Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Mwabukusi anashindwa kuelewa kwamba haya yanatokea kwa sababu zile kamati za siri ziitwazo deep state zilibariki eti siasa ndio iwe kazi yenye malipo makubwa kuliko kazi nyingine!!! Ndio maana uchawa ni karata kubwa kwa ajili ya teuzi Ili wale mapesa!!

Akipatikana mtu kama Mimi nitakayeifanya siasa kuwa kazi ya kawaida isiyo. Na malipo makubwa kama ya ualimu tu vile nakuambia tutatatua tatizo kubwa sana,mapato ya siasa yaende kwenye ueledi Ili kuleta tija kwenye maendeleo ya watu wote!!!


Nitaendelea kulia na dola siku zote!!
 

Shida uchaguzi kwa katiba hii na sheria zilizopo ni Bure tu. Serikali ndio inaamua nani akae wapi na asikae wapi.
 
Historia ya ccm huko siku za nyuma ilikuwa ina maana kwa kiwango fulani, ila baada ya kujazana mafisadi, kwa sasa inaongooza kutokana na kujaa makondoo hapa nchini. Haina sifa nyingine zaidi ya kuwa chama Cha majizi.

Cdm hawana muda wa kushiriki upuuzi ili ionekane ina sifa ya kutosusia. Na Isitoshe kususia na njia sahihi ya kisiasa popote pale duniani. Hata sisi kama nchi tumewahi kususia baadhi ya nchi. Mfano tuliwasusia Africa kusini wakati wa apartheid, lakini hatukuzuia SA kuwa matajiri na uchumi mkubwa.

Huko cdm Mimi ni shabiki wa kutupwa na Wala sijavamia. Sina popote ninapowasifia au kuwaunga mkono majizi ya ccm. Sasa unaposema nalalamika sijui unaanisha Nini. Tume ya uchaguzi na katiba mpya sio ombi ni lazima maana vimedaiwa kwa more than 30yrs, hivyo enough is enough. Hatuna muda wa kuendelea kushiriki upuuzi uitwao uchaguzi wakati tunaona kabisa hilo zoezi haliheshimiwi. Uchaguzi tunashindwa ama ni uhayawani huwa unaendelea? Hakuna ccm ya kuendelea kushinda kama mtakavyo.

Siasa ni science, ila sio kwa hizi siasa za kipuuzi mnazoendesha ccm. Labda kama hilo neno science unalitumia kama fashion.
 

Hayo ungesema kukiwa na Time huru na mabadiliko ya katiba. Sio kwenye nchi hii ambayo Mkuu wa mkoa anampigia kampeni mbunge wa CCM.
 
Swala la uchaguzi nitaamuliwa na vikao halali vya chama na wanachama, chadema sio chama cha mchezo msifikili ikitokea wakasusa uchaguzi kwamba patakalika, haijalishi ni vyama vya mfukoni vingapi vinaweza shiriki, hilo ccm wakae wakilijua na wasilete hujua na jambo hili ,

Unapozungumzia siasa za tz ndani na nje ya nchi unazungumzia ccm vs Chadema , so hacha ccm wajichanganye ndo watakapo lifikisha taifa pale wanapataka
 
uchaguzi chadema itashiriki ,na itashindwa kihalali
Hakuna ccm ya kushinda kihalali nchi hii. Na siku ccm itakubali ushindani wa halali ndio itakuwa mwisho wake. Cdm kama chama kushiriki huo ni uamuzi wao, lakini sisi wapiga kura tulio wengi hatutakuwa na muda tena wa kushiriki huo upuuzi usioheshimiwa.
 

Ukweli kabisa. Yeye anaona wengine hawafanyi chochote.
 

Tusiteme big G kwa karanga za kuonjeshwa. Nadhani hujui motive ya Mwabukusi. Mwabukusi anatumia nguvu nyingi kuishambulia upinzani kuliko CCM. Kwanza kadai wapinzani wanafanya biashara ya demokrasia nk. Sasa kwa kauli Kama hiyo huyo yupo upinzani kwa lengo gani. Hapo kaipa CCM milage kubwa Sana.

Mimi simuamini Tena. Kuna kauli mtu akizisema unajua huyu sio mpinzani ana mission yake tofauti. Mtu unaushambulia upinzani kuliko hata Makonda na chongolo. Muangali Mwabukusi kwa jicho la mbali utaujua ukweli.
 
Nchi za Africa Magharibi nyingi zipo kwny mikono ya Wanajeshi na Raia wanapigania zirudi kwa Raia japp hapo awali waliona bora Mapinduzi ya kijeshi yatokee

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
Tunataka hayo mapinduzi ya kijeshi, kisha tukirudi kiraia tuanze Moja, hakutakuwa na chama chochote kupendelewa. Hapo Kila mmoja atashinda kwa sera na sio huu uhuni unaoendelea sasa.
 
uchaguzi chadema itashiriki ,na itashindwa kihalali

Ikishiriki kwa Katiba hii na sheria hii na serikali hii, ambayo mkuu wa mkoa Homera anampigia kampeni mwana CCM za ubunge, nitakubaliana na kauli ya Mwabukusi na kumuomba Radhi hapa JF.
 
Unamlaumu nani?. CHADEMA kiliwafukuza wakaenda mahakama kuu, na spika kuwalinda ingawa sio wanachama. Sasa Kama watu wanalindwa na serikali unalaumuje upinzani?.
Huwezi kujua,mchezo wa siasa ulivyo, hivi unajua uwepo wao pale bungeni, ndio nafuu ya serikali yako kkt kuomba misaada huko nje? Hivi unajua uwepo wao pale una baraka zote ambazo wewe ,hoya hoya huwezi kuzijua kamwe? Baki kuwa hoya hoya huku watu wakikuonesha majumba yao na wakila bata
 
Hakuna mpinzani ,narudia tena hakuna mpinzani tanzania ,kama hujui jua sasa, labda mpinzani we wewe na dhiki zako
 
Wapiga kura kidogo sio tu wanaonesha raia hawaiungi mkono CCM bali hata upinzani pia hauungwi mkono, mana kama wangeupenda upinzani basi wangejitokeza kwa wingi sanaaaaaaa kwenda kuwapa kura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…