Sidhani kama yupo anayejielewa atautilia shaka msimamo wa Adv. Mwabukusi, na ni ngumu sana kwa mtu mwenye msimamo wa aina ile, aliyeiweka mpaka nafsi yake rehani, kuchanganywa kundi moja na wapinzani maslahi wanaoutafuta utajiri kupitia siasa, hiyo ni sawa na kuchanganya maji na mafuta.
Huyu ameamua kusema kweli liwalo na liwe, kwani ameshaona dalili huko tuendako, ni wapinzani ndio wataanza kucheza ngoma za CCM na sio vice versa, CCM wameshajua hawa wakitaka kitu chelewa kuwapa mwishowe watageukana wenyewe, kwa sababu hawana misimamo ya pamoja.
Hiki ndicho Adv. Mwabukusi amekiona na kukilaani, na wala sio vinginevyo, ambacho kwangu ni ukweli mtupu.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app