denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Una matatizo kichwani.Terms mbona hazina shida
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Una matatizo kichwani.Terms mbona hazina shida
Unaposema huwezi kutumia sheria za ndani kuvunja mkataba wa kimataifa, kwa nini jaji ametoa hoja ya kufanya marekebisho kwenye vipengele vya ule mkataba, badala ya kuwapa ushindi wa moja kwa moja Jamhuri?
Mkuu mbona unakuwa mkali, nini shida? Mwenzako kasema wote sio Mwambukusi na wenzake tu, na amewagusa hata hao majaji na katoa sababu na kueleza mapungufu ya pande zote. Sasa wewe unakuja na mapovu- tulia leta hoja majadala uendeUnaandika vipi mawakili kuna hoja hawakuziwasilisha vizuri, wakati jaji kwenye hukumu yake amekiri kuna makosa kwenye vipengele vya ule mkataba na vinatakiwa kufanyiwa marekebisho?
Kama wasingewasilisha hoja zao vizuri, jaji angeweza kuwaelewa vipi mpaka akiri kuna makosa kwenye vipengele vya ule mkataba wa hovyo wa bandari?
Usidharau kazi waliyofanya kina Adv. Mwabukusi, watanganyika tumeiona kazi yao na kuielewa.
Mkuu kwa kesi yetu concession contract au investment contract hazijafikiwa bado- kwa hiyo reference ya Kenya naiona kama ni irrelevant
Asante.Mkuu Denoo J nimefurahi kukuona hapa, hebu turudi kwenye mada:
Mahakama kutoa ushauri siyo sawa na kutangaza kuwa mkataba ni batili. Mara nyingi mahakama hata kwenye kesi za kikatiba huwa haitangazi moja kwa moka kwamba sheria fulani ni batili kwasababu tu inakinzana na katiba ya nchi. Huwa inatangaza haki za wadai, inalishauri bunge juu ya hiyo sheria, inatoa mapendekezo na kuirudisha hiyo sheria irekebishwe na bunge.
Muda ukipita bila bunge kurebisha hiyo sheria basi inapigwa chini moja kwa moja. Lakini, fahamu kwamba mbali na nguvu ya mahakama kutoa haki, haiwezi kupoka madaraka ya mihimili mingine. Haya madaraka kisheria tunaita "Prerogatives". Hili liliwekwa wazi kwenye kesi za katiba za miaka ya 90's. Hebu tukazipitie, tutaona hili nalosema hapa. Huu ndiyo uelewa wangu wa kawaida wa sheria za katiba, kama nakosea naomba nirekebishwe.
Sasa mambo kama " War, Diplomacy, Treaties", yanaangukia kwenye nguvu za moja kwa moja za serikali (Prerogative of the Executive). Mikataba ya kimataifa huingiwa kwa kupitia sheria za kimataifa, hivyo hata kuuvunja inabidi utumie sheria za kimataifa, siyo vinginevyo. Hii ndiyo kanuni kuu ya sheria za kimataifa, kwenye suala la mikataba (Pacta-Sunt-Servanda). Bunge na serikali vitashauriwa na mahakama, ila mahakama haiwezi kamwe kuvunja mkataba.
Hili likiruhusiwa basi fahamu kwamba, dunia nzima itakuwa na matatizo kwasababu mataifa mengi yataenda mahakamani kujaribu kuvunja mikataba kiholelea wakitumia mwanya wa katiba. Marehemu Kanali Ghadafi aliingia kwenye mgogoro mkubwa miaka ya 1960's, 1970's na 1980's baada ya kuvunja mikataba ya uwekezaji ambayo iliachwa na Mfalme Idriss. Kesi zilikuwa ni nyingi mno hadi Libya akazidiwa. Ukienda mtandaoni utazikuta ziko nyingi tu, zisome.
Kule Urusi, wakomunisti baada ya kupindua nchi, waliamua kukataa mikataba ya kimataifa ya madeni. Walikataa kulipa na kusema ni mikataba wa kinyonyaji, wakomunisti na ujeuri wao waliifanya nchi yao, iingine kwenye Debt-Default jambo ambalo walilijutia sana. Hivyo basi inabidi tuzingatie haya yafuatayo:
1. Mikataba ya kimataifa huvunjwa kwa kutumia sheria za kimataifa.
2. Mikataba ya kimataifa inaweza kuvunjwa endapo bunge likaamua kuishurutisha serikali.
3. Mikataba ya kimataifa inabidi ijadiliwe sana na bunge kabla ya kupitishwa (Before Ratification)
NB: Kama ingekuwa ni rahisi hivi, basi Marehemu Magufuli angeivunja yote huko mahakamani.
Ninaona shida yako iko wapi- unajadiliana na watu ambao wanakwenda hatua kwa hatua katika safari ambayo wewe umeshapita mara nyingi. Ulishaangalia mararudio ya mechi na mtu ambaye ndiyo mara ya kwanza anaiingalia? Utakuwa unamwambia sasa hapo goli linaingia sasa, na hiyo siyo sawa.Uhalali wa Concession au International Commercial Contract hutoka kwenye Bilateral Investment Treaty au Multilateral Investment Treaty. Hapa kwetu hatuna BIT hivyo uhalali wa HGA/Project Agreement lazima utatokana na IGA. Kwenye sheria za uwekezaji, kinachofanya HGA/Concessions/Commercial Contract ziwe kitu kimoja na BIT/IGA/MIT ni vipengele viitwavyo, UMBRELLA CLAUSE na STABILIZATION CLAUSES.
Mkataba wa Vienna 1969, umeweka wazi kabisa kuhusu hili na ndiyo utaratibu ulivyo. Mkataba wowote ule wa kimataifa wa uwekezaji au jambo jingine, uwe ni BIT/IGA au Concession/Contract/HGAs ambazo ziko chini ya BIT/IGA/MITs vinaweza kuvunjwa chini ya sheria za kimataifa. Nashangaa ambavyo bado mnaendelea kukomaa tu.
Unaandika vipi mawakili kuna hoja hawakuziwasilisha vizuri, wakati jaji kwenye hukumu yake amekiri kuna makosa kwenye vipengele vya ule mkataba na vinatakiwa kufanyiwa marekebisho?
Kama wasingewasilisha hoja zao vizuri, jaji angeweza kuwaelewa vipi mpaka akiri kuna makosa kwenye vipengele vya ule mkataba wa hovyo wa bandari?
Usidharau kazi waliyofanya kina Adv. Mwabukusi, watanganyika tumeiona kazi yao na kuielewa.
Ninaona shida yako iko wapi- unajadiliana na watu ambao wanakwenda hatua kwa hatua katika safari ambayo wewe umeshapita mara nyingi. Ulishaangalia mararudio ya mechi na mtu ambaye ndiyo mara ya kwanza anaiingalia? Utakuwa unamwambia sasa hapo goli linaingia sasa, na hiyo siyo sawa.
Ukweli hatuna tayari HGA/ CONCESSION/LEASE CONTRACTS kwa hiyo hatuna mfanano wowote na Kenya
Asante.
Kwa maelezo uliyotoa, tayari yanaenda kinyume na kile jaji alichofanya, pamoja na kuliagiza bunge likafanye marekebisho, lakini jaji hakutoa haki kwa wadai, au utuambie hapa, ni ipi extent ya haki ya wadai, kuna ubaya kwangu kuita haki ya wadai ni sawa na wao kushinda kesi?
Namuomba Moderator aupandishe uzi huu na kuuweka kama quote kwenye first post.Hata hili nalo lina walakini mkubwa. Hata katiba ya nchi nayo ni sheria kama sheria nyingine, sema tu ni sheria mama (The Mother-Law). Kiutaratibu, mikataba ya kimataifa huwa haivunjwi kupitia mahakama za ndani, kama ingakuwa inafanyika hivyo basi, mikataba mingi sana ya kimataifa ingekuwa inavunjwa kwa hila au ujanja pale ambapo nchi inahisi kubanwa.Anyway,
Chini ya sheria za kimataifa za mikataba, kuna kanuni kongwe sana iitwayo "Pacta-Sunt-Servanda", ambayo hutaka nchi ziheshimu makubaliano iliyoyaingia bila ujanja-ujanja mwingine. Tukisema tunatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa basi tutakuwa tunaweka mwanya wa nchi kuvunja hii kanuni ya "Pacta-Sunt-Servanda"
Upande mwingine, Customary International Law, inasema dhahiri kwamba, suala zima la kusaini mikataba liko chini ya mamlaka ya serikali. AU, signing international treaties, falls within the prerogative of the executive. Hivyo bunge linapewa mamlaka ya kuridhia tu (Endorsing), kama mbinu ya ushirikishwaji wa wananchi, ila utiaji sahihi wa mikataba ni suala la serikali (The Executive). Ukishafahamu hili, utatambua kwamba mahakama haina uwezo wa kuvunja mikataba ya kimataifa kwasababu mamlaka yake ni ndani ya nchi tu.
Kesi za kikatiba za Rev. Christopher Mtikila, za miaka ya 90's ziliweka hizi kanuni wazi kabisa, kwamba kuna baadhi ya mambo siyo ya mahakama bali mihimili mingine. Hivyo mahakama inachoweza kufanya ni kutangaza haki na wajibu wa wahusika (Declaration of Rights) na kulishauri bunge lifanya mabadiliko muhimu. Hili niliongea majuzi na ndugu yangu Kalamu lakini nadhani hatukuelewana vizuri.
=============================================================
Sasa nirudi kwenye kesi na makosa niliyoyaona mwanzoni kabisa katika hoja tano ambazo mawakili wetu wasomi hawakuziangalia vizuri. Hata binafsi, nilishangaa kwanini mawakili wa serikali nao hawakuzizingatia vizuri hasahasa, Pre-Trail Conference (PTC):
Mosi, hoja ya kwamba Dubai siyo nchi hivyo haiwezi kusaini mikataba ya kimataifa. Wakili Mwabukusi alitumia mkataba wa kimataifa uitwao, The Monte-Video Convention, 1933 ambao unatoa vigezo vya sehemu kuitwa nchi. Hili ukiliangalia katika upande mmoja unaweza ukahisi ni sahihi, lakini katika mapana yake, lina walakini mkubwa.
Prof Hersch Lauterpatch aliandika mwaka 1958 kwenye chapisho la The International Law Commission (ILC), Commentary on International Treaties, kwamba "Treaties signed and entered by composition states/composite states, are treaties in the ordinary meaning of treaties entered by states"
Ukizingatia, State-Practice, hili linafanyika sana hapa duniani. Madola madogo (Composite States) ndani ya muungano au shirikisho huruhusiwa kusaini mikataba ya kimataifa chini ya udhamini wa dola kubwa. Mfano, Katiba ya Shirikisho la Ujerumani, chini ya Ibara ya 32 (3) inasema hivi "In so far as the Lander have power to legislate, they may, with the consent of the Federal Government, conclude treaties with foreign states"
Hichi kipengele ndicho kililipa ruhusa jimbo la Bavaria la Ujerumani Magharibi, kuingia makubaliano ya kimataifa mwaka 1960 na nchi kama Austria na Switzerland kwenye utunzaji wa ziwa Constance dhidi ya uchafuzi. Hivyo hili linawezekana vizuri tu. Lakini kubwa na muhimu ni kwamba siku hizi hatutumii, The Monte-Video Convention 1933, peke yake kupima uwezo wa eneo linalojitawala kuwa dola, bali tunatumia, The Badinter Principles ambazo ziliandialiwa na European Union kwenye kuzitambua nchi huru zilizojitoa kwenye shirikisho la Yugoslavia.
Pili, kutumia sheria ya mikataba "The Law of Contract Act" kupinga mkataba wa kimataifa. Haya ni makosa makubwa mno. Mikataba yote ya kimataifa hutafasiriwa na kusomwa chini ya The Vienna Convention on the Law of Treaties, 1969. Bahati mbaya kwenye ile kesi, hii sheria haikutumika, wala mawakili wa serikali hawakuitumia na sifahamu kama hata Jaji Ndunguru naye kaitumia. Kama hajautumia huu mkataba kwenye kuhukumu hii kesi, basi binafsi nasema, Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Bagosha (In Magu's Voice).
The Law of Contract Act, ingetumika endapo tu kama Tanzania/TPA ingekuwa imeshasaini HGA na DP-World. Maana, HGA ndiyo mkataba (A Contract/Concession/International Commercial Contract), bali IGA ni mkataba wa kimataifa (A Treaty). Japo, hata hapa kuna mianya mingi tu, ambayo mawakili wangeweza kupenya endapo wangepewa muda zaidi wa kujipanga.
Tatu, Jaji Ndunguru, Mawakili wa Serikali na Mawakili wetu kuna kitu muhimu kimewapita ambacho kama wangesoma vizuri, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, wangeweza kuutupilia mbali kabisa huu mkataba wa DP-World. Nchi jirani ya Kenya mwaka 2000-2001 waliweza kutupilia mbali kabisa mkataba wa kimataifa ambao ulizua taharuki kama hapa kwetu. Nadhani hili likifanyika na hapa kwetu, sijui serikali itaweka wapi uso wake.
Mambo ni mengi, na huyo wakili wako unayemsifia hapa naye kapuyanga vibaya. Wakina Mwabukusi walikuwa na baadhi ya hoja nzuri sana, sema tu hawakuziwakilisha vizuri mbele ya mahakama.
Hata kama angevunja kuna sunset clause ambayo italinda maslahi ya watu na naomba ieleweke kwamba sio kila mwekezaji ni tapeli na sio kila mzungu ni ni mwizi wa mali za Tanzania kwa hiyo sio kila ngozi nyeupe ni mzunguMkuu Denoo J nimefurahi kukuona hapa, hebu turudi kwenye mada:
Mahakama kutoa ushauri siyo sawa na kutangaza kuwa mkataba ni batili. Mara nyingi mahakama hata kwenye kesi za kikatiba huwa haitangazi moja kwa moka kwamba sheria fulani ni batili kwasababu tu inakinzana na katiba ya nchi. Huwa inatangaza haki za wadai, inalishauri bunge juu ya hiyo sheria, inatoa mapendekezo na kuirudisha hiyo sheria irekebishwe na bunge.
Muda ukipita bila bunge kurebisha hiyo sheria basi inapigwa chini moja kwa moja. Lakini, fahamu kwamba mbali na nguvu ya mahakama kutoa haki, haiwezi kupoka madaraka ya mihimili mingine. Haya madaraka kisheria tunaita "Prerogatives". Hili liliwekwa wazi kwenye kesi za katiba za miaka ya 90's. Hebu tukazipitie, tutaona hili nalosema hapa. Huu ndiyo uelewa wangu wa kawaida wa sheria za katiba, kama nakosea naomba nirekebishwe.
Sasa mambo kama " War, Diplomacy, Treaties", yanaangukia kwenye nguvu za moja kwa moja za serikali (Prerogative of the Executive). Mikataba ya kimataifa huingiwa kwa kupitia sheria za kimataifa, hivyo hata kuuvunja inabidi utumie sheria za kimataifa, siyo vinginevyo. Hii ndiyo kanuni kuu ya sheria za kimataifa, kwenye suala la mikataba (Pacta-Sunt-Servanda). Bunge na serikali vitashauriwa na mahakama, ila mahakama haiwezi kamwe kuvunja mkataba.
Hili likiruhusiwa basi fahamu kwamba, dunia nzima itakuwa na matatizo kwasababu mataifa mengi yataenda mahakamani kujaribu kuvunja mikataba kiholelea wakitumia mwanya wa katiba. Marehemu Kanali Ghadafi aliingia kwenye mgogoro mkubwa miaka ya 1960's, 1970's na 1980's baada ya kuvunja mikataba ya uwekezaji ambayo iliachwa na Mfalme Idriss. Kesi zilikuwa ni nyingi mno hadi Libya akazidiwa. Ukienda mtandaoni utazikuta ziko nyingi tu, zisome.
Kule Urusi, wakomunisti baada ya kupindua nchi, waliamua kukataa mikataba ya kimataifa ya madeni. Walikataa kulipa na kusema ni mikataba wa kinyonyaji, wakomunisti na ujeuri wao waliifanya nchi yao, iingine kwenye Debt-Default jambo ambalo walilijutia sana. Hivyo basi inabidi tuzingatie haya yafuatayo:
1. Mikataba ya kimataifa huvunjwa kwa kutumia sheria za kimataifa.
2. Mikataba ya kimataifa inaweza kuvunjwa endapo bunge likaamua kuishurutisha serikali.
3. Mikataba ya kimataifa inabidi ijadiliwe sana na bunge kabla ya kupitishwa (Before Ratification)
NB: Kama ingekuwa ni rahisi hivi, basi Marehemu Magufuli angeivunja yote huko mahakamani.
Ok, hebu twende sawa..Mkuu, Denoo J, you're bigger than this,
Hakuna anayedharau hoja za Advocate Mwabukusi, mimi mwenyewe nimewaunga mkono na nitaendelea kuwaunga mkono. Ila tunapotofautiana mimi ni ninyi ni kwamba, mimi ni Mwanasheria hivyo nachangia kama Mwanasheria. Hayo ya siasa na mengineyo siyo yangu.
Kesi ilikuwa na hoja tano, baadhi ya zile hoja kama CAPACITY OF PARTIES na STATUS OF IGA hazikuwa na usahihi wowote ule kwenye sheria za kimataifa. Hata hivyo kuna baadhi ya sheria kama mkataba wa Vienna 1969, ambao ndiyo sheria ya msingi kabisa kwenye kutafasiri mikataba hawakuitumia, wenyewe wametumia The Law of Contract Act, The Constitution etc.
Wangeutumia ule mkataba wangepata uwanja mpana maana hata ule mkataba nao ni sehemu ya sheria za nchi yetu ambazo bunge ziliipitisha (Domesticated) kipindi cha Mze Nyerere. Kutokuutumia kumechangia kwa sehemu kubwa baadhi ya hoja zao kuwa dhaifu. Huu ndiyo ukweli wenyewe. Jambo jema kabisa kutegemea sheria za rasilimali (Natural Wealth Protection Laws) na sheria za manunuzi (Procurement Laws), lakini kwasababu huu ni mkataba wa kimataifa ni lazima ungetumia mkataba wa Vienna ambao ni sehemu ya sheria za Tanzania.
Mimi nafikiri tumeshatumia lugha laini sana Tanzania kilibaki ni kukatipia ili watu waamke kutoka kwenye usingizini wa upumbavuNi stahiki yako ila wakati mwingine tumia lugha laini ila ujumbe wako ufike
Tazama hiyo moja hapo juu please.Mkuu Denoo J, uwe na siku njema,
Mimi hapa nimeshamaliza lililonileta sasa naenda kutekeleza majukumu mengine.
Hauko sawa, yaani wakristo wanasema hawawezi kuvunja ndoa kwa sababu imefungwa kiislam halafu wewe best man unapeleka hiyo kesi vatican ili iweje?Ok, hebu twende sawa..
Hapa kuna point ya wazi kabisa ambayo nakuona una miss, unashindwa kutofautisha ni wakati gani zitumike sheria za kimataifa, na wakati gani zitumike sheria za ndani.
Mfano tukiangalia shauri lililotolewa hukumu leo mahakamani, wale wapeleka maombi walikuwa wanalalamika juu ya sheria za ndani zilizovunjwa wakati wa kuingia ule mkataba wa IGA, na kwa mantiki hii, kwangu kwao kuonesha hizo sheria kwa kutumia Katiba yetu, Law of Contract Act na nyinginezo ni sahihi kabisa, kwamba ndio zimevunjwa.
Hawakutakiwa kutumia sheria za nje wakati wale walikuwa wanailalamikia serikali yetu, ambapo kama wangeshinda ile kesi, na mahakama kutoa order ile IGA ni batili...
Sasa hapo serikali yetu ndio ingetakiwa kwenda kwenye hayo mabaraza ya nje ya usuluhishi, ambapo huko, hizo sheria za kimataifa kama Vienna Conventions na nyinginezo ndio hutumika, pale ambapo serikali yetu inakuwa ikitaka kuvunja ule mkataba wa hovyo dhidi ya waarabu wa Emirati..
Naamini unaielewa pointi yangu, ndio maana nikaona kama una under-estimate kwa namna fulani kazi nzuri iliyofanywa na wakina Adv. Mwabukusi na wenzake, kazi amabayo imesababisha jopo la majaji kutoa maelekezo kwa bunge nini wakafanye.
Kwangu ni hayo tu.
Mantiki ya kile nilichoandika ni hiki..Hauko sawa, yaani wakristo wanasema hawawezi kuvunja ndoa kwa sababu imefungwa kiislam halafu wewe best man unapeleka hiyo kesi vatican ili iweje?
Serikali ianaenda hatua ya HGA/CONCESSION na LEASE; XMASS tutakuwa na DP WORLD TANZANIA; 65% DP WORLD na 35% WATANZANIA. Mkuu jiandae kununua hisaMantiki ya kile nilichoandika ni hiki..
Mkataba wa IGA una matatizo, unakiuka sheria zetu za ndani, ndipo wapeleka maombi kina Adv. Mwabukusi na wenzake wakaenda mahakamani kuiomba mahakama iseme ule mkataba wa IGA ni batili, kwa kuonesha baadhi ya sheria zetu za ndani zilizokiukwa, kama Contract Act, na nyingine..
Baada ya hapo haki ya wapeleka maombi ikipatikana, ndio waende mbele, ambapo sasa itakuwa ni baada ya mkataba wa IGA kuonekana batili.
Ndipo serikali yetu itaenda kwenye mabaraza ya nje kuwashtaki waarabu, lakini hapo sasa ndipo sheria za kimataifa kama Vienna Convention zitaanza kutumika, ambayo The Boy Wonder amesema haikutumika, ambapo mimi nikamwambia matumizi yake hayakuwa ya ndani.