Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Amekuwa Wakili wa Mamluki walioishitaki Chadema akiwemo Lembrus Mchome anayepinga kufukuzwa
Mndeme amekuwa ofisi ya Katibu Mkuu na alipelekwa bungeni ofisi ya KUB
Kimsingi, Wakili ana wajibu wa kitaaluma kumtetea mteja yeyote anayemwajiri, asikiuke sheria au kanuni za maadili ya taaluma (Advocates Remuneration and Professional Conduct Rules).
Lakini ameenda kuwatetea ‘wahuni’ ambao wamekwenda Mahakamani kuishtaki CHADEMA.
Katika jambo hili, angeweza kutazama na kupima kuhusu mgongano wa Kisiasa na kimaadili (Political & Moral Dilemma) na kuchagua kati ya misingi ya maadili na utu dhidi ya maslahi au ulingo wa kisiasa.
Je, unaweza kuwa wakili upande wa mtu ambaye anamshtaki Baba yako au Mama yako kwa sababu ya kulipwa pesa za uwakili? Kwanini nasema hivyo?
Wakili Jonathan Wilfried Mndeme amekuwa:
1. Msaidizi wa Katibu wa Mbunge wa Ubungo (John Mnyika)
2. Ufadhili wa kusoma masomo ya Masters ya sheria - CHADEMA HQ
3. Ufadhili wa masomo (Law School) - CHADEMA HQ
4. Ofisa katika Kambi rasmi ya Upinzani ubungeni (KUB)
5. Katibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB)
6. Msaidizi binafsi wa Mwenyekiti Freeman Aikaeli Mbowe.
7. Afisa wa sheria CHADEMA, Makao Makuu.
8. Mkurugenzi wa Sheria CHADEMA, Makao Makuu.
9. Mjumbe wa Sekretariati CHADEMA, Makao Makuu.
10. Umeshiriki marekebisho (amendments) Katiba ya chama
Mtu aliyelelewa, kufadhiliwa masomo, na kupewa nafasi za juu za uongozi na taasisi (ndani ya CHADEMA na KUB), jamii na wanachama wa taasisi yetu tulimtazama kama “mtoto wa nyumbani”.
Wakili aliyejengwa na taasisi kusimama upande wa pili dhidi ya waliokuwa viongozi au walezi wake ni usaliti wa kiitikadi na ukosefu wa shukrani, hata kama kisheria una haki ya kufanya hivyo.