
Kuna hoja za uhuru wa watu kucheka vitu vinavyochekesha katika nchi yao.
Uhuru wa msingi unaotetewa kikatiba unavunjwa.
Kwa hilo, Idris anaonesha mapungufu makubwa sana katika mifumo yetu, mapungufu ambayo yanachangia katika umasikini wetu.
Nchi ambayo wananchi hawaruhusiwi kumcheka rais anayevaa suti msulupwete, rais akiiba hela, wananchi wataruhusiwa kusema rais kaiba hela?
Au wataambiwa kusema hivyo ni kinyume cha sheria na ni kumdhalilisha Mkuu wa Nchi?
Sent from my typewriter using Tapatalk
Comedy ni nini na kumdhalilisha mtu ni nini?Nimeangalia ile sio commedy, alilenga kumdhalilisha Mkuu wa Nchi lazima achunguzwe huwenda kuna mtu anamtumia nyuma ya pazia
Exposure nayo ni issue.Hawa ndiyo wale niliokuambia kuwa wanagandamizwa ila bado wanaunga mkono juhudi za ugandamizaji za wanaowagandamiza!
nyie ma CCM wapuuzi kweli kweli, kama nyie ni waoga msidhan kila mtu ni muoga kama nyie, kuicheka picha tuu eti nako ni kosaa??? duuu yajayo yanafurahisha!
sawa lakini huo ujinga wake akafanye kwa billnas ndo saizi yake sio kwa kiongozi wa nchi jamani