Wakili Madeleka awaanika 'wasiojulikana' kwa majina

Huyu wakili mwanasiasa huwa simwelewi kabisa
Kweli mko wengi humu JF! Mnatetea Mtanzania kumfanyia unyama Mtanzania mwenzake eti kisa? Ni mpinzani, anaikosoa serikali!

Mlivyojipanga humu mnatisha! Mara mnamtaka Wakili Madeleka atoe ushahidi, mara aripoti polisi, mara anayo matatizo ya akili...my God!

Na pia mnao ujasiri wa ajabu...eti mkishafanya yote hayo bado mnao uthubutu wa kurudi nyumbani kwa wake zenu na watoto wenu!

Mbona huku ni kuinajisi si tu familia zenu, kizazi chenu na ukoo wenu wote na kujipa laana ya bure! Kweli kuwa CCM kwahitaji roho ngumu!
 
Huyu kama vile ana ugonjwa wa kichaa, ntashangaa kama Kuna watu wanampa kesi awawakilishe mahakamani.

Audio clip inaonyeshaje mtu anangolewa jino? Analawitiwa? Audio?
Na wewe usijifanye kichwani umeweka makamasi na siyo ubongo. Amesema ''sauti zinasika'' na hakusema zinaonyesha. You are more than idiot! Kama umekasirika sana mfuate bwanako Magufuli kule alikokwenda!
 
Huyu Bwana achoki tu, shukuru Mungu KILA jambo wakati mwingine kukaa jela kumbe Mungu kakuepusha na hatari au kifo.
 
Halafu hawa wote ni vilaza walioshindwa maisha wakapenyezwa kwenye vikundi vichafu vya system wakati wa Magufuli. Bado wako kwenye nyakati kama zile za Iddi Amini na vikundi vyake vya mauaji. Primitive wanaodhani kuwa kwenye vyombo vya usalama basi ni tiketi ya kuua na kutesa unavyotaka. Waache wadhani ni invincibles. Na thread zote zinazoanzishwa za kumtetea Sabaya ni hivi vikundi vinahusika.
 
Kwa hiyo hata hii miili iliyookotwa itakuwa ni hao vijana majina Yao pale CLUBHOUSE ni commando,Jimmy Jones,Mayi,A B,na Ado November
 
Na wewe usijifanye kichwani umeweka makamasi na siyo ubongo. Amesema ''sauti zinasika'' na hakusema zinaonyesha. You are more than idiot! Kama umekasirika sana mfuate bwanako Magufuli kule alikokwenda!
Madereka ni kichaa, hata kesi ya Mbowe, aliomba ajiunge, kibatala akasema hataki mental case, itaharibu kesi
 
Haya yote yanaelekea mwishoni wala msihofu watanzania hawa wasiojulikana kwanza tutambue kwamba ni waoga ndio maana wakifanya matukio hayo wanajificha wakati wa utekelezaji,maana yake nini,hata wao hawapendi kutendewa hivyo.MUNGU hajawahi shindwa kamwe.
 
Mm namfahamu jamaa mmoja anaitwa Addo, ni kada lialia wa chama, ni kiongozi wa wasanii, ni mwinjilisti, shabiki wa yanga na mani yuu. Bila shaka siye aliyetajwa hapa
 
Huyo wakili kuna uwezekano mkubwa akawa hayupo sawa kisaikolojia anahitaji msaada.

Anaumwa ugonjwa wa kutafuta umaarufu.
Kama magufuli alikufa ye anaogopa nini...eti mzee
 
Mm namfahamu jamaa mmoja anaitwa Addo, ni kada lialia wa chama, ni kiongozi wa wasanii, ni mwinjilisti, shabiki wa yanga na mani yuu. Bila shaka siye aliyetajwa hapa
Mimi simfahamu huyo Addo na hata nikikutana naye siwezi kumtambua lakini haya majamaa makatili ni majitu ya kawaida sana kwa muonekano.

Sasa subiri siku yakupate...

Hayana pembe wala umbo za kutisha ila siku moja wao akitambulishwa kwako, huwezi kuamini kwani anaweza kuwa rafiki, jirani au hata ndugu wa karibu.

Sasa ngoja siku yakupate...

Huwezi kuamini huyu anayekufanyia unyama ni yule yule ambaye kwa nyakati fulani fulani unashinda naye mkikata kiu, mkisakata rumba au mkisali pamoja.

Sasa ngoja yakufike...

Hayo mashetani pamoja na kujua wewe ni mme/mke wa mtu, ni baba/mama wa watu, ni kiongozi katika jamii...yatakufanyia unyama huku yakicheka na kupongezana!

Ni swala la muda tu...

Mtambeza Wakili Madeleka, mtamtukana, mtamuita kichaa...lakini iko siku! Leo ni wao wanafanyiwa, mko kimya, kesho na kesho kutwa inaweza kuwa zamu yenu!

Ndugu zangu amkeni...

Tunaishi nao, tunacheza nao, tunashiriki nao, tunastarehe nao, tunapiga vigelegele nao lakini iko siku utalia peke yako, utapiga mayowe peke yako...peke yako, peke yako!
 
Mungu atawalipa kwa kipimo hicho hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…