Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Sio kufeli wewe unaweza ishi bila ela nijibu hili swali
Siasa ni kazi na career kama zilivyo nyingine wanastaili kupata chochote kile unafikiri kusimama majukwaani na kushawishi watu ni kazi rahisi jaribu uone
Nakwambia hukijui unachotetea, wala madhara yake. Kama unapenda pesa, siasa sio mahala pake kafanye biashara.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
HAKUNA TOFAUTI KATI YA CCM NA WAPINZANI, NI WALEWALE" MWABUKUSI

Upinzani na CCM hawana tofauti, kitendo cha kutaka kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya ni kwa sababu ya maslahi binafsi na sio maslahi ya Taifa, ndio maana kuna chawa wa chama tawala na huku upinzani nako kuna machawa huku kwetu kwenye upinzani

Hakuna mtu yuko tayari kumwambia kiongozi wake kwamba anayoyafanya hayako sawa, hatuna hata mgambo lakini nakuhakikishia sisi wapinzani ni wabaya kuliko hawa walioko madarakani, tunaogopana kuambiana ukweli, sisi na CCM hatuna tofauti kabisa.

Najiuliza kwanini wapinzani tunashindwa kuonyesha msimamo?

kwanini twende kushiriki uchaguzi bila katiba mpya?

Nilishasema kuna biashara ya Demokrasia inafanyika hapa nchini"

Chanzo : Jambo Tv
Mada za namna hii, kijumla jumla, bila ya uchambuzi wowote chini yake unakwa hauna msaada sana kwa wanaozisoma.

Sote sasa tunaelewa kuna matatizo huko CHADEMA (ndio upinzani pekee uliokuwa umebaki). Uchambuzi wa kina kuhusu matatizo yaliyoingia kwa ghafla ndani ya chama hicho na kuzima matumaini ya kuiondoa CCM kwenye madaraka ungefaa sana, kuliko hivi vipande vya ulalamishi pekee.

Je, sasa kwa kuwa CHADEMA nao wamekuwa sehemu ya CCM, waTanzania wafanye nini kupambania taifa lao?
Hizi ndizo mada zinazotakiwa kujadiliwa humu wakati huu; tena kwa haraka, maana muda ndio huo unakatika sasa.

Maoni yangu juu ya hili ni kwamba, huko ndani ya Upinzani (CHADEMA); kama ilivyo ndani ya CCM yenyewe, kuna waTanzania wanaoumia sana kuona mwelekeo wa taifa letu unavyokwenda sasa hivi.

Je, kuna njia yoyote ya kuwatia moyo hawa wote ili ndio kiwe chanzo cha ukombozi wa nchi yetu?
 
Afadhali umejua kwamba wapinzani ni wabaya kuliko ccm, sasa nimsikie mtu anasem ccm ni wabaya
 
Mkuu, Mwabukusi anatokea Mbeya. Kwenye uchaguzi mdogo wa mbarali viongozi wa CHADEMA wa wilaya na hata mkoa wakiwemo wanachama waliimba chama kishiriki, CHADEMA kikagoma kishiriki. Leo anatokea mtu wa Mbeya hapo hapo na kuanza kubeza hata hicho kidogo. Juzi CHADEMA wametukanwa na Rais Samiah kwa kugomea mkutano wa vyama vya siasa , halafu hata kuapriciate hakuna. Mwabukusi hapana, anafanya kazi ya Makonda. Aende zake huko.
Umekuwa mkali sana mpaka huioni mantiki ya kile alichokisema Adv. Mwabukusi.

Kwani hujawasikia baadhi ya viongozi wa Chadema wakiwa tayari kuwaondoa wabunge wa CCM majimboni, licha ya kujua chama chao kilisema hakitashiriki uchaguzi mpaka Katiba Mpya ipatikane?

Wapo hao watu, ndio maana nakwambia alichokisema Adv. Mwabukusi kina ukweli.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Nakwambia hukijui unachotetea, wala madhara yake. Kama unapenda pesa, siasa sio mahala pake kafanye biashara.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Watu wa aina hiyo, (huyo uliye mjibu), ndio waliojaa tele kwenye kinachoitwa "siasa" hapa Tanzania. Hakuna mwenye 'conviction" yoyote juu ya anacho kisimamia katika siasa, bali manufaa yake binafsi.
 
Usipoziba nyufa zenu kama wapinzani ni vigumu sana kuwashinda CCM mkiwa hampo organised, na hii inasababishwa na tamaa ya ubunge anayoilaumu Adv. Mwabukusi, kuwa na msimamo usioyumba wa kile unachopigania ni muhimu sana,hapo ndipo CCM hushtuka.

Lakini uliona Samia anasema kule ndani kwao hapajatulia, ujue ameshawapima uzito akajua kilo zenu, hamumtishi tena, ndio maana Adv. Mwabukusi anawataka kurudi kwenye drawing board muangalie mnakosea wapi, yuko sahihi kabisa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Sasa Mkuu kwa maoni yako Adv.Mwabukusi anatoa hoja zenye kujenga ili kuimarisha Upinzani au anatoa Hoja za kubomoa ili kudhoofisha Upinzani??

Kwa maoni yangu Mimi ni kwamba kwenye Timu ya mpira, Mwenzenu akipiga mkwaju wa penalty bahati mbaya mpira ukapaa na kutoka nje hupaswi kumshambulia mpigaji wala wale waliompendekeza awe mpigaji. Bali mnamtia moyo kisha mnasonga mbele. Kwa kufanya hivyo anaweza kuja kufunga goli zuri bila kupitia mkwaju wa penalty.

Adv. Mwabukusi anakosea sana kwa kuwashambulia wenzake wanaohangaika kwa kutumia mbinu mbali mbali ikiwemo majadiliano kuhakikisha wanapata mabadiliko ya kweli kwenye Siasa za Nchi yetu.
 
Umekuwa mkali sana mpaka huioni mantiki ya kile alichokisema Adv. Mwabukusi.

Kwani hujawasikia baadhi ya viongozi wa Chadema wakiwa tayari kuwaondoa wabunge wa CCM majimboni licha ya kujua chama chao kilisema hakitashiriki uchaguzi mpaka Katiba Mpya ipatikane?

Wapo hao watu, ndio maana nakwambia alichokisema Adv. Mwabukusi kina ukweli.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Natamani sana uliyemjibu hoja zake akusome kwa makini na akuelewe ulicho kiandika hapa.
Katika hali ya kuwa 'frustrated' na mienendo ya baadhi ya viongozi ndani ya chama, isiwe ndiyo sababu ya kulaani kila kitu na kutupa mikono hewani.

Haya ni mapambano; huwezi kukimbia uwanja wa mapambano kwa sabbbu kuna baadhi ya watu wameuza roho zao kwa shetani
Najua mkuu 'econonist' analitambua hili.
 
Najiuliza kwanini wapinzani tunashindwa kuonyesha msimamo?
Hili nililisema mapema. Sisi wengine tunajuana vema. Lililobaki ni ubabaishaji tu. Hata haya maneno nayaona ni kutafuta visingizio tu. Maskini Tanzania.
 
Wapiga kura kidogo sio tu wanaonesha raia hawaiungi mkono CCM bali hata upinzani pia hauungwi mkono, mana kama wangeupenda upinzani basi wangejitokeza kwa wingi sanaaaaaaa kwenda kuwapa kura
Kwa taarifa yako hao wapiga kura wachache ndio huwa wa ccm, Bali hupora za wapinzani. Kwakuwa wapinzani kuendelea kushiriki hizo chaguzi kunawapa ccm uhalali baada ya kupora kuwa wanaaungwa mkono na watu wengi, ni Bora waende hao wachache ili ifahamike ccm haikubaliki.

Ifahamike wapinzani hawana uwezo wa kulinda kura zao, kwani wanaoshiriki huo wizi ni vyombo vya Dola vyenye silaha. Kwahiyo hakuna haja ya wapinzani kuendelea kubambikiwa kesi, kuumizwa na vyombo vya dola, na vikundi vya uvccm vyenye backup ya vyombo vya Dola.
 
Sasa Mkuu kwa maoni yako Adv.Mwabukusi anatoa hoja zenye kujenga ili kuimarisha Upinzani au anatoa Hoja za kubomoa ili kudhoofisha Upinzani??

Kwa maoni yangu Mimi ni kwamba kwenye Timu ya mpira, Mwenzenu akipiga mkwaju wa penalty bahati mbaya mpira ukapaa na kutoka nje hupaswi kumshambulia mpigaji wala wale waliompendekeza awe mpigaji. Bali mnamtia moyo kisha mnasonga mbele. Kwa kufanya hivyo anaweza kuja kufunga goli zuri bila kupitia mkwaju wa penalty.

Adv. Mwabukusi anakosea sana kwa kuwashambulia wenzake wanaohangaika kwa kutumia mbinu mbali mbali ikiwemo majadiliano kuhakikisha wanapata mabadiliko ya kweli kwenye Siasa za Nchi yetu.
Kwangu Adv. Mwabukusi anatoa hoja za kujenga upinzani, kwasababu anawaonesha makosa yao ili wayarekebishe then wasonge mbele, usiogope kuambiwa ukweli kwa kuhofia upinzani utayumba, kwangu hizo ni siasa za kuviziana na za kiuoga, zisizo na maana.

Tazamaneni usoni muambizane ukweli, ili mtakapokwenda kupambana na mpinzani wenu wote muwe kitu kimoja, sio hizi sasa wengine wanawaza Katiba Mpya kwanza, wengine wanawaza kuwaondoa wabunge wa CCM majomboni mwao, hii haitakiwi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hivi CHADEMA imeshiriki uchaguzi gani?. Tuwe serious kidogo. Wanaoshiriki so wanajulikana?. Kwanini asiwaseme moja kwa moja?
Kasema wapinzani, hajawataja kwa majina,
Ila naona CHADEMA mnapiga kelele 🤣🤣🤣
 
kwamba kwenye Timu ya mpira, Mwenzenu akipiga mkwaju wa penalty bahati mbaya mpira ukapaa na kutoka nje hupaswi kumshambulia mpigaji wala wale waliompendekeza awe mpigaji. Bali mnamtia moyo kisha mnasonga mbele. Kwa kufanya hivyo anaweza kuja kufunga goli zuri bila kupitia mkwaju wa penalty.

Adv. Mwabukusi anakosea sana kwa kuwashambulia wenzake wanaohangaika kwa kutumia mbinu mbali mbali ikiwemo majadiliano kuhakikisha wanapata mabadiliko ya kweli kwenye Siasa za Nchi yetu.
Nimekuelewa.
Kiufupi ni hivi:
Huyo mchezaji mwenzenu kwenye timu, kama anaonyesha dalili za kuwachimba wenzake, au kufifisha lengo lenu la ushindi, hiyo ni sababu tosha kabisa ya kutompa nafasi kwenye timu.

Haya ya "...majadiliano kuhakikisha wanapata mabadiliko ya kweli kwenye siasa..."; inashangaza kweli kuyaandika maneno kama hayo uliyo andika hapa!
Hata sijui unalenga kitu gani hasa!.
 
Watu wa aina hiyo, (huyo uliye mjibu), ndio waliojaa tele kwenye kinachoitwa "siasa" hapa Tanzania. Hakuna mwenye 'conviction" yoyote juu ya anacho kisimamia katika siasa, bali manufaa yake binafsi.
Kama watu wa aina hiyo ndio wapo kwenye siasa zetu, basi tunapotezeana muda. Tumeigeuza siasa kama kijiwe cha wacheza karata.

Hatutasogea popote.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Yuko sahihi, na hii tabia imedhohofisha sana upinzani na kuwakatisha tamaa wapiga kura.

Kwa hii tabia CCM Itatawala milele yote.
Wapinzani wangekuwa siriaz hadi leo hii CCM ingekuwa Chama cha upinzani.

Unampigia kura leo mpinzani kwa lengo la kuimarisha demokrasia kesho anahamia CCM.

Ndio maana CCM inatumia viruzuku tu kuwamaliza Wapinzani.

RIP. Christopher Mtikila, kidogo alikuwa siriaz.
Mkuu hayo ni matatizo ya Mtu moja mmoja na sio msimamo wa Upinzani kununuliwa na chama cha Mapinduzi baada ya kushinda uchaguzi.
 
Yupo sahihi , Siasa ni Biashara ndio mana Lowasa pamoja na Makando kando yale yote bado Chadema wali mpick kama Flag bearer wao
 
Mada za namna hii, kijumla jumla, bila ya uchambuzi wowote chini yake unakwa hauna msaada sana kwa wanaozisoma.

Sote sasa tunaelewa kuna matatizo huko CHADEMA (ndio upinzani pekee uliokuwa umebaki). Uchambuzi wa kina kuhusu matatizo yaliyoingia kwa ghafla ndani ya chama hicho na kuzima matumaini ya kuiondoa CCM kwenye madaraka ungefaa sana, kuliko hivi vipande vya ulalamishi pekee.

Je, sasa kwa kuwa CHADEMA nao wamekuwa sehemu ya CCM, waTanzania wafanye nini kupambania taifa lao?
Hizi ndizo mada zinazotakiwa kujadiliwa humu wakati huu; tena kwa haraka, maana muda ndio huo unakatika sasa.

Maoni yangu juu ya hili ni kwamba, huko ndani ya Upinzani (CHADEMA); kama ilivyo ndani ya CCM yenyewe, kuna waTanzania wanaoumia sana kuona mwelekeo wa taifa letu unavyokwenda sasa hivi.

Je, kuna njia yoyote ya kuwatia moyo hawa wote ili ndio kiwe chanzo cha ukombozi wa nchi yetu?
Inaonekana njia ya kuwaondoa watanzania kwenye huu mkwamo ni kuanzisha chama kipya [ maoni ya wengi humu ndani].

Lakini nionavyo, hicho chama kipya hata kama kitaanzishwa, kiwe kutokea Mbeya au Sumbawanga, kama bado mazingira yanayozunguka siasa zetu yataendelea kubaki kama yalivyo sasa, basi tusitegemee badiliko lolote.

Hicho chama kitaanzishwa, kitakutana na hizi sheria mbovu za uchaguzi, matokeo yake nacho kitakuwa "neutralised" kama ambavyo tunaona Chadema imekuwa neutralised kwa sasa.

Lazima kwanza tuufumue mfumo wa siasa zetu, sheria kandamizi zote ziondolewe, how? hilo swali namuachia kila mmoja ajiulize, wala sio kwa Samia kupeleka muswada bungeni, yale ni maigizo matupu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Nakwambia hukijui unachotetea, wala madhara yake. Kama unapenda pesa, siasa sio mahala pake kafanye biashara.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Wewe huku unalipwa mshahara, unataka wanaume wenzako wakupiganie bure

Na-nikusaidie wanasiasa wote ni wafanyabiashara sababu huwezi pata mda wa kwenda majimboni huko kama wewe ni mwajiriwa mfano angalia mbowe, boniphase, heche, lema, zitto n.k wote hawa wana-biashara zao

Huwezi kuwa mwajiriwa huku unafanya siasa sababu hakuna mwajiri atakayekupa ruhusa za kila mara kwenda kufanya mikutano ya siasa huku kazi zinakusubiria mara umekaa korokoroni wanasiasa wote ni wafanyabiashara kama hulikua hulijui na hata mwabukusi ni mwanasheria wa kujitegemea hajaajiriwa na mtu

Kama sio mfanyabiashara na umejiajiri kazi ya siasa itakua ngumu sana kwako
 
Back
Top Bottom