TANZIA Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

RIP Prof. Mwaikusa na mwanao pamoja na jirani. Poleni wafiwa, ndugu na marafiki. Hali hii yatisha na kusikitisha !
 
RIP Prof. J Mwaikusa, Inasikitisha sana kusikia mtu ametolewa uhai wake just like that! Poleni wafiwa


Mkj nafikiri huyo lawyer ni somebody Kapinga kama sikosei.

Bi Senti 50..
Kapinga unayemzungumzia ni yule aliyeuawa na shamba boy wake mwaka 2002 (ambae inasemekana alikuwa rafiki mkubwa wa Mkapa ?)


 
Nimepata taarifa kuwa wanae wote wako salama namaanisha Baraka, Msafiri, Amu na Adolf.Aliyeuawa ni mpwa wake alikuwa akisoma VETA na kuna mtu hapa kamtaja kwa jina la Gwamaka.Mods tafadhari sio mtoto wake ni mpwa wake!!

"mwanga wa milele uwaangazie eeh Bwana"
 
Kwa kweli inasikitisha sana kuona watu wanauawa kikatili hivyo hasa ukichukulia Profesa mwaikusa kwa jinsi alivyokuwa mlemavu kiasi kwamba kama kweli mtu ni jambazi sijui kama prof. angeweza kuleta resistance ya kupelekea kumfyatulia risasi. Hatuwezi kujua yaliyojiri wakati wa tukio,lakini kwani nini auwawe na mpwawe na tena jirani ndiyo kufunika pazia kuonyesha kwamba prof.hakuwa aimed na kwamba jamaa walikuwa wanaua kila waliyemkuta tuuu au jambo lenyewe lina maana gani? Msiba wake umestusha mno na kuacha maswali mengi. Faculty of law udsm na watanzania kwa ujumla tumeachiwa pengo kubwa sana kwa kuondokewa na msomi mashuhuri na bobezi katika fani ya administrative and constitutional law. Binafsi Prof. ni mwalimu wangu first and second year pale mlimani, kwa kweli nitamkumbuka sana kwa jinsi alivyokuwa deep na mwalimu mzuri
 
Yaelekea wewe ni mwandishi mwandamizi wa serikali na unayejua siri nyingi za serikali. Tuhabarishe basi kushughulikia watu kimya kimya maana yake nini manake inabaki ni mafumbo kwa waioelewa.
 
RIP Prof.Mwaikusa,
hii kitu imenikumbusha kifo cha aliewahi kuwa waziri miaka ya mwishoni na tisini Prof. Nicas Mahinda kama sikosei na yeye aliuawa na majambazi kama sijakosea mitaa ya huko mbezi beach,Inasikitisha sana vichwa muhimu kwa kanchi ketu vinapotea hivihivi.
 

Mkuu,

You have said it all!!!!

Tiba
 
Maneno yaliyoandikwa hapa ni vigumu kuamini kama yanaweza kutamkwa na mwajiriwa wa wananchi. Kila neno liliandikwa ni zito mno...hata mahakama kuu!. Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa maneno haya yametamkwa na mtu anayetarajiwa kuwajibika kwa wananchi mpaka nisikie mwenyewe kwa masikio yangu. Mwenye hotuba airushe hapa ili tuhakikishe wenyewe. Maana tunahitaji madaraka ya serikali yarudi kwa wananchi ili tuwe salama zaidi.
 
Hili ni fundisho kwa wasomi wanaojifanya kuunga mkono opposition.
Bongolander

Una maana gani kusema hivyo ina maana umesha conclude kuwa ni mauaji ya kisiasa, i dont think so, kama una uhakika basi ni vizuri ukaisaidia polisi.
 
Naungana na wewe sioni mauaji haya yanahusianaje na kesi ya mgombea binafsi, kesi ilitupiliwa mbali angalau basi ingepita, kama ni mauaji yanayohusiana na kesi hiyo labda yangetokea kipindi cha kesi yenyewe na hasa kabla ya hukumu na si baada ya hukumu kutolewa.
 

Daily News pia wamereport habari hii ya kusikitisha kwa kweli. RIP Prof. Mwaikusa.
 
Last edited by a moderator:
Jamani-ee mola uliyetuumba sisi binadamu-upokee roho za hao waliotangulia mbele ya haki
 

Ulinzi wa raia uko mikononi mwa nani kama sio serikali ambayo inakusanya kodi kwa kazi hiyo? Kwa nini tunakuwa wagumu kuita spade as spade na tunaanza kutafuta sababu nyingine? Maisha yake mengine yapi? Kwani visasi vimeruhusiwa kuua? Kipimo cha maisha ya Mtanzania ni kuoanisha na Kenya au Congo? Je maisha ya Watanzania ni rahisi hivyo?

Ukweli ni lazima usemwe serikali ya JK chini ya Chama Cha Majambazi inaonyesha its true colours. Je wafe wangapi ndio serikali ifahamu wajibu wake?
 
Watu msi conclude kuwa ni suala la kisiasa ingawaje ujambazi nao haumo kwa sababu hawakuiba kitu,ila watu wanasahau kuwa hakuna mtu ambaye hana mapungufu duniani.Inawezekana kabisa ikawa ni ishu ya kudunguliana wake,gfriend au pesa n.k.
Kisiasa pia mie napinga sio kweli kwani hatiiishi kihivyo kama akina Slaa,Zito,Maalim na wengineo,Nafikiri suala hili litakuwa kibinafsi zaidi na maybe visasi.
Lets wait vyombo vya sheria vifanye kazi yake tusizushe vitu ambavyo sivyo.
rip prof.
 
Sehemu alizofanya kazi zina siri nzito sana...Hivi hiyo Mkono advocates si ndiyo ile ya Nimrod Mkono?Hao na kina Maregesi ndo wanajuwa issue nyingi za ufisadi ie EPA,Kagoda nk....CV yake inaonyesha ni mtu aliyekuwa na info nyingi tu na siri nzito.
Ni vigumu kujua adui ni nani lakini ndugu jamaa na marafiki wa karibu watakuwa wanajuwa kama uwezekano wa kuuwawa kwa visasi upo ama la.
Ni kazi ya jeshi lapolisi kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane,hiyo ndiyo njia pekee ya serikali kuitendea haki familia ya Mwaikusa.
 

Mwaikusa alikuwa jirani yangu kwa muda mrefsu sana tangu akiwa Lecturer na hadi kuwa Senior Lecturer hapo UDSM; nilihama kabla hajawa Profesa. Kwa jinsi ninavyomfahamu, ni vigumu sana kuamini kuwa alikuwa na personal issues na mtu yeyote. Alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kujenga uhusiano mzuri na mtu yeyote. Ni muda mrefu sasa umepita tangu tuachane, lakini siamini kuwa Mwaikusa angewaza kubadilika na kuwa mtu asiyejali kiasi cha kujijengea maadui binafsi. Wasiwasi wangu mkubwa ni kuwa huenda amenyamazishwa ili kesi alozokuwa anasimamia mahakamani zikwame. Swali langu linakuwa: je, ni kesi gani alizokuwa akisimamia kabla hajaletewa mauti hayo?

Mwaikusa alikuwa ni jirani pekee aliyefanya nilifaidi sana raha ya kuwa na jirani; baada ya kuupoteza ujirani wake sijawahi tena kujisikia kwenye ujirani mweingine; Mungu ampumzishe pema peponi
 
Yaelekea unayafahamu maisha binafsi ya Prof. Tueleze na utupatie ushahidi. Tunachojua sisi serikali ni mwajiriwa wa wananchi na inatarajiwa kuwajibika na kuwalinda wananchi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…