Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Kwa majira haya Lissu hakupaswa kuwa CHADEMA
Mbowe hana nia ya dhati kwasasa kuinua upinzani.

Bora hata Lema alimchana kuwa asiwaamini ccm

Mbowe anazingua, ila mwabukusi kuita wapinzani ni wabaya kuliko CCM Hilo ni tusi baya na dharau. Aanzishe chama chake Sasa.
 
Lakini kuna nini cha uongo kasema? Mbona hata Lissu huwa anasema haya hasa kushiriki uchaguzi bila katiba mpya? Je ni wangapi wanakubaliana na Lissu?
Kama wasiposhiriki chaguzi za 2024/25 na kuiachia CCM unafikiri wao watabaki salama tena? Najua ndiyo matamanio ya CCM kuufuta upinzani kwa staili hii.
 
Narudia tena, hakuna mtu mwenye akili timamu ataendelea kushiriki hizi chaguzi za kipuuzi. Serekali kutumikia wananchi ni wajibu hata ingeingia serekali ya kijeshi itatumikia wananchi, as long as wanakusanya Kodi. Hapa tunazungumzia legitimacy ya umma. Unaweza kukaa madarakani bila ridhaa ya umma.

Tunapiga kura na kuwapa watu tuwatakao na sio hao wanaochomekwa na ccm kwa kunajisi uchaguzi. Kama issue ni serekali kutumikia wananchi, uchaguzi ni wa nini wakati hata mkoloni alikuwa na serekali?
sikiliza bunge kuna vifungu vingi vya sheria ya uchaguzi vimerekebishwa
 
Slaa anamdanganya sana huyu jamaa
Kwenye maisha hamnaga short-cut hasa kwenye mambo yanayohusu itikadi kama siasa

Kama anajiamini aanzishe chama chake asitake kutumia watu kama mgongo wa kufikia malengo yake maisha sio marahisi hivyo yaani chadema waache agenda zake wamfuate yeye mbona ni kituko na kichekesho

Shida ya Mwabukusi anadhani upinzani ni lelemama. Anadharau kila mtu, kila siku ni kuponda upinzani tu. Ameita maanadamano kaona serikali ilivyomwekea ngumu, halafu anadai CCM ni Bora kuliko wapinzani. Sasa si ahamie CCM .
 
sasa mwabukusi yeye 2025 atagombea wapi? nccr haipo tena imenunuliwa na ccm na yeye ameichamba, ACT zitto hawezi kumpokea kwasababu ...., ccm hawezi kuingia, chadema ndio hii anaichamba. au ameshakata tamaa kugombwa?
Kashaanza kuchanganyikiwa...anaanza kuona joto la sirikali...uwakili ukienda na mishe za kusaka ugali zitaathirika pakubwa!

Alidhani zile rhetorics za DPW zingetosha kuitisha sirikali...truth being revealed before him kwamba sirikali ni lidude likuubwa ambalo kushindana nalo inabidi uende kwa steps za tahadhari!
 
Yeye mwenyewe mwabukuzi ameona upinzani ulivyo mgumu, kashindwa kufanya maanadamano. Nadhani anapanic kwa ugumu uliopo.
Sidhani kama yupo anayejielewa atautilia shaka msimamo wa Adv. Mwabukusi, na ni ngumu sana kwa mtu mwenye msimamo wa aina ile, aliyeiweka mpaka nafsi yake rehani, kuchanganywa kundi moja na wapinzani maslahi wanaoutafuta utajiri kupitia siasa, hiyo ni sawa na kuchanganya maji na mafuta.

Huyu ameamua kusema kweli liwalo na liwe, kwani ameshaona dalili huko tuendako, ni wapinzani ndio wataanza kucheza ngoma za CCM na sio vice versa, CCM wameshajua hawa wakitaka kitu chelewa kuwapa mwishowe watageukana wenyewe, kwa sababu hawana misimamo ya pamoja.

Hiki ndicho Adv. Mwabukusi amekiona na kukilaani, na wala sio vinginevyo, ambacho kwangu ni ukweli mtupu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Yeye Boniface Mwabukusi yuko wapi kwani?

Ni m - CCM au naye ni mpinzani wa CCM?

Kama ni sehemu ya wanaopigana na CCM, basi kumbe sasa hata yeye ni mpinzani wa CCM.

Kama ni hivyo, basi huyu Mwabukusi anawalaumuje wenzake na kuacha kujilaumu mwenyewe?

Na kwa maoni yangu, tatizo kubwa la Boniface Mwabukusi ni kutaka mambo yafanyike kwa terms na conditions zake yeye na mwenzake Dr Slaa..

Na kwa kuwa mambo hayaendi kama wanavyotaka yaende, basi wameamua kubwatuka hovyo kulaumu wenzake..
 
Nasema hivi hakuna sifa yoyote ya kuungana wapinzani ili kupewa nafasi za hisani. Kama ushindani wa sera ndio ungekuwa unatoka mshindi hapa kwetu, Leo hii ccm isingekuwa madarakani, na hata kama ingekuwa isingekuwa na uwezo kufanya maamuzi itakavyo. Hilo neno sera mnalitumia kama fashion, lakini ccm haiko madarakani kutokana na sera, Bali sababu za kihistoria, na hasa hasa katiba mbovu ya chama kimoja.

Hizi chaguzi za kihayawani unazoziona, ni ili kuhakikisha ccm inaendelea kukaa madarakani huku kizazi kikiwa kimeichoka. Huo usanii kuwa mko madarakani kwa ajili ya sera, kawaambieni wale wajinga mnaowasomba kwenye malori. Zama za ccm kuendelea kukaa madarakani zilishapita na kizazi chake. Hivyo hizo chaguzi mnazolazimisha kukaa madarakani, fanyeni/shirikini na wenye huo mda mchafu. Na ukitaka kuamini hiki si kizazi Cha ccm, subiri uone idadi ndogo ya wapiga kira watakaojitokeza, kama ishara kuwa hamkubaliki na kizazi hiki tena.
uchaguzi chadema itashiriki ,na itashindwa kihalali
 
Logic is simple; Ukishakuwa Mfanyabiashara mkubwa tu, huwezi kuwa mwanaharakati wa mstari wa mbele sababu YOU HAVE SOMETHING TO LOSE. Wanaharakati wote duniani wa Mstari wa mbele, walikuwa ni watu toka vyuoni, wasomi, watu wa mtaani— sababu THEY HAD NOTHING TO LOSE, na sifa kuu ya mpigania haki frontline, anapaswa awe hana cha kupoteza.

CHADEMA miaka 15 iliyopita ilikuwa na watu wenye njaa, vijana wasomi, hawana kazi wala hawana mali, kina Mdee, Kina Nasari, Kina Heche, Kina Wenje leo wote hawa si 'masikini tena', ni wafanyabiashara, wana mikopo benki, wana international business connection, wanafamilia. USITEGEE WAINGIE FRONTLINE KAMWE.

Kinachotakiwa sasa ni hawa kina MBOWE, kina HECHE, MNYIKA, WENJE, wakae pembeni, waendelee kufanya biashara zao na kutajirika zaidi ili wawe wafadhili wa harakati za kisiasa za mstari wa mbele.

Katika mazingira ya sasa, CHADEMA imestuck, wataendelea kuwa wapinzani kama vyeo vya kuendelea kuwa na political influence tu inayowawezesha kujijenga kiuchumi tu.
 
Mgawanyiko huu huko upinzani, ni kwa sababu ya afya njema na uchapa kazi hodari wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi katika kuyashughulikia matatizo ya wananchi...

Wapinzani hawana hoja yenye mashiko, hawaelewani, hawana diria wala hawana uelekeo kabsaa....

Na hiki ndicho anachotaka Mwabukusi, kuwachanganya wapinzani kwa kuwatukana kila siku. Mpinzani gani unadai CCM ni Wazuri kuliko upinzani?. Yeye CCM hiyo hiyo imezuia maanadamano yake , Leo anadai ni wazuri. Shauri zake
 
sasa mwabukusi yeye 2025 atagombea wapi? nccr haipo tena imenunuliwa na ccm na yeye ameichamba, ACT zitto hawezi kumpokea kwasababu ...., ccm hawezi kuingia, chadema ndio hii anaichamba. au ameshakata tamaa kugombwa?

Mimi mpinzani yeyote anayewashambulia wapinzani wenzake kila siku, huku akiwasifu CCM huwa namuona ni pandikizi.
 
Na hiki ndicho anachotaka Mwabukusi, kuwachanganya wapinzani kwa kuwatukana kila siku. Mpinzani gani unadai CCM ni Wazuri kuliko upinzani?. Yeye CCM hiyo hiyo imezuia maanadamano yake , Leo anadai ni wazuri. Shauri zake
Focus na kile alichosema Adv. Mwabukusi wacha kumlaumu kwa kutoa maoni yake, au hutaki upinzani usemwe hata wakikosea? kufanya hivyo huoni ndio unazidi kuthibitisha ubinafsi walionao wapinzani anaousema Adv. Mwabukusi!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa, wote wachumia tumbo tu.

Ila wa report ya CAG mnawalamba matako. Mnafiki Sana. Bungeni mmejaza CCM , halmashauri zote na asilimia 96 ya vijiji na Mitaa ni CCM. Ila kil siku kuwasema upinzani na kuwalamba miguu wezi. Yani mwenye mamlaka mnamuogopa, ila mmebaki kuwasema wasiokuwa na mamlaka. Mnaboa Sana.
 
Back
Top Bottom