TANZIA Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania


Huu tena sio ujambazi bali ni staili ya kimafia ya Tanzania kwani sio hao waalimu tu bali hata yule journalist ambae alikuwa anaandika column kwenye East African naye aliuawa kwa stili hii hii pale Kimara!! Mpaka sasa hatima ya hao waliomuua haijulikani ; they just add to the statistics of murdered Tanzanians!!
 

Hivi hakuna kauli zozote rasmi zilizotolewa za kuyalaani maneno yale?Nashangazwa sana na hilo....Rais wa nchi kusema kuwa ana uwezo wa kufanya chochote bila ya kujali haki za binadamu ni hatari sana,na ni hatari zaidi pale kauli kama hizo zinapoonekana kuwa za kawaida.
 
Wahenga walikwisha onya kuwa muangalieni vizuri huyu mkwere ana traits za kidictator kama mtamuachia afanye atakalo!!
Maybe his true colors are now coming out,nadhani wamejipanga kufanya anything,Mwanakijiji ndiyo anasema aachiwe kwasababu there is nothing next if he is to loose on the next elections...Unaambiwa ukistaajabu ya Musa....Cha ajabu ni kwamba sijasikia kauli hizo zikilaaniwa..Amesema wazi kabisa msione anacheka mkadhani anawechekea.
 
mmh nahisi mbinu chafu hapa,hasa kwamba prof alikua jaji I.C.T.R.hii kufungua milango ya E.A.C.nayo watu wanaweza kuingia wakammaliza kisha wakarudi kwao kimya.

Mkuu thats too low yaani auawe kwa sababu ya kuwa Judge ICTR kwani hiyo mahakama imeanza juzi mbona majaji wangapi wa hiyo mahakama wamashauwawa ?
Mshamdulumu jamaa uhai wake basi life goes on but who will be next?
 

Mkuu hapo umenimaliza.
 

Your mind is slow uko dunia gani,wanauwa bila kuiba what is that?is that hard to conect dots and conclude!!!?
 

amani na utulivu upi watu wanauwawa!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????wake up
 

unajuaje wao uliowataja wanajirindaje?
 
"BABA yako asingekuwa mbishi tusingemuua, lakini tumemuua kutokana na ubishi wake," ni kauli ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliompiga risasi na kumuua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Wakili bingwa wa Mambo ya Katiba, Profesa Jwan Mwaikusa (50).

Kauli hiyo waliitoa kwa mtoto wa marehemu, Baraka (28), ambaye baada ya kushuhudia baba yake amepigwa risasi, alijitoa mhanga kumsaidia lakini watu hao wakamdhibiti na kumwonya kuwa wangemtoa roho kama walivyofanya kwa baba yake.

"Na wewe unataka tukuue kama tulivyomuua baba yako?" Walihoji watu hao naye akajibu "hapana," ndipo wakamwamuru: "Kama hauko tayari kufa, kimbia haraka na usigeuke nyuma."

Profesa Mwaikusa kabla ya kupigwa risasi, watu hao walishampiga risasi na kumuua mpwa wake, Gwamaka Mwasanjala (25), ambaye aligoma kuwekwa chini ya ulinzi na mmoja wa watu hao na kulazimika kupigana nao kwa muda na ndipo wakammaliza kwa risasi.

Lakini pia watu hao walipomaliza kufanya unyama huo, walikwenda eneo lingine jirani ambako walifanya uporaji na kumuua mtu mwingine aliyetambuliwa kwa jina la John Mtui Ngowi (45).

Inadaiwa Ngowi aliuawa baada ya watu hao kubaini kuwa alikuwa na bastola mfukoni. Licha ya kuwa Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lakini pia alikuwa anafanya uwakili na kampuni ya uwakili ya Mkono and Advocates ya Dar es Salaam.

Msomi huyo pia alikuwa wakili katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyoko Arusha. Pia alishiriki katika jopo la marafiki wa Mahakama ya Rufaa Tanzania katika shauri la mgombea binafsi hivi karibuni.

Tukeni Mfyati ambaye ndiye kijana aliyefungua geti wakati Profesa alipopiga honi, anasema mara tu baada ya kufungua geti na Profesa kuingiza gari, majambazi hao waliingia kwa miguu na kumweka chini ya ulinzi na kumtaka atii maelekezo yote anayopewa.

"Waliniuliza huyu mzee unamfahamu, nikajibu ndiyo, naomba utupeleke pale anapoegesha gari," alisema Mfyati ambaye ni mpwa wa mtumishi ndani ya nyumba ya Profesa Mwaikusa. Mfyati alisema wakati anawapeleka, Profesa alipokuwa anataka kuegesha gari, mmoja akamwamuru mwenzake warudi katika lango kwa ajili ya kulifunga na walipolifikia geti wakakutana na Gwamaka ambaye wakati huo alikuwa anatoka dukani.

Alisema wakati Gwamaka anaingia, jambazi aliyefuatana na kijana huyo akamweka chini ya ulinzi Gwamaka, lakini akagoma kutii na wakaanza kupigana kwa muda na ndipo jambazi aliyebaki ndani ya nyumba akarudi getini baada ya kuona tafrani hiyo.

"Yule jambazi tuliyemwacha ndani alikuja na kusema, huyo anayeleta ubishi usimwache hai, mpige risasi, Gwamaka baada ya kugundua mtu aliyekuwa anapigana naye ana bunduki, alikimbia; lakini akapigwa risasi ya mgongoni na kuanguka," alisema Mfyati.

Kijana mwingine Francis ambaye wakati tukio hilo linatokea alikuwa anaangalia televisheni na Baraka katika nyumba ndogo ya uani, alisema wakati ilipopigwa risasi iliyomuua Gwamaka, walidhani ni gari limepata pancha.

Lakini ghafla wakasikia kelele za "toka nje, fungua mlango" na walipotoka wakaona jambazi huyo ameelekeza silaha kwenye gari huku Profesa akiwa ndani ya gari, akimwangalia jambazi huyo aliyekuwa anamwamuru afungue mlango wa gari au dirisha.

Wakati anatoa amri hiyo, watoto wa kike waliokuwa ndani walikuwa wakipiga kelele za kuomba msaada na jambazi huyo akapiga risasi kwenye moja ya madirisha kuwanyamazisha.

Baada ya risasi hiyo ya dirisha, ghafla jambazi huyo alipiga risasi ya kwanza na ya pili kupitia dirisha la dereva zikampata Profesa na kumuua papo hapo.


Aliongeza kuwa baada ya kufyatua risasi hizo, jambazi huyo aliingiza mkono kwenye gari na kulizima na akafungua mlango na kumvuta Profesa Mwaikusa ambaye tayari mauti yalishamkuta.

Alisema jambazi huyo baada ya kumvutia chini, waliwasha taa ya ndani ya gari na kupekua hata kwenye mifuko yake ya suruali na ndipo Baraka baada ya kuona baba yake ameuawa, alikimbia sehemu hiyo na kuhoji sababu za kumuua baba yake.

Baraka alisema baada ya kuona baba yake anavutwa kutoka ndani ya gari na kukanyagwa kifuani, ilimuuma, akajitosa kuwahoji majambazi sababu ya kufanya hivyo, ndipo wakamjibu kwa ukali.

"Nilipata ujasiri wa ajabu hadi nikaenda na kuwahoji huyu ni baba yangu kwa nini mnamuua, ndipo wakanijibu majibu hayo," alisema.

Baraka alisema pia kuwa wakati wakiwa kwenye majibizano na majambazi hao, alimtazama mmoja usoni kitendo kilichompandisha hasira na kumwamuru aangalie pembeni.

"Wewe kwa nini unanichunguza usoni, ni kosa kubwa kuchunguza sura yangu," alisema Baraka akimkariri jambazi huyo na kufafanua kuwa kutokana na hasira, jambazi huyo alinyanyua bunduki na kutaka kumpiga kwa kitako naye akakwepa.

"Nilipokwepa nilipigwa makofi wakaniambia ‘ondoka hapa kimbia', mwingine akaniuliza ‘chumba chako kiko wapi?'

Nikawaambia kiko huku wakaniambia ‘haya kimbia nyuma usigeuke'," alisema Baraka ambaye anaamini kuna kitu walichokuwa wanakitafuta, lakini na yeye hajajua ni kitu gani.

Naye Flora Mwakasala anaripoti kwamba Polisi Dar es Salaam inawatafuta watu wawili walioua watu watatu akiwamo Profesa Mwaikusa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Charles Kenyela, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa nane usiku Salasala. Kwa mujibu wa Kamanda Kenyela watu wengine waliouawa Gwamaka (25) ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi cha Veta na Mtui.

Alisema jirani wa Mwaikusa (Mtui) alitoka na bastola yake aina ya Revolver namba 87668 ndipo akashambuliwa. Profesa Mwaikusa ameacha mjane na watoto wanne, Baraka, Musa, Amu na Adolf.
 
Kama haumfahamu muuaji kwa asilimia 100% unawezaje kusema fulani hahusiki?

Mkuu kuna mambo mengine hutuna haja ya kutumia akili nyingi kugungua nani kafanya hili na nani hajafanya hili. Kama Mwaikusa alichagia kufikia hukumu for or against RPF au Interhamwe, kuumua hakubadilishi lolote, na hakuna maana yoyote kwa Rwanda, wanyarwanda au wahutu na watusi, just unthinkable. Ni sawa na kukuta yai na kuaza kusema inawezekana ni mbuzi ametaga yai hili. Hii haiwezekani kabisa. Mwaikusa tumemuua sisi wenyewe watanzania, kusema ni wanyanrwanda ni kujaribu kuexport weaknesses zetu na kutafuta cheap scape goats. It is not the first kutokea hapa Tanzania, even worse it not the last .
 
Mtujuze kama ni majambazi tu au kuna mkono mwingine.

I feel like sio majambazi, coz nikifikiria kwa yule profesa majambazi yangekuwa interested na nini sipati jibu, and in fact hawajaiba kitu chochote .... so clearly kunakuwa na mazingira yasiyo na shaka kuwa kuna agenda nyingine ya siri.

Maana yule profesa wa watu haweki hela nyumbani .. na sasa kama ni vibaka wa kuiba tu-vitu vya ndani mbona wametumia excessive force na hawajaiba kitu..... isije ikawa ni zile kesi za mauaji ya Kimbari alizokuwa anazitetea ICTR ndio zimesababisha haya>>>> maana sipati link nyingine ya possible cause of such hatred! Ee mola tusaidie maana polisi kama kawaida yao wanasema watafanya uchunguzi wa kina. lakini wote tujuavyo ripoti haitatoka au ikitoka inakuwa feki na inatolewa baada ya muda mwingi kupita... and abve all haimrudishi Prof wetu duniani! Mungu tuepushe na mabalaa haya, maana Salasala kila kukicha unasikia majambazi yanatamba, vyombo vyetu vya usalama kimya hawana strategy zozote za kulishughulikia hili. Hadi inafikia point mtu unajihoji hivi vyombo vyetu vya usalama ni kwa ajili ya kulinda usalama wa raia na mali zao au vya kufanya uchunguzi. Inavyoonekana wamejikita zaidi kwenye kufanya uchunguzi wa matukio yaliyokwishafanywa badala ya kuyazuia strategically....


Inatia uchungu sana, maana kwa profesa miaka 54 bado ni mchanga sana hata taifa halijamtumia vya kutosha...ee mola tutie nguvu! Amen
 
Aliyekuwa Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sheria, Profesa Jwan Mwaikusa (58), amefariki dunia saa nne usiku wa Julai 13, 2010 baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake eneo la Salasala jijini Dar es Salaam.

Mwaikasu ni mmoja kati ya watu watatu waliouawa katika tukio hilo ambapop wengine waliouawa ni pamoja na mpwa wake, Gwamaka Mwakanjara (25), na jirani yake John Ngowi, mwenye umri wa miaka zaidi ya 40.

(bofya picha zilizopo hapa kuzikuza na kusoma maelezo yanayoambatana na picha husika)














Imeelezwa na mashuhuda wa tukio hilo kuwa wauaji hao hawakuchukua mali yeyote, ingawa mmoja wa watoto wa Profesa Mwaikusa alisema aliwaona wakimpekua baba yake baada ya kumuua. Washiriki wa mauaji hayo walimwinda Profesa Mwaikusa wakati akiingia kwenye lango la nyumbani kwake baada ya kufunguliwa lango hilo na kuingia ndani ya nyumba yake.

Akisimulia tukio hilo, mtoto wa Profesa Mwaikusa, Baraka Mwaikusa (28), alisema wakati baba yake anauawa kwa risasi alikuwa ndani akijiandaa kulala na alishuhudia tukio lote baada ya kusikia kishindo na kutoka nje.



















"Hili ni tukio baya sana kwangu, kwa sababu baba ameuawa wakati namuona, wakati akiingia hapa nyumbani na gari lake alifunguliwa lango na kijana mmoja jirani yetu, wakati huo mimi nikiwa ndani.

"Nilisikia muungurumo wa gari, nikajua tu kuwa ni mzee anaingia, nikamuona akiendesha gari kuelekea geti la juu ili ageuze gari kama kawaida yake.

"Wakati akigeuza gari, ghafla nilisikia kishindo cha ajabu, nikashtuka kwa sababu sikujua kilikuwa ni kitu gani ila nilihisi ni kitu Fulani kilichokanyagwa na tairi la gari.

"Kumbe kishindo nilichosikia ilikuwa ni risasi ambayo tayari majambazi hao walikuwa wamempiga binamu yetu Gwamaka baada ya kukutana nao getini uso kwa uso na kupishana Kiswahili, huku wao wakimtaka kuinua mikono juu.

"Dakika chache baada ya Gwamaka kuuawa, nikasikia watu wawili wakimwamrisha baba, ‘fungua mlango wa gari, "Nakwambia fungua mlango, fungua haraka ushuke chini."

















"Mzee hakutii amri yao, akaendelea kukaa kwenye gari huku akiwa amefunga vioo," alisema Baraka.

Kwa mujibu wa Baraka, wakati majambazi hao wakimwamrisha Profesa Mwaikusa kisha kumuua kwa risasi, yeye alikuwa ndani akiwaona kupitia dirishani.

"Baba alipokataa kutii amri yao, nikaona mmoja ananyanyua bunduki akamlenga baba na kumpiga risasi mbili kifuani na kumuua hapo hapo kisha wakamshusha kwenye gari na kuanza kumkanyaga huku wakimpekua mifukoni.

"Nilipoona hivyo, nilichanganyikiwa na kutoka nje, na kuwafuata eneo hilo na kuwauliza kwa nini wamemuua baba?

"Wakaniambia, ‘asingekuwa mbishi tusingemuua', mmoja wao akatoa bastola, akaniuliza tena, ‘na wewe unataka tukuue kama baba yako'?

"Hapo nikanyamaza, wakanikamata na kuanza kunipiga ngumi na makofi, kisha wakaniambia ‘mikono juu, ondoka hapa, kimbia haraka hatutaki kukuona'.

"Niligeuka nikaondoka taratibu, wakanirushia mawe nami nikaanza kukimbia, kwa kweli wakati huo sikuwa na akili hata moja ya kufikiri lolote nilipoteza kabisa kumbukumbu," alisema.

















Baada ya majambazi hao kumuua Profesa Mwaikusa na mpwa wake, waliondoka nyumbani hapo na kuvamia maduka kadhaa na kupora fedha, vocha za simu na mali nyingine.

Inasemekana wakati wa uvamizi huo, Ngowi alipekuliwa na kukutwa na bastola. Hatua ya kukutwa na bastola ilimfanya mmoja wa wajambazi hao ampige risasi mbili. Imeelezwa kuwa Ngowi alifika nyumbani kwake na kuchukua bastola hiyo baada ya kupita kwa Profesa Mwaikusa na kuona purukushani zilizokuwa mahala hapo na kuhisi kuwa kuna tukio la uvamizi. Wakati Ngowi akiwa anarudi eneo la tukio, ghafla naye alitekwa na kuunganishwa na wengine waliokuwa wamelazwa chini nje ya duka na kuanza kupekuliwa, wengine wakipokonywa simu na fedha na alipopekuliwa yeye alikuwa mbishi na ndipo alipopekuliwa kwa nguvu na kukutwa na Bastola na kisha kupigwa risasi ambapo alikimbia kutoka eneo hilo akiwa amechanganyikiwa na kufia eneo la Kanisani.




















Kaimu Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha watu hao wanakamatwa.
 



I am a fighter
I was once a fighter,
A fighter of great prowess,
A fighter of great calibre.
"I am a fighter!" I shouted,
And before I had realised it,
I had won the fight.

My opponents gave way
And surrendered with fear
"You have won, " they said,
And grim faced, they left.
Without another glance at me, they saw the fighter,
Carried shoulder high by cheering supporters.

"I am a fighter!" I shouted
But there was nobody to fight,
So I had to relax.

But how can a fighter relax
Except by fighting?
How can a killer repose
Except by killing?
How can a dancer recreate
Except by dancing?
I had to relax too,
I had to repose,
I had o recreate.

"I am a fighter!" I shouted
But my enemies were no longer there,
They had long joined the mocking audience
Looking at me with nobody to fight.

So
I turned grimly to my supporters
Holding me high in worship:
"I am a fighter!" I declared to them.

Jwani Mwaikusa (1980: 63 - 64), Summons: Poems from Tanzania, published by Tanzania Publishing House (TPH)
 

Waliopanga Haya Hawata Fika Mbali, Tatizo litabaki pale pale!
 
Hii ndio kazi ya usalama wa taifa? Au usalama wa viongozi wabovu? Circumstantial evidence shows that his death is associated with independent candidacy court of appeal proceedings! Hivi wewe Augustino Ramadhani na jopo lako la majaji sita mlishindwa kuamua wenyewe?

Ila aliye juu na mwenye uweza kuliko wote atalishughulikia suala ili na kutoa haki. Na wauwaji hawana muda wa kuishi zaidi ya miaka 50 kutoka 2010 ukizingatia life expectancy yetu; hivyo wanahangaikia mambo ya kupita.

RIP Prof.
 
Kwa hiyo wewe unafanya kazi ya kuwatakasa baadhi ya watu, unafanya kazi ya afisa uhusiano? Kwa taarifa yako uchunguzi kwenye mauaji ya aina hii hauna mipaka. Teba utetezi wako unaweza kutia mashaka zaidi na kuelekeza huko unakotetetea kuwa moja ya sehemu za kuchunguza kwa ukaribu zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…