Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Mgawanyiko huu huko upinzani, ni kwa sababu ya afya njema na uchapa kazi hodari wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi katika kuyashughulikia matatizo ya wananchi...HAKUNA TOFAUTI KATI YA CCM NA WAPINZANI, NI WALEWALE" MWABUKUSI
Upinzani na CCM hawana tofauti, kitendo cha kutaka kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya ni kwa sababu ya maslahi binafsi na sio maslahi ya Taifa, ndio maana kuna chawa wa chama tawala na huku upinzani nako kuna machawa huku kwetu kwenye upinzani
Hakuna mtu yuko tayari kumwambia kiongozi wake kwamba anayoyafanya hayako sawa, hatuna hata mgambo lakini nakuhakikishia sisi wapinzani ni wabaya kuliko hawa walioko madarakani, tunaogopana kuambiana ukweli, sisi na CCM hatuna tofauti kabisa.
Najiuliza kwanini wapinzani tunashindwa kuonyesha msimamo?
kwanini twende kushiriki uchaguzi bila katiba mpya?
Nilishasema kuna biashara ya Demokrasia inafanyika hapa nchini"
Chanzo : Jambo Tv
Wapinzani hawana hoja yenye mashiko, hawaelewani, hawana diria wala hawana uelekeo kabsaa....