Wakili Serikali Mulwambo: Mantiki sahihi ni kuingalia IGA dhidi ya katiba ya Tanzania na siyo sheria za Tanzania

Unaposema huwezi kutumia sheria za ndani kuvunja mkataba wa kimataifa, kwa nini jaji ametoa hoja ya kufanya marekebisho kwenye vipengele vya ule mkataba, badala ya kuwapa ushindi wa moja kwa moja Jamhuri?
Mkuu Denoo J nimefurahi kukuona hapa, hebu turudi kwenye mada:

Mahakama kutoa ushauri siyo sawa na kutangaza kuwa mkataba ni batili. Mara nyingi mahakama hata kwenye kesi za kikatiba huwa haitangazi moja kwa moka kwamba sheria fulani ni batili kwasababu tu inakinzana na katiba ya nchi. Huwa inatangaza haki za wadai, inalishauri bunge juu ya hiyo sheria, inatoa mapendekezo na kuirudisha hiyo sheria irekebishwe na bunge.

Muda ukipita bila bunge kurebisha hiyo sheria basi inapigwa chini moja kwa moja. Lakini, fahamu kwamba mbali na nguvu ya mahakama kutoa haki, haiwezi kupoka madaraka ya mihimili mingine. Haya madaraka kisheria tunaita "Prerogatives". Hili liliwekwa wazi kwenye kesi za katiba za miaka ya 90's. Hebu tukazipitie, tutaona hili nalosema hapa. Huu ndiyo uelewa wangu wa kawaida wa sheria za katiba, kama nakosea naomba nirekebishwe.

Sasa mambo kama " War, Diplomacy, Treaties", yanaangukia kwenye nguvu za moja kwa moja za serikali (Prerogative of the Executive). Mikataba ya kimataifa huingiwa kwa kupitia sheria za kimataifa, hivyo hata kuuvunja inabidi utumie sheria za kimataifa, siyo vinginevyo. Hii ndiyo kanuni kuu ya sheria za kimataifa, kwenye suala la mikataba (Pacta-Sunt-Servanda). Bunge na serikali vitashauriwa na mahakama, ila mahakama haiwezi kamwe kuvunja mkataba.

Hili likiruhusiwa basi fahamu kwamba, dunia nzima itakuwa na matatizo kwasababu mataifa mengi yataenda mahakamani kujaribu kuvunja mikataba kiholelea wakitumia mwanya wa katiba. Marehemu Kanali Ghadafi aliingia kwenye mgogoro mkubwa miaka ya 1960's, 1970's na 1980's baada ya kuvunja mikataba ya uwekezaji ambayo iliachwa na Mfalme Idriss. Kesi zilikuwa ni nyingi mno hadi Libya akazidiwa. Ukienda mtandaoni utazikuta ziko nyingi tu, zisome.

Kule Urusi, wakomunisti baada ya kupindua nchi, waliamua kukataa mikataba ya kimataifa ya madeni. Walikataa kulipa na kusema ni mikataba wa kinyonyaji, wakomunisti na ujeuri wao waliifanya nchi yao, iingine kwenye Debt-Default jambo ambalo walilijutia sana. Hivyo basi inabidi tuzingatie haya yafuatayo:

1. Mikataba ya kimataifa huvunjwa kwa kutumia sheria za kimataifa.
2. Mikataba ya kimataifa inaweza kuvunjwa endapo bunge likaamua kuishurutisha serikali.
3. Mikataba ya kimataifa inabidi ijadiliwe sana na bunge kabla ya kupitishwa (Before Ratification)

NB: Kama ingekuwa ni rahisi hivi, basi Marehemu Magufuli angeivunja yote huko mahakamani.
 
Mkuu mbona unakuwa mkali, nini shida? Mwenzako kasema wote sio Mwambukusi na wenzake tu, na amewagusa hata hao majaji na katoa sababu na kueleza mapungufu ya pande zote. Sasa wewe unakuja na mapovu- tulia leta hoja majadala uende
 
Mkuu kwa kesi yetu concession contract au investment contract hazijafikiwa bado- kwa hiyo reference ya Kenya naiona kama ni irrelevant
Uhalali wa Concession au International Commercial Contract hutoka kwenye Bilateral Investment Treaty au Multilateral Investment Treaty. Hapa kwetu hatuna BIT hivyo uhalali wa HGA/Project Agreement lazima utatokana na IGA. Kwenye sheria za uwekezaji, kinachofanya HGA/Concessions/Commercial Contract ziwe kitu kimoja na BIT/IGA/MIT ni vipengele viitwavyo, UMBRELLA CLAUSE na STABILIZATION CLAUSES.

Mkataba wa Vienna 1969, umeweka wazi kabisa kuhusu hili na ndiyo utaratibu ulivyo. Mkataba wowote ule wa kimataifa wa uwekezaji au jambo jingine, uwe ni BIT/IGA au Concession/Contract/HGAs ambazo ziko chini ya BIT/IGA/MITs vinaweza kuvunjwa chini ya sheria za kimataifa. Nashangaa ambavyo bado mnaendelea kukomaa tu.
 
Asante.

Kwa maelezo uliyotoa, tayari yanaenda kinyume na kile jaji alichofanya, pamoja na kuliagiza bunge likafanye marekebisho, lakini jaji hakutoa haki kwa wadai, au utuambie hapa, ni ipi extent ya haki ya wadai, kuna ubaya kwangu kuita haki ya wadai ni sawa na wao kushinda kesi?
 
Ninaona shida yako iko wapi- unajadiliana na watu ambao wanakwenda hatua kwa hatua katika safari ambayo wewe umeshapita mara nyingi. Ulishaangalia mararudio ya mechi na mtu ambaye ndiyo mara ya kwanza anaiingalia? Utakuwa unamwambia sasa hapo goli linaingia sasa, na hiyo siyo sawa.
Ukweli hatuna tayari HGA/ CONCESSION/LEASE CONTRACTS kwa hiyo hatuna mfanano wowote na Kenya
 
Mkuu, Denoo J, you're bigger than this,

Hakuna anayedharau hoja za Advocate Mwabukusi, mimi mwenyewe nimewaunga mkono na nitaendelea kuwaunga mkono. Ila tunapotofautiana mimi ni ninyi ni kwamba, mimi ni Mwanasheria hivyo nachangia kama Mwanasheria. Hayo ya siasa na mengineyo siyo yangu.

Kesi ilikuwa na hoja tano, baadhi ya zile hoja kama CAPACITY OF PARTIES na STATUS OF IGA hazikuwa na usahihi wowote ule kwenye sheria za kimataifa. Hata hivyo kuna baadhi ya sheria kama mkataba wa Vienna 1969, ambao ndiyo sheria ya msingi kabisa kwenye kutafasiri mikataba hawakuitumia, wenyewe wametumia The Law of Contract Act, The Constitution etc.

Wangeutumia ule mkataba wangepata uwanja mpana maana hata ule mkataba nao ni sehemu ya sheria za nchi yetu ambazo bunge ziliipitisha (Domesticated) kipindi cha Mze Nyerere. Kutokuutumia kumechangia kwa sehemu kubwa baadhi ya hoja zao kuwa dhaifu. Huu ndiyo ukweli wenyewe. Jambo jema kabisa kutegemea sheria za rasilimali (Natural Wealth Protection Laws) na sheria za manunuzi (Procurement Laws), lakini kwasababu huu ni mkataba wa kimataifa ni lazima ungetumia mkataba wa Vienna ambao ni sehemu ya sheria za Tanzania.
 
Mkuu Comte, nitasema mara ya mwisho kabisa,

Mkataba wetu wa uwekezaji wa DP-World unatokana na IGA baina ya Tanzania na Dubai. Kitaalamu hii IGA is a sectoral investment agreement. Kama huu mkataba siyo halali hata utekelezaji hauwezi kuwa halali. Kanuni ambazo zinatumika kuvunja mkataba wa uwekezaji mkubwa (IGA) na mdogo (HGA) ziko sawa endapo uwekezaji huo umefanya ukiukwaji wa sheria.

Kukusaidia tu, kapitie The ICSID Convention, LCIA Rules, UNICITRAL Rules, Vienna Convention, na World Bank Guidelines on Treatment of Foreign Direct Investment, kote utaona kwamba kanuni zinazovunja mkataba mkubwa wa uwekezaji (BIT/MIT) ndizo hizo-hizo zinavunja mkataba wa utekelezaji (Concession/HGA/Contract).

Binafsi, nimeshatoa mchango wangu wa kile ninachokifahamu. Kama Mkristo naamini nimeshatimiza wajibu wangu, hivyo nanawa mikono kama Pilato. Mkiamua kuwa makini na kufuata weledi, itakuwa vyema, mkikataa pia, hewalaaaa mimi sipungukiwi na chochote.

Uwe na siku njema mkuu.

 
Mkuu Denoo J, uwe na siku njema,
Mimi hapa nimeshamaliza lililonileta sasa naenda kutekeleza majukumu mengine.
 
Namuomba Moderator aupandishe uzi huu na kuuweka kama quote kwenye first post.

Inassidia kufungua mianya ya intellectual convos
 
Hata kama angevunja kuna sunset clause ambayo italinda maslahi ya watu na naomba ieleweke kwamba sio kila mwekezaji ni tapeli na sio kila mzungu ni ni mwizi wa mali za Tanzania kwa hiyo sio kila ngozi nyeupe ni mzungu
 
Ok, hebu twende sawa..

Hapa kuna point ya wazi kabisa ambayo nakuona una miss, unashindwa kutofautisha ni wakati gani zitumike sheria za kimataifa, na wakati gani zitumike sheria za ndani.

Mfano tukiangalia shauri lililotolewa hukumu leo mahakamani, wale wapeleka maombi walikuwa wanalalamika juu ya sheria za ndani zilizovunjwa wakati wa kuingia ule mkataba wa IGA, na kwa mantiki hii, kwangu kwao kuonesha hizo sheria kwa kutumia Law of Contract Act na nyinginezo ni sahihi kabisa, kwamba ndio zimevunjwa.

Hawakutakiwa kutumia sheria za nje wakati wale walikuwa wanailalamikia serikali yetu, ambapo kama wangeshinda ile kesi, na mahakama kutoa order ile IGA ni batili...

Sasa hapo serikali yetu ndio ingetakiwa kwenda kwenye hayo mabaraza ya nje ya usuluhishi, ambapo huko, hizo sheria za kimataifa kama Vienna Conventions na nyinginezo ndio hutumika, pale ambapo serikali yetu inakuwa ikitaka kuvunja ule mkataba wa hovyo dhidi ya waarabu wa Emirati..

Naamini unaielewa pointi yangu, ndio maana nikaona kama una under-estimate kwa namna fulani kazi nzuri iliyofanywa na wakina Adv. Mwabukusi na wenzake, kwa kutoielewa hiyo concept, kazi ambayo imesababisha jopo la majaji kutoa maelekezo kwa bunge nini wakafanye.

Kwangu ni hayo tu.
 
Ni stahiki yako ila wakati mwingine tumia lugha laini ila ujumbe wako ufike
Mimi nafikiri tumeshatumia lugha laini sana Tanzania kilibaki ni kukatipia ili watu waamke kutoka kwenye usingizini wa upumbavu
 
Mimi nafikiri tumeshatumia lugha laini sana Tanzania kilibaki ni kukatipia ili watu waamke kutoka kwenye usingizini wa upumbavu
Mkuu kwa kuwa humu ukizdi sana una 28 yrs na Tanzania ina 62 years
 
Hauko sawa, yaani wakristo wanasema hawawezi kuvunja ndoa kwa sababu imefungwa kiislam halafu wewe best man unapeleka hiyo kesi vatican ili iweje?
 
Hauko sawa, yaani wakristo wanasema hawawezi kuvunja ndoa kwa sababu imefungwa kiislam halafu wewe best man unapeleka hiyo kesi vatican ili iweje?
Mantiki ya kile nilichoandika ni hiki..

Mkataba wa IGA una matatizo, unakiuka sheria zetu za ndani, ndipo wapeleka maombi kina Adv. Mwabukusi na wenzake wakaenda mahakamani kuiomba mahakama iseme ule mkataba wa IGA ni batili, kwa kuonesha baadhi ya sheria zetu za ndani zilizokiukwa, kama Contract Act, na nyingine..

Baada ya hapo haki ya wapeleka maombi ikipatikana, ndio waende mbele, ambapo sasa itakuwa ni baada ya mkataba wa IGA kuonekana batili.

Ndipo serikali yetu itaenda kwenye mabaraza ya nje kuwashtaki waarabu, lakini hapo sasa ndipo sheria za kimataifa kama Vienna Convention zitaanza kutumika, ambayo The Boy Wonder amesema haikutumika, ambapo mimi nikamwambia matumizi yake hayakuwa ya ndani.
 
Serikali ianaenda hatua ya HGA/CONCESSION na LEASE; XMASS tutakuwa na DP WORLD TANZANIA; 65% DP WORLD na 35% WATANZANIA. Mkuu jiandae kununua hisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…