Wakili Peter Madeleka amtumia Ujumbe Tundu Lissu kuhusu kesi ya Dkt. Slaa

Wakili Peter Madeleka amtumia Ujumbe Tundu Lissu kuhusu kesi ya Dkt. Slaa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Screenshot 2025-01-22 172908.png

Wakili Peter Madeleka ameandika "Nitamuomba JENERALI Tundu Lissu ASIFANYE TAFRIJA ya KUSHEREKEA USHINDI WA CHADEMA mpaka DR. WILBROAD SLAA ATOKE GEREZANI. Ni muhimu pia DPP akahudhuria TAFRIJA hiyo."

===================================

Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam leo Jumatano Januari 22, 2025 imesimamisha uamuzi wa kesi inayomkabili mwanasiasa maarufu nchini, Dk Wilbrod Slaa, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, iliyopangwa kutolewa kesho pamoja na mwenendo wa wote wa kesi hiyo.

Hatua hiyo inatokana na mashauri mawili tofauti aliyoyafungua Dk Slaa mahakamani hapo kupitia mawakili wake kutokana na kutoridhishwa na namna Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili, jinsi anavyoiendesha.

Dk Slaa amefungua mashauri hayo ya maombi Mahakama Kuu kufuatia uamuzi wa Hakimu Nyaki kuridhia mapendekezo ya upande wa mashtaka katika kesi hiyo kuwa usikilizwaji wa maombi yao ( upande wa mashtaka) kupinga Dk Slaa kupewa dhamana yasikilizwe baada ya uamuzi wa pingamizi la Dk Slaa kuhusiana na uhalali kesi hiyo.

Hivyo, kupitia kwa mawakili wake amefungua mashauri mawili ya maombi Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura.

Chanzo: Mwananchi
 
Lissu hawezi kufanya tafrija hili ni jukumu zito amepewa
 
niko nae hapa mheshimiwa antipas na pia kanambia hili swala anaingia yeye mzgoni akiwa kama mtaalamu wa sheria duniani ko slaa atatoka hata waite wanasheria wao na waliopo shuleni. maaanina!!
 
Spana alizowapiga club house zimewauma sana mpaka wameamua wamnyime dhamana , wavunje katiba na sheria waziwazi .
 
Back
Top Bottom