TANZIA Wakili msomi Judith Mushumbusi hatunae tena

Watanzania fanyeni mazoezi, mwili unatakiwa uchangamshe.

Jitahidini hata utembee km 2 kwa siku.

Huu ugonjwa hauna madhara kwa watu wanaoushughulisha mwili.

Mbona mama ntilie, machinga, wapiga debe, mafundi ujenzi, wanamichezo, dereva bajaji na bodaboda hawafi?

Sababu miili yao haikai kizembe kama hawa wanaokaa kwenye viyoyozi ofisini.

Note:
Tangu Corona ianze hakuna mwanamichezo duniani aliyefariki.

Wanaupata ila hauwadhuru
usijipe moyo, unaweza ukakimbia na kifua kikakubania huko huko ukaja kwenye machela kaka, haka ka ugonjwa hakana formulla - kakishakupenda wewe ni basi tena.

Sema cha muhimu sana ni kufata kanuni zote za kujikinga toka WHO na si hizi za kibongo.
 
R.I.P Wakili Msomi Judith Mushumbusi

Raha ya milele umpe Ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani tukaonane tena katika asubuhi ile iliyo njema na Kuu.

NOTE: Tuendelee kujikinga na Corona! Maisha sio mali ya serikali unayoishabikia, sio mali ya Kanisa unaloabudu, sio mali ya Kiongozi wako wa kidini wala sio mali ya chama chako. Maisha ni mali yako!

Niwarai tu tena kwamba kama hujaumizwa na Corona basi mshukuru Mungu jiepushe kutoa matamko yanayowaumiza walioumizwa na Corona.

View attachment 1700061
Umetuletea TANZIA, content ni jambo lingine kabisa
 
Nilisikia yule Dr kavavila Arusha naye hatunaye. Alikuwa doctor mzuri sana wa watoto pale Aicc hospital.
 
Hivi kuna ugumu gani kwa Magufuli kudeclear kwamba gonjwa lipo na hivyo kuwapa uhuru wataalamu wa afya kufanya kazi zao bila woga kwamba wanapingana na mwenye Nchi?

Hakuna fedheha wala aibu kusema kwamba Corona “imerudi” baada ya kuwa “tumeiondoa” kwa maombi yetu July 2020

Kinyume chake ni ujuha tu na upunguwani
 
Watanzania fanyeni mazoezi, mwili unatakiwa uchangamshe.

Jitahidini hata utembee km 2 kwa siku.

Huu ugonjwa hauna madhara kwa watu wanaoushughulisha mwili.

Mbona mama ntilie, machinga, wapiga debe, mafundi ujenzi, wanamichezo, dereva bajaji na bodaboda hawafi?

Sababu miili yao haikai kizembe kama hawa wanaokaa kwenye viyoyozi ofisini.

Note:
Tangu Corona ianze hakuna mwanamichezo duniani aliyefariki.

Wanaupata ila hauwadhuru
Siyo kila anayefariki hafanyi mazoezi au anakaa kwenye kiyoyozi. Mwezi uliopoita jirani kwetu alifariki kijana mwenye miaka 30 na alikuwa active. Tatizo ni kuwa alikuwa na kisukari. Huu ugonjwa una complications nyingi sana. (naomba nieleweke kuwa sipingi kama mazoezi husaidia sana kupambana na huu ugonjwa). Kuna watu wanakuwa wako active lakini wanapopatwa huu ugonjwa damu inakuwa ''sticky'' na kusababisha ''clot'' kwenye ubongo na hivyo kifo. Kuna wengine kinga za mwili zinaushambulia tena mwili wa mgojwa (kinga zinaingia kwenye overdrive) na kusababisha inflamation kwenye mapafu na hivyo kifo. Kwa kifupi huu ugonjwa mtu akishakuwa over 40 years kunakuwa na hatari ya aina fulani. Ila kama nilivyosema naunga mkono kuwa kwa wenye mazoezi na wanaofanya kazi za nguvu ugonjwa umeonekana kutowa-affect sana.
 
Hivi kuna ugumu gani kwa Magufuli kudeclear kwamba gonjwa lipo na hivyo kuwapa uhuru wataalamu wa afya kufanya kazi zao bila woga kwamba wanapingana na mwenye Nchi?

Hakuna fedheha wala aibu kusema kwamba Corona “imerudi” baada ya kuwa “tumeiondoa” kwa maombi yetu July 2020

Kinyume chake ni ujuha tu na upunguwani
Magufuli ndiye sababu ya mambo yote kwenda mrama! Ila Tanzania kusema kweli tuna wasomi na raia wajinga na waoga sijawahi kuona. Kama yule prof. wa chuo Kikuu Huria alivyotoa tahadhari nimeshangaa mno mno kada ya wasomi inamwambia aombe radhi. Hii nchi kuna limwata tumelishwa si bure! Inakuwaje mtu mmoja tena anaoneka kama mentaly unstable apelekeshe nchi nzima?
 
nimeshangaa mno mno kada ya wasomi inamwambia aombe radhi. Hii nchi kuna limwata tumelishwa si bure!
Hoja yao ni kwamba eti ametumia headed paper yenye nembo ya Chuo/Serikali na hakuonyesha takwimu kuback up tamko lake. Kwamba angelitoa lile tamko kama individual na sio kutumia mgongo wa chuo

Lakini hii haiondoi ukweli kwamba jumuiya ya wasomi hawa ni wachumia tumbo na wasaka tonge tu.
 
Ni kweli. Hapo ni uchumia tumbo tu.
 
Hivi kuna ugumu gani kwa Magufuli kudeclear kwamba gonjwa lipo na hivyo kuwapa uhuru wataalamu wa afya kufanya kazi zao bila woga kwamba wanapingana na mwenye Nchi?

Hakuna fedheha wala aibu kusema kwamba Corona “imerudi” baada ya kuwa “tumeiondoa” kwa maombi yetu July 2020

Kinyume chake ni ujuha tu na upunguwanI
Mwalimu Nyerere mwaka 1952 Dec aliwahi kusema "Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo"

RIP - kauli yako ina zaidi ya miaka 50 ila bado inakamata hadi wa leo
 
Kwani huwa Kuna wakili ambaye siyo msomi?
 
Japo simfahamu ila Roho yake ipumzike kwa Amani na M/Mungu amuepushe na adhabu ya kaburi
 
Back
Top Bottom