Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM



Unajua, ni rahisi kumshinda adui ikiwa wewe mwenendo wako mzima ni tofauti kabisa na adui?

Huwezi kumshinda adui ambae taa zikizimwa mkabaki wawili gizani (wewe na adui) wote mienendo yenu inakua Sawa bin sawia.
 


Safi. Huu ndio Ukweli na ushauri mujarab.

Tindo
 
Na hiki ndicho anachotaka Mwabukusi, kuwachanganya wapinzani kwa kuwatukana kila siku. Mpinzani gani unadai CCM ni Wazuri kuliko upinzani?. Yeye CCM hiyo hiyo imezuia maanadamano yake , Leo anadai ni wazuri. Shauri zake


Unamnukuu kinyume kabisa, unapotosha.


Amesema UPinzani ni mbaya kuliko CCM.

Tafsiri nyepesi kabisa ni kwamba CCM ni mbaya lakini Upinzani ni mbaya zaidi.
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu. Mtu anadhani upinzani wanaweza wote kuwa na mtazami mmoja
 
Reactions: RMC
nikimkumbuka mbunge flani wa viti maalum alivyompiga mumewe chini baada ya kuwa mbunge alafu kaolewa tena na kigogo wa chama chao ndiyo ninaamin ni maslay tu!
Sasa kama ni hivyo kwanini mnawaogopa sana watu wasiyo na uelekeo?
 
Kinacho fanya upinzani usiungane Tz ni kipi? Jibu ni tumbo, kila mtu anataka ajaze tumbo Lake kwanza, Mwabukusu yuko sahihi.
 
Mimi mpinzani yeyote anayewashambulia wapinzani wenzake kila siku, huku akiwasifu CCM huwa namuona ni pandikizi.


Tatizo la mashabiki wengi wa WANASIASA wa Tanzania ni hawana kabisa utulivu unaohitajika kwenye kusikiliza hoja na kuzijibu kwa ustahiki wake.


Wengi wako tayari muda wote kwa ajili ya ku protect a person/character (politician) badala ya ku defend the agenda/Sera.

Wako tayari ku attack personalities na kupelekea kuchafuana na kukaa mwisho wa siku kujiita wahanga wa siasa chafu.
 
ccm wako bungeni asilimia 100 wabadilishe sheria mbovu ambazo haziwajibishi waizi wa mali za umma hio lawama tena unawapa chadema hii ni kali
Ndiyo maana nilisema mjadala nawe kwangu utakuwa ni mgumu, kwa sababu unaweka mambo yasiyokuwepo; sijui kwa maksudi tu, au kukosa upeo wa unayo andika juu yake.

Nimekupa maswali ujibu, lakini badala ya kuyajibu, unapiga kivyako tu?

Sasa niambie, ni wapi nimewatwisha CHADEMA mzigo unaousema wewe, na kwa nini usifikiri kuwa nawatwisha mzigo huo hao hao CCM?
Kuna mahali popote nilipo andika kuwawekea kinga hao CCM?.
 
Hili halina ubishi. Liko wazi kabisa......
 
Sasa Mkuu Mwabukusi anapambana na nani na CCM au Wapinzani. Yaani uko vitani na Wenzako ghafula unawageuka na kuanza kuwashambulia, unategemea adui unampunguzia au unamuongezea nguvu?


Hajashambulia, amesema kile anachoamini yeye ni sahihi.

Ina maana Kama mko vitani na wenzako wakatenda makosa tofauti na inavyotakiwa, utaacha kuwaonya?

Na Kama ukiwaonya ndani ikashindikana kusikilizwa hutosema hadharani endapo ukipata nafasi ya kufanya hivyo? Huku ukiamini moyoni usemayo ni kweli tupu?
 
Kipindi billcanars inataifishwa, mashamba ya mbowe yanaharibiwa na mkuu wa wilaya kule hai, na kumbuka account za mbowe zimefungwa na zimefunguliwa wakati wa samia au kipindi hiko mbowe anafanyiwa hayo madhila ulikua bado mtoto
Haya sasa, unakielewa unacho eleza hapa?

Kwamba, Mbowe sasa atelekeze juhudi za chama alicho kiongoza kushika madaraka ya nchi na kuleta mageuzi, kwa vile sasa anafaidika na anachopewa yeye na hao hao waliokuwa wakimuumiza yeye binafsi siku zote?
Maana yako ni kwamba, bei ya Mbowe katika maisha yake ya 'kisiasa' sasa imekamilika, kwa hiyo hana sababu tena ya kuhangaika na shughuli za chama kukiwezesha kushika madaraka, ili aliyo kuwa akiyapigania miaka yote, kama mwanasiasa yatimie!

'Theme' hii ndiyo unayo ielezea tokea mwanzo wa maelezo yako katika mada hii. Mawazo ambayo ni kinyume kabisa na kuwa na mwanasiasa halisi anaye pigania anayo yaamini yeye na chama chake.

Unamhimiza Mbowe sasa aungane na CCM ya Samia, ili na yeye afaidi uhondo wa kuwapiga waTanzania.
 
So wewe unataka Mbowe, Lema, Lissu, Heche na Sugu waongoze hii nchi? hata mimi ningekuwa usalama wa taifa nisingekubali kamwe hao wahuni wapewe nchi
Kazi ambayo JK na Magufuli wameweza nani ataishindwa?
 
The Beetles mwaka 1969 waliimba wimbo BACK TO THE USSR huyu ananikumbusha. Kaonja joto ya jiwe, out of the frying pan into the fire, karuka mkojo kakanyaga mavi kweeeeli.
 
sasa kama wewe hunifahamu hilo tena si kosa langu , najua mmezoea kudanganywa , ila kuhusu mimi muulize Mwakyembe Kyela , mimi ndio nilimstaafisha siasa
Mkuu msimamo wako ni upi kuhusu chadema kushiriki uchaguzi mkuu na katiba hii na tume hii ya uchaguzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…