Wakili Madeleka awaanika 'wasiojulikana' kwa majina

Wakili Madeleka awaanika 'wasiojulikana' kwa majina

Huyu wakili mwanasiasa huwa simwelewi kabisa
Kweli mko wengi humu JF! Mnatetea Mtanzania kumfanyia unyama Mtanzania mwenzake eti kisa? Ni mpinzani, anaikosoa serikali!

Mlivyojipanga humu mnatisha! Mara mnamtaka Wakili Madeleka atoe ushahidi, mara aripoti polisi, mara anayo matatizo ya akili...my God!

Na pia mnao ujasiri wa ajabu...eti mkishafanya yote hayo bado mnao uthubutu wa kurudi nyumbani kwa wake zenu na watoto wenu!

Mbona huku ni kuinajisi si tu familia zenu, kizazi chenu na ukoo wenu wote na kujipa laana ya bure! Kweli kuwa CCM kwahitaji roho ngumu!
 
Huyu kama vile ana ugonjwa wa kichaa, ntashangaa kama Kuna watu wanampa kesi awawakilishe mahakamani.

Audio clip inaonyeshaje mtu anangolewa jino? Analawitiwa? Audio?
Na wewe usijifanye kichwani umeweka makamasi na siyo ubongo. Amesema ''sauti zinasika'' na hakusema zinaonyesha. You are more than idiot! Kama umekasirika sana mfuate bwanako Magufuli kule alikokwenda!
 
Huyu Bwana achoki tu, shukuru Mungu KILA jambo wakati mwingine kukaa jela kumbe Mungu kakuepusha na hatari au kifo.
 
Kweli mko wengi humu JF! Mnatetea Mtanzania kumfanyia unyama Mtanzania mwenzake eti kisa? Ni mpinzani, anaikosoa serikali!

Mlivyojipanga humu mnatisha! Mara mnamtaka Wakili Madeleka atoe ushahidi, mara aripoti polisi, mara anayo matatizo ya akili...my God!

Na pia mnao ujasiri wa ajabu...eti mkishafanya yote hayo bado mnao uthubutu wa kurudi nyumbani kwa wake zenu na watoto wenu!

Mbona huku ni kuinajisi si tu familia zenu, kizazi chenu na ukoo wenu wote na kujipa laana ya bure! Kweli kuwa CCM kwahitaji roho ngumu!
Halafu hawa wote ni vilaza walioshindwa maisha wakapenyezwa kwenye vikundi vichafu vya system wakati wa Magufuli. Bado wako kwenye nyakati kama zile za Iddi Amini na vikundi vyake vya mauaji. Primitive wanaodhani kuwa kwenye vyombo vya usalama basi ni tiketi ya kuua na kutesa unavyotaka. Waache wadhani ni invincibles. Na thread zote zinazoanzishwa za kumtetea Sabaya ni hivi vikundi vinahusika.
 
Kwa hiyo hata hii miili iliyookotwa itakuwa ni hao vijana majina Yao pale CLUBHOUSE ni commando,Jimmy Jones,Mayi,A B,na Ado November
 
Na wewe usijifanye kichwani umeweka makamasi na siyo ubongo. Amesema ''sauti zinasika'' na hakusema zinaonyesha. You are more than idiot! Kama umekasirika sana mfuate bwanako Magufuli kule alikokwenda!
Madereka ni kichaa, hata kesi ya Mbowe, aliomba ajiunge, kibatala akasema hataki mental case, itaharibu kesi
 
Haya yote yanaelekea mwishoni wala msihofu watanzania hawa wasiojulikana kwanza tutambue kwamba ni waoga ndio maana wakifanya matukio hayo wanajificha wakati wa utekelezaji,maana yake nini,hata wao hawapendi kutendewa hivyo.MUNGU hajawahi shindwa kamwe.
 
WASIOJULIKANA WAANIKWA HADHARANI.

Kweli dunia ni eneo dogo sana nimeamini ya kwamba unaweza kutembea na uovu lakini usifikie nao mbali. Huyu Mungu ni wa ajabu sana pale anapoamua kushughulika na fedhuli na wenye roho chafu.

Katika hali isiyokua ya kawaida, Wakili Msomi nchini ndugu Petter Madeleka kupitia mazungumzo ya Mtandao wa Clubhouse amewataja kwa majina Vijana waliomteka kwa majina yao na kusema ya kwamba anawajua mpaka sura zao.

Ndugu Madeleka ambaye ni wakili wa kujitegemea wa ameyataja majina ya Commando, Jimmy Jones na Ado ambaye alikua mwanasheria wa shirikisho la wasanii nchi kua ni watu waliomteka, Wakili amethibisha kwa kusema ya kwamba walipomteka walikua wakimwekea Audio Clips zenye sauti za watu wakilia wakiliwalawitiwa, wengine wakipigiwa misumari, wengine waking'olewa meno, wengine wakipigwa short ya umeme ili aweze kutishika, amesema aliwatambua kwa majina hayo kwa sababu kwenye sauti hizo za Audio wakiwa wanafanya unyama huo wanatajana kwa majina hayo hayo ya Commando, Jimmy Jones na Ado ambayo pia wanayatumia kwenye mtandao wa Clubhouse na sauti zao hizo hizo.

Jimmy Jones, Commando, Ado, Jordan Balindo na Wengine wanatajwa kujifanya kua ni waanzilishi wa mijadala mbali mbali katika mtandao wa Clubhouse kupitia chamber zao za PATRICEUMUMBA na COURT ROOM lengo lao likiwa ni kuhamisha mijadala ya kitaifa inayoendelea nchini, wanaweza kujifanya kua wako serious sana kuleta jambo lenye kuibua hisia na kujifanya wana uchungu sana kumbe lengo lako ni kuhamisha mijadala ya kitaifa.

Vijana hawa nao wanatajwa umri wao kua miaka 30-40 wapo katika mitandao yote ya kijamii ikiwa Tweeter, Makundi ya Watsap, Instagram, Facebook nk.Kazi yao ni kuilinda CCM na serikali yao.

Mungu anendlee kuwaomumba na wengine wapuuzi wenye tabia kama hizi. Isiwe tunahangaika na suala la maridhiano lakini hawa hawalali wanafanya kazi za kukwamisha juhudi Mheshimiwa Rais.
View attachment 2325327
Mm namfahamu jamaa mmoja anaitwa Addo, ni kada lialia wa chama, ni kiongozi wa wasanii, ni mwinjilisti, shabiki wa yanga na mani yuu. Bila shaka siye aliyetajwa hapa
 
Huyo wakili kuna uwezekano mkubwa akawa hayupo sawa kisaikolojia anahitaji msaada.

Anaumwa ugonjwa wa kutafuta umaarufu.
Kama magufuli alikufa ye anaogopa nini...eti mzee
 
Mm namfahamu jamaa mmoja anaitwa Addo, ni kada lialia wa chama, ni kiongozi wa wasanii, ni mwinjilisti, shabiki wa yanga na mani yuu. Bila shaka siye aliyetajwa hapa
Mimi simfahamu huyo Addo na hata nikikutana naye siwezi kumtambua lakini haya majamaa makatili ni majitu ya kawaida sana kwa muonekano.

Sasa subiri siku yakupate...

Hayana pembe wala umbo za kutisha ila siku moja wao akitambulishwa kwako, huwezi kuamini kwani anaweza kuwa rafiki, jirani au hata ndugu wa karibu.

Sasa ngoja siku yakupate...

Huwezi kuamini huyu anayekufanyia unyama ni yule yule ambaye kwa nyakati fulani fulani unashinda naye mkikata kiu, mkisakata rumba au mkisali pamoja.

Sasa ngoja yakufike...

Hayo mashetani pamoja na kujua wewe ni mme/mke wa mtu, ni baba/mama wa watu, ni kiongozi katika jamii...yatakufanyia unyama huku yakicheka na kupongezana!

Ni swala la muda tu...

Mtambeza Wakili Madeleka, mtamtukana, mtamuita kichaa...lakini iko siku! Leo ni wao wanafanyiwa, mko kimya, kesho na kesho kutwa inaweza kuwa zamu yenu!

Ndugu zangu amkeni...

Tunaishi nao, tunacheza nao, tunashiriki nao, tunastarehe nao, tunapiga vigelegele nao lakini iko siku utalia peke yako, utapiga mayowe peke yako...peke yako, peke yako!
 
Haya yote yanaelekea mwishoni wala msihofu watanzania hawa wasiojulikana kwanza tutambue kwamba ni waoga ndio maana wakifanya matukio hayo wanajificha wakati wa utekelezaji,maana yake nini,hata wao hawapendi kutendewa hivyo.MUNGU hajawahi shindwa kamwe.
Mungu atawalipa kwa kipimo hicho hicho
 
Back
Top Bottom