Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

Ndugu Watanzania,

Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa wakili msomi Boniface Kanjunjule Mwabukusi amekamatwa na Jeshi la Polisi kule Mikumi, Morogoro akiwa pamoja na Katibu wa Kanda wa CHADEMA, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali.

Inadaiwa kuwa walikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, watu waliojitambulisha kuwa ni Askari ndio wamewakamata pasipo kutaja kosa lao na wapi wanapelekwa zaidi ya kuambiwa ni Maelekezo kutoka Juu. Pia, vifaa vyao vya mawasiliano (Simu za mkononi) vimechukuliwa.

Pia soma: RPC Morogoro: Sina taarifa ya kukamatwa kwa Wakili Mwabukusi, Mdude na Masonga
Serikali isijiendeshe kigangstar.

Naona watu ndani ya serikalli wanamharibia rais wetu mpendwa kwa makusudi
 
Hawa jamaa wanaojifanya watetezi wa Bandari wanataka tuwaamini kwa kila wanachosema eti nyasi zote zina rangi ya blue ole wako upinge naona busara zote zime fikia mwisho wanahitaji matibabu hawa tiba nyingine ili kunusuru mgonjwa lazima apewe nusu kaputi ili afanyiwe upasuaji salama.
Wamebembelezwa sana inatosha.
Kosa lao ni kupinga utaratibu wa uwekezaji ndo uwaone kama hawana haki ya kuishi?
 
Mlikuwa mnamchukia bure JPM utawala huu ndio wa kidhalimu hata shetani anaukataa kuwa na usharika nao.

Vitendo vya kutisha wananchi kwa kutumia madaraka waliyopewa na wananchi wenyewe itafikia ukingo wa uvumilivu

Free #Mwabhukusi, Mdude na Mwaisonga without any condition lest spade-a-spade
Hao labda wasiwekwe ndani zaidi ya wiki 2, bila hivyo lazima warudi majumbani mwao na uja uzito, sijui watawaambia nini familia zao.
 
This is a police state mimi sishangai. Kinachonishangaza ni reaction ya watu. Kwa sababu watu wanadhani haliwaathiri wao jwa sababu hawahudiki moja kwa moja. How wrong. Mnakumbuka 1990 wanafunzi wa UDSM walipinga suala zima la mikopo ya wanafunzi. Chuo kilifungwa na wanafunzi wa primary na secondary schools wakaandamana kuwalaani UDSM. Ujinga wao hawakufikiria kwamba nao wanapitia huko huko. Waliokuja kuathirika zaudi ni wao na mpaka leo watu wanapata shida na mikopo hiyo. The same is happening now. Believe me tutapata maumivu makubwa sana. In fact tumeshaanza. Tunatakiwa kulipa 1.5trn na kesi bado xinaendelea.
Walipinga mikopo walitaka wasome Bure!?..hela itoke wapi!?..mbwa wale walizowea bure
 
Ni vema taarifa ziwe zinaletwa kwa Lugha sahihi ili tusiibue taharuki.

Kichwa cha thread kinajieleza sasa niambieni huyo Wakili alikuwa anatoroka au ni Katika Utaratibu wa kawaida wa Polisi kumshikilia Mtu kwa Mahojiano?

Tuendelee na Sabato ya Bwana!

Pia soma: Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam
Kwanini wanawashikilia bila taarifa kwa RPC wa mkoa wa Morogoro na kosa kuainishwa? Kwanini wanawakamata kabla ya uchunguzi? CCM na serikali yake mmekuwa wanyanyasaji sana wa wananchi kwa hofu ya kuanikwa mabaya yenu. Halafu bado unaishabikia hicho chama cha kijani kilichojaa wezi, waovu na wabinafsi. Kwanini wanawahofia sana watu wasiokuwa na silaha yoyote? Kwanini mmemzuia asiende kukataa rufaa ya hukumu elekezi ya huko Mbeya?

Bado dakika chache sana wananchi ambao mnawaona kwamba mkikamata mtu wanakaa kimya...!!!
"This time around it shall not prevail other than invoking a backlash with a negative impact on the sitting regime".
 
Hawa jamaa wanaojifanya watetezi wa Bandari wanataka tuwaamini kwa kila wanachosema eti nyasi zote zina rangi ya blue ole wako upinge naona busara zote zime fikia mwisho wanahitaji matibabu hawa tiba nyingine ili kunusuru mgonjwa lazima apewe nusu kaputi ili afanyiwe upasuaji salama.
Wamebembelezwa sana inatosha.
Ccm mnajiona malaika sana
 
Ndugu Watanzania,

Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa wakili msomi Boniface Kanjunjule Mwabukusi amekamatwa na Jeshi la Polisi kule Mikumi, Morogoro akiwa pamoja na Katibu wa Kanda wa CHADEMA, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali.

Inadaiwa kuwa walikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, watu waliojitambulisha kuwa ni Askari ndio wamewakamata pasipo kutaja kosa lao na wapi wanapelekwa zaidi ya kuambiwa ni Maelekezo kutoka Juu. Pia, vifaa vyao vya mawasiliano (Simu za mkononi) vimechukuliwa.

Pia soma: RPC Morogoro: Sina taarifa ya kukamatwa kwa Wakili Mwabukusi, Mdude na Masonga
Dduuhhh 🤨
 
Ni vema taarifa ziwe zinaletwa kwa Lugha sahihi ili tusiibue taharuki.

Kichwa cha thread kinajieleza sasa niambieni huyo Wakili alikuwa anatoroka au ni Katika Utaratibu wa kawaida wa Polisi kumshikilia Mtu kwa Mahojiano?

Tuendelee na Sabato ya Bwana!

Pia soma: Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam
Unakamatwa halafu unashikiliwa. Labda kama walijipeleka wenyewe bila kushurutishwa.

Amandla...
 
Back
Top Bottom