kwahiyo hajawahi kuhurudhia hata kwenye tribunal tu, manake hapo wamesema kwa miaka hiyo awe aliappear kwenye mahakama, au tribunal. kabla ya 2013 hajawahi kuhudhuria hata tribunal tu? if that is the case, then there might be a problem. pamoja na kwamba, sioni faida kubwa kulishadadia hili, kila mtu anafika pale alipo kwa kudra za Mungu, awe amequalify au hajaqualify, ni vile Mungu angependa kumtumia mtu vile apendavyo na vile alivyo. kuna watu unaweza kuona hawafai kuwepo sehemu fulani lakini Mungu ndio amewafikisha pale, na ukijaribu kuwashambulia unakutana na yule aliyewaweka pale, ndiye utakayepambana naye. siri hii ni kubwa sana katika maisha.
pia, kipimo kile upimacho kwa wenzako, ndicho na wewe utakachopimiwa. vile unavyowafanyia wenzako, na wewe kwa namna moja ama nyingine kwenye maisha yako utafanyiwa tu. chochote unachokifanya ili kutia mchanga kitumbua cha wenzako, na wewe au watoto wako kwa namna moja ama nyingine utakuja kufanyiwa tu kwenye eneo ambao una udhaifu nalo au pengine hata huna udhaifu, ila unalipwa uliyowafanyia wengine. hii sheria katika maisha nimeithibitisha na kuiona kabisa. haimaanishi kwamba hata wewe unastahili kuwepo kwenye kila position katika maisha, iwe uhai, iwe cheo, iwe uwezo wa kutafuta pesa, iwe chochote kinachokufanya ulishe familia yako, vyote ulivyo navyo, ni kwa Neema tu ya Mungu. ukishambulia wengine, na wewe jiandae kushambuliwa kwenye kitumbua unacholishia watoto wako. ni ushauri tu.