Kibatala, kama uko humu, ubarikiwe sana na Mungu akujalie, akuzidishie wema na alinyanyue jina lako juu zaidi. Mtu safi, mchukia mikwaruzo na mpenda haki... ya nini kukamata watu kisha bango? Naombeni hata nyie polisi walinda haki, uhuru na mali za watu, badilikeni basi, dunia inasonga kwa kasi sana, ya nini kuwa katika mawazo mgando na kuwaonea watu? Mabango yamekuwapo enzi na enzi hata wakoloni hawakuwakamata wafuasi wa Kifimbo kwa kuonesha hisia zao kwa njia ya ,mabango.. acheni kuonea watu, ipo siku watu wataanza kujitoa muhanga, msije sema hamkuliona hilo... Chululu chululu sio ndondondo... haba na haba hujaza kibaba, shauri yenu... nyie endeleeni tu kuwaonea wenye nchi na wenye haki... haya ya uonevu, yana mwisho wake. Nyie endeleeni tu kuwa kama mamba anayekimbilia mtoni wakati mvua inanyesha...