Hapana. Lazima vyama vya upinzani viingie kwenye uchaguzi ili kupata nguvu ya kupambana na chama tawala. Mawazo na msimamo wa adv. Mwabukusi ni sahihi, lakini, si sahihi sana kwa wakati huu. Mapambano katika uwanja ya vita lazima kubadili mbinu za medani mara kwa mara kutokana na wakati na mazingira.HAKUNA TOFAUTI KATI YA CCM NA WAPINZANI, NI WALEWALE" MWABUKUSI
Upinzani na CCM hawana tofauti, kitendo cha kutaka kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya ni kwa sababu ya maslahi binafsi na sio maslahi ya Taifa, ndio maana kuna chawa wa chama tawala na huku upinzani nako kuna machawa huku kwetu kwenye upinzani
Hakuna mtu yuko tayari kumwambia kiongozi wake kwamba anayoyafanya hayako sawa, hatuna hata mgambo lakini nakuhakikishia sisi wapinzani ni wabaya kuliko hawa walioko madarakani, tunaogopana kuambiana ukweli, sisi na CCM hatuna tofauti kabisa.
Najiuliza kwanini wapinzani tunashindwa kuonyesha msimamo?
kwanini twende kushiriki uchaguzi bila katiba mpya?
Nilishasema kuna biashara ya Demokrasia inafanyika hapa nchini"
Chanzo : Jambo Tv
Nashauri vyama vya upinzani, ... Njoo vijijini kama Chadema walivyofanya huko kanda ya ziwa, Rukwa na kwingineko. Waelimisheni Watanzania juu ya hali yao na wanavyostahili kuwa. Wataelewa. Na baada ya hapo ingieni kwenye uchaguzi huku mkiimarisha usimamizi wa zoezi au mchakato mzima wa kura. Nendeni wilayani Nkasi mkajifunze Wananchi walifanyaje hadi Serikali na Chama tawala wakasalimu amri mwaka 2020 hata mwanamke, tena binti mdogo tuu Aidah Kenani akamgaragaza kwa aibu aliyekuwa mbunge machachari na maarufu Ally Kessy Mohamed. Inawezekana.
Kimsingi, Wananchi walikwishaichoka CCM na Serikali yake. Wanataka mabadiliko. Lakini, ni nani atakayewaongoza kuleta mabadiliko hayo? Ni Chama gani? Hawa hawa wachumia-tumbo Chadema, ACT, TLP, and the like?!
Anyway, vyama vya upinzani hamjachelewa bado, ingieni vijijini, "mwageni sumu" kwa Wananchi; wataelewa na kukisubiri CCM kwenye sanduku la kura.
Mwabheja sana!