Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Wakili Richard Manyota amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, watu wanaoishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili na kutambulika na jamii kama wanandoa wanaweza kutambuliwa kisheria kuwa ni wanandoa hata kama hawajafunga ndoa rasmi. Amesema sheria inatambua aina tatu za ndoa ambazo ni za kimila, kidini na za kisheria.
Manyota amesema kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa kinatambua dhana ya ndoa na kulinda haki za pande zote pamoja na watoto wanaopatikana katika mahusiano hayo. Aidha, mali zilizochumwa wakati wa kuishi pamoja zinaweza kugawanywa kwa kuzingatia mchango wa kila upande, ikiwemo fedha, nguvu kazi au huduma ndani ya familia.
Amesisitiza kuwa hakuna upande unaoweza kuchukua mali zote kwa madai kuwa hakukuwa na ndoa rasmi, huku akiwashauri wanaoishi pamoja kurasimisha ndoa zao na kuandikisha mali kwa majina ya pande zote ili kuepusha migogoro ya baadaye.