Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Tunaungana kwenye kushiriki chaguzi za haki, sio hizo za kwenda kupotezeana muda kisha kupewa viti viwili vitatu vya hisani ili kuhada umma na dunia kuwa Kuna demokrasia.

Ni hivi, tumechoka kuongozwa na chama hiki hiki miaka yote tena kwa shuruti. Tunataka chaguzi za haki anayeshinda ashinde kihalali, na sio kupotezea wanaume muda wao kwenye mistari ya kura, wakati mnalazimisha kuongoza kizazi kilichowachoka. Serekali inaweza kuundwa na watanzania wengine, sio lazima ccm bila ridhaa ya umma.


Unajua, ni rahisi kumshinda adui ikiwa wewe mwenendo wako mzima ni tofauti kabisa na adui?

Huwezi kumshinda adui ambae taa zikizimwa mkabaki wawili gizani (wewe na adui) wote mienendo yenu inakua Sawa bin sawia.
 
Logic is simple; Ukishakuwa Mfanyabiashara mkubwa tu, huwezi kuwa mwanaharakati wa mstari wa mbele sababu YOU HAVE SOMETHING TO LOSE. Wanaharakati wote duniani wa Mstari wa mbele, walikuwa ni watu toka vyuoni, wasomi, watu wa mtaani— sababu THEY HAD NOTHING TO LOSE, na sifa kuu ya mpigania haki frontline, anapaswa awe hana cha kupoteza.

CHADEMA miaka 15 iliyopita ilikuwa na watu wenye njaa, vijana wasomi, hawana kazi wala hawana mali, kina Mdee, Kina Nasari, Kina Heche, Kina Wenje leo wote hawa si 'masikini tena', ni wafanyabiashara, wana mikopo benki, wana international business connection, wanafamilia. USITEGEE WAINGIE FRONTLINE KAMWE.

Kinachotakiwa sasa ni hawa kina MBOWE, kina HECHE, MNYIKA, WENJE, wakae pembeni, waendelee kufanya biashara zao na kutajirika zaidi ili wawe wafadhili wa harakati za kisiasa za mstari wa mbele.

Katika mazingira ya sasa, CHADEMA imestuck, wataendelea kuwa wapinzani kama vyeo vya kuendelea kuwa na political influence tu inayowawezesha kujijenga kiuchumi tu.


Safi. Huu ndio Ukweli na ushauri mujarab.

Tindo
 
Na hiki ndicho anachotaka Mwabukusi, kuwachanganya wapinzani kwa kuwatukana kila siku. Mpinzani gani unadai CCM ni Wazuri kuliko upinzani?. Yeye CCM hiyo hiyo imezuia maanadamano yake , Leo anadai ni wazuri. Shauri zake


Unamnukuu kinyume kabisa, unapotosha.


Amesema UPinzani ni mbaya kuliko CCM.

Tafsiri nyepesi kabisa ni kwamba CCM ni mbaya lakini Upinzani ni mbaya zaidi.
 
Wewe na mkeo (kama unaye) huwa mnakubaliana kila kitu? Hao unaosema wapinzani kuna matoleo kadhaa kuanzia upinzani uliojengeka kwa misingi ya dini, dhehebu, kabila, vyama binafsi vya watu, maslahi binafsi, maslahi ya taifa nk kama wanaharakati walivyo na mirengo tofauti : feminism, usboga, vijana, dini nk. Hivyo haiwezekani wote wakawa na msimamo mmoja kwa kila jambo. Pia sio suala la kulaumu kwani kila mtu anatumia uhuru wake atakavyo mradi havunji sheria.

Hata mtu au chama kijifanye wajanja lakini mwisho wa siku kuzungumza na serikali hakuepukiki ikiwa unataka kupush ajenda ambayo mtu anadhani ina manufaa kwa nchi. Yeye zMwabukusi wacha ajidanganye kiwa anaweza kulazimisha anachotaka yeye ndicho hicho hicho kitimizwe tena na serikali iliyopo madarakani.
Mkuu umeongea ukweli mtupu. Mtu anadhani upinzani wanaweza wote kuwa na mtazami mmoja
 
  • Thanks
Reactions: RMC
nikimkumbuka mbunge flani wa viti maalum alivyompiga mumewe chini baada ya kuwa mbunge alafu kaolewa tena na kigogo wa chama chao ndiyo ninaamin ni maslay tu!
Sasa kama ni hivyo kwanini mnawaogopa sana watu wasiyo na uelekeo?
 
Kinacho fanya upinzani usiungane Tz ni kipi? Jibu ni tumbo, kila mtu anataka ajaze tumbo Lake kwanza, Mwabukusu yuko sahihi.
 
Mimi mpinzani yeyote anayewashambulia wapinzani wenzake kila siku, huku akiwasifu CCM huwa namuona ni pandikizi.


Tatizo la mashabiki wengi wa WANASIASA wa Tanzania ni hawana kabisa utulivu unaohitajika kwenye kusikiliza hoja na kuzijibu kwa ustahiki wake.


Wengi wako tayari muda wote kwa ajili ya ku protect a person/character (politician) badala ya ku defend the agenda/Sera.

Wako tayari ku attack personalities na kupelekea kuchafuana na kukaa mwisho wa siku kujiita wahanga wa siasa chafu.
 
ccm wako bungeni asilimia 100 wabadilishe sheria mbovu ambazo haziwajibishi waizi wa mali za umma hio lawama tena unawapa chadema hii ni kali
Ndiyo maana nilisema mjadala nawe kwangu utakuwa ni mgumu, kwa sababu unaweka mambo yasiyokuwepo; sijui kwa maksudi tu, au kukosa upeo wa unayo andika juu yake.

Nimekupa maswali ujibu, lakini badala ya kuyajibu, unapiga kivyako tu?

Sasa niambie, ni wapi nimewatwisha CHADEMA mzigo unaousema wewe, na kwa nini usifikiri kuwa nawatwisha mzigo huo hao hao CCM?
Kuna mahali popote nilipo andika kuwawekea kinga hao CCM?.
 
HAKUNA TOFAUTI KATI YA CCM NA WAPINZANI, NI WALEWALE" MWABUKUSI

Upinzani na CCM hawana tofauti, kitendo cha kutaka kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya ni kwa sababu ya maslahi binafsi na sio maslahi ya Taifa, ndio maana kuna chawa wa chama tawala na huku upinzani nako kuna machawa huku kwetu kwenye upinzani

Hakuna mtu yuko tayari kumwambia kiongozi wake kwamba anayoyafanya hayako sawa, hatuna hata mgambo lakini nakuhakikishia sisi wapinzani ni wabaya kuliko hawa walioko madarakani, tunaogopana kuambiana ukweli, sisi na CCM hatuna tofauti kabisa.

Najiuliza kwanini wapinzani tunashindwa kuonyesha msimamo?

kwanini twende kushiriki uchaguzi bila katiba mpya?

Nilishasema kuna biashara ya Demokrasia inafanyika hapa nchini"

Chanzo : Jambo Tv
Hili halina ubishi. Liko wazi kabisa......
 
Sasa Mkuu Mwabukusi anapambana na nani na CCM au Wapinzani. Yaani uko vitani na Wenzako ghafula unawageuka na kuanza kuwashambulia, unategemea adui unampunguzia au unamuongezea nguvu?


Hajashambulia, amesema kile anachoamini yeye ni sahihi.

Ina maana Kama mko vitani na wenzako wakatenda makosa tofauti na inavyotakiwa, utaacha kuwaonya?

Na Kama ukiwaonya ndani ikashindikana kusikilizwa hutosema hadharani endapo ukipata nafasi ya kufanya hivyo? Huku ukiamini moyoni usemayo ni kweli tupu?
 
Kipindi billcanars inataifishwa, mashamba ya mbowe yanaharibiwa na mkuu wa wilaya kule hai, na kumbuka account za mbowe zimefungwa na zimefunguliwa wakati wa samia au kipindi hiko mbowe anafanyiwa hayo madhila ulikua bado mtoto
Haya sasa, unakielewa unacho eleza hapa?

Kwamba, Mbowe sasa atelekeze juhudi za chama alicho kiongoza kushika madaraka ya nchi na kuleta mageuzi, kwa vile sasa anafaidika na anachopewa yeye na hao hao waliokuwa wakimuumiza yeye binafsi siku zote?
Maana yako ni kwamba, bei ya Mbowe katika maisha yake ya 'kisiasa' sasa imekamilika, kwa hiyo hana sababu tena ya kuhangaika na shughuli za chama kukiwezesha kushika madaraka, ili aliyo kuwa akiyapigania miaka yote, kama mwanasiasa yatimie!

'Theme' hii ndiyo unayo ielezea tokea mwanzo wa maelezo yako katika mada hii. Mawazo ambayo ni kinyume kabisa na kuwa na mwanasiasa halisi anaye pigania anayo yaamini yeye na chama chake.

Unamhimiza Mbowe sasa aungane na CCM ya Samia, ili na yeye afaidi uhondo wa kuwapiga waTanzania.
 
So wewe unataka Mbowe, Lema, Lissu, Heche na Sugu waongoze hii nchi? hata mimi ningekuwa usalama wa taifa nisingekubali kamwe hao wahuni wapewe nchi
Kazi ambayo JK na Magufuli wameweza nani ataishindwa?
 
HAKUNA TOFAUTI KATI YA CCM NA WAPINZANI, NI WALEWALE" MWABUKUSI

Upinzani na CCM hawana tofauti, kitendo cha kutaka kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya ni kwa sababu ya maslahi binafsi na sio maslahi ya Taifa, ndio maana kuna chawa wa chama tawala na huku upinzani nako kuna machawa huku kwetu kwenye upinzani

Hakuna mtu yuko tayari kumwambia kiongozi wake kwamba anayoyafanya hayako sawa, hatuna hata mgambo lakini nakuhakikishia sisi wapinzani ni wabaya kuliko hawa walioko madarakani, tunaogopana kuambiana ukweli, sisi na CCM hatuna tofauti kabisa.

Najiuliza kwanini wapinzani tunashindwa kuonyesha msimamo?

kwanini twende kushiriki uchaguzi bila katiba mpya?

Nilishasema kuna biashara ya Demokrasia inafanyika hapa nchini"

Chanzo : Jambo Tv
The Beetles mwaka 1969 waliimba wimbo BACK TO THE USSR huyu ananikumbusha. Kaonja joto ya jiwe, out of the frying pan into the fire, karuka mkojo kakanyaga mavi kweeeeli.
 
sasa kama wewe hunifahamu hilo tena si kosa langu , najua mmezoea kudanganywa , ila kuhusu mimi muulize Mwakyembe Kyela , mimi ndio nilimstaafisha siasa
Mkuu msimamo wako ni upi kuhusu chadema kushiriki uchaguzi mkuu na katiba hii na tume hii ya uchaguzi?
 
Back
Top Bottom