kati ya vitu vya kujilisha upepo hapa duniani ni kutegemea mwanadamu. nimekuwepo kwenye tasnia ya sheria kwa muda mrefu, na huwa nikiona ma laymen wakisema "nina mwanasheria wangu", au namna clients wanavyoweka matumaini makubwaa kwa mwanasheria wake, huwa nawaonea huruma sana kwasababu tunaoijua tasnia ya sheria ni sisi wenyewe wanasheria, wengine hamtakuja kujua na sitawaambia siri. yaani hata kama mtu mbumbumbu wa sheria lakini akivaa ile suti nyeusi na mkoba wa mafile, kagari, n.k akiongea na client wake unaona kabia matumaini yalivyo makubwa. mwanasheria huyohuyo akipigwa chini kwa ubovu wa kichwa chake au uzoefu anakudanganya tu "tutakata rufaa mahakama ya juu, we ongeza mshiko"...hamjui kama ni biashara. hata ukisema ni probono, lakini kwa upande mwingine anatuimia publicity hiyo ili kujitangaza wateja wa kuwadanganya waje wengi. kalagha baho.