Wakili Malangalila: Mhadhiri wa UDOM aachiwa kwa dhamana, Mahakama yakataa ombi la fidia

Wakili Malangalila: Mhadhiri wa UDOM aachiwa kwa dhamana, Mahakama yakataa ombi la fidia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, imeamuru Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kaijage, aachiwe kwa dhamana kuanzia Julai 21, 2026, wakati upelelezi wa tuhuma za uchochezi zinazomkabili ukiendelea.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Joachim Tiganga wakati wa usikilizwaji wa Shauri Na. 15653/2026.

Kaijage amekuwa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Chang'ombe kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano yaliyojulikana kama "Sabasaba".

1784638666398.png
Upande wa Serikali ulieleza mahakamani kuwa haukuwa na pingamizi kwa maombi ya kumwachia kwa dhamana, na kwamba taratibu za dhamana zinaweza kuendelea kwa mujibu wa sheria.

Wakili wa mwombaji, Prosper Malangalila, alidai kuwa mteja wake alikaa mahabusu kwa siku 12 bila kufikishwa mahakamani, licha ya kosa analotuhumiwa kuwa linadhaminika.

Soma: Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba

Malangalila aliiomba Mahakama iamuru Kaijage aachiwe kwa dhamana, alipwe fidia kwa kuzuiliwa kwa muda huo na Serikali pia ilipe gharama za maombi hayo.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Mahakama iliamuru Kaijage aachiwe kwa dhamana, lakini ikakataa ombi la kulipwa fidia.

Mahakama imeeleza kuwa baada ya upelelezi kukamilika, Kaijage atafikishwa mahakamani kujibu rasmi tuhuma zinazomkabili

Nje ya Mahakama hiyo, tumezungumza kwa ufupi na Wakili Prosper Malangalila ambaye ni Wakili wa mleta maombi. Video ipo hapo juu
 
Kwa nini upelelezi usiwe unakamilika kwanza ndiyo mtu akamatwe?

99.9% ya kesi zote zinafikishwa mahakamani huku upelelezi haujakamilika,huwa wana harakia kwenda wapi?

Watu wana familia zinawategemea na wengine wanapoteza hadi vibarua vyao kisa kusoteshwa kusubiri upelelezi kukamilika.
 
Hizo mbinu za upelelezi wa kisasa na timilifu wanatoa wapi?
 
Hizo mbinu za upelelezi wa kisasa na timilifu wanautoa wapi?
Mitaala yao ipitiwe upya,wakajifunze pia kwa walioweza na waache kuajiri failures.

1.Tuwe na kanuni zitakazo walazimisha polisi kukamata watu baada ya upelelezi wao kukamilika.

2.Mahakama ikiambiwa upelelezi haujakamilika,imuachie huru huyo mtu hapohapo nawamlipe fidia.
 
Hiyo 1 &2 wameshaambiwa hadi imechosha lakini bado wanaendelea.Ndiyo ujue aina ya watu waliopo wanapenda aidha shortcuts au wanafanya makusudi ili wawatese na kukomoa watuhumiwa.
 
Back
Top Bottom