Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM


Hata Mimi naunga mkono Lissu apewe uwenyekiti na Mbowe astaafu kwa Sasa awe mshauri tu. Maana yeye ndio kasababisha yote haya.
 

Umeongea Jambo la msingi mkuu, nadhani wampe ushauri wa jinsi ya kufanya mambo. Ila kwa ninavyomuona sidhani Kama atapokea ushauri.
 
Hata Mimi naunga mkono Lissu apewe uwenyekiti na Mbowe astaafu kwa Sasa awe mshauri tu. Maana yeye ndio kasababisha yote haya.
Tatizo sio lissu bali watanzania wamelala usingizi wa pono
Lissu kapigwa risasi kuna mwananchi hata mmoja aliyetoka kuandamana

Lisu hana ujasiri wa mbowe hashindwi kuwakimbia na kuwaachia chama hapo kitendo cha yeye kwenda uamishoni baada ya uchaguzi wa 2020 lile lilikua doa kubwa kwake sana
 
Mkuu watu wanafiki sana. Mtu kakaa kwake, akina Lissu wanalimwa risasi na Mbowe kupewa kesi ya ugaidi na hasara nyingi tu, halafu anadai waote wachumia tumbo.
Wanataka wanasiasa wafanye kazi bure sasa familia zao zitaishije
Hii nchi ina-wajinga wengi sana ambao wanaupeo mdogo sana

Mtu mzima amekaa na familia yake amekunja nne alafu anataka wanaume wengine wampiganie bure
 
Sasa ataanzisha Chama kipi wakati yeye mwenyewe kashasema Upinzani ni kubaya kuliko CCM??
Ndo hapo sasa watu wanaumiza vichwa namna ya kuondokana na mfumo dhalim wa ccm ,yeye ndo anajiona yupo na akili kubwa kuliko watz wote mil 60.

Kama kweli unalipigania taifa huwezi kuja na maneno mepesi ya hivi , songa mbele na yule unaona mpo na mlengo mmoja huwezi fuata mstari wako na wengine wafuate mstari wao kama lengo ni moja mtakutana mbele simple, kutuhum vyama haina maana yoyote
 
Nimekutishia wapi?. Kukwambia siku yako inakuja nimekutishia?. Nimekuona sehemu unaikanja CHADEMA kijinga nikachukia Sana Tena kwenye suala sensitive wewe unafanya dhihaka. Ndio maana nikakwambia siku yako inakuja.
😄😄😄

Wewe unaipenda Chadema sisi Wenzako tulichangia kwa Jasho kubwa wakati imeasisiwa hivyo tuna Haki kuitaja kama tuzitajavyo Simba na Yanga
 
hivi kususa chaguzi, kususa kutumia mtandao fulani wa simu wakati fulani na hata kule nyuma kwenye kususa bunge la katiba kumewahi kusaidia chochote chadema au upinzani kwa ujumla?

Au kumewahi kubadili kitu chochote?

Tanzania tuna vyama vya siasa zaidi ya 22 vyenye usajili wa kudumu, kachama kamoja kususa uchaguzi kati ya hivyo vyote kataathiri nini unadhani?

Pale Jamuhuri ya Kenya,
Raila Odinga, aliwahi kususa uchaguzi wa marudio, aliambilia nini kama sio kubwekabweka tu.....

Pale Zanzibar,
Hayati Maalim Seiph Sharifu Hamad aliwahi kususa uchaguzi wa marudio, alifaidika na nini zaidi ya kubwekabweka tu.....

Understand the Vision and Mission of Tundu Antipas Lisu and forces bihind him on the move at kususa uchaguzi.

Atawapoteza vizuri mno huyu muungwana na mpotelee kusikojulikana nae akiwachungulia na kuwacheka kwa dharau akila bata na mabwenyenye huko ng'ambo......
 
Tatizo la jamaa anapenda short-cut na kufikiri maisha ni kitu kirahisi sana na anayemjaza huu ujinga ni msaliti dr slaa
Unaposema anajazwa ujinga na Dr Slaa inamaana Mwambukusi uwezo wake wa kuchanganua mambo ni mdogo?
 
Mimi binafsi naamini haki inapiganiwa na sio kususiwa hivyo washiriki uchaguzi mpaka kieleweke

Point ni kwamba unavyosusa they don't care kwa hiyo kususa sio suluhisho
 
Shida ya Mwabukusi anadhani upinzani ni lelemama. Anadharau kila mtu, kila siku ni kuponda upinzani tu. Ameita maanadamano kaona serikali ilivyomwekea ngumu, halafu anadai CCM ni Bora kuliko wapinzani. Sasa si ahamie CCM .
Na kwa maneno yao haya wenda ndo maana hata ayo maandamano hayakwenda vizuri, kwa kauli hizi hata yangeenda vizuri kwa vyama kadhaa kushiriki bado ingeonekaka yeye na watu wake ndo kila kitu
 
Wapinzani Tanzania ni janga ,hakuna mpinzani ,mnapotezewa muda tu

Punguza unafiki hakuna upinzani ndio kitu gani?. Mnataka upinzani ufanyeje?. 2020 mmejaza wabunge wa CCM bungeni na madiwani karibia wote wa CCM , halafu unaleta kauli za kinafiki hakuna upinzani.

Ingekuwa nusu ya wabunge wanatoka upinzani halafu wakapitisha mkataba wa DP world au mafao ya wenzi wa viongozi wakuu, huku mama mjamzito akifa kwa kukosa lakini na nusu? basi hata Mimi ningesema hakuna upinzani.

Ila mmejaza CCM kwenye vyombo vya maamuzi lakini lawama kwa upinzani. Mnataka upinzani wafanyeje?. Waanze harakati Kama za akina Prince Johnson wa Liberia enzi hizo?
 
Kama kweli watakubali kushiriki uchaguzi ujao bila katiba mpya,sitokuwa na sababu ya kuwa mwanachama wa upinzani,sitokuwa na sababu ya kwenda kwenye mikutano ya wapinzani kuwasikiliza wala kwenda kupanga foleni kumpigia kura yeyote mwanasiasa yeyote.
 

Mazingira ya Sasa hayaruhusu wananchi kuandamana. Mbona kipindi Cha JK watu waliandama Sana? Mpaka CHADEMA kikaitwa chama Cha kigaidi.
 
Umeongea Jambo la msingi mkuu, nadhani wampe ushauri wa jinsi ya kufanya mambo. Ila kwa ninavyomuona sidhani Kama atapokea ushauri.
Mtakua mmetekeleza wajibu wenu mwema na wenye nia njema kwake vizur sana.

Suala la kuuchukua ushauri na uzoefu huo na kuufanyia kazi linabaki kwake binafsi na publics itamuhukumu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…