Wakili wa Clinton Nyundo na wenzake hajaridhishwa na hukumu

Wakili wa Clinton Nyundo na wenzake hajaridhishwa na hukumu

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Godfrey Wasonga ambaye ni miongoni mwa Mawakili waliokuwa wakiwatetea kina Nyundo na wenzake ambao wamehukumiwa kifungo cha maisha Gerezani kutokana na kesi ya kumbaka na kumlawiti Binti wa Yombo, amesema wao kama Mawakili siku zote huwa wanaheshimu maamuzi ya Mahakama lakini hawajaridhika na hukumu iliyotolewa.

Akiongea na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama Jijini Dodoma amesema kuna mambo mbalimbali na kwamba hawakuona kama Washtakiwa hao walikuwa na kesi ya kujibu “tuliona hakuna kesi ya kujibu, huwezi kuja kuleta video za mtandao.................. kwa mfano kosa la pili hata anayeingiliwa naye alitakiwa ashtakiwe, kwanini aliruhusu wakati anasema yeye alienda kule aka-enjoy akafurahi, ilitakiwa na yeye ashtakiwe?”

PIA SOMA
- Nyundo na wenzake wakutwa na hatia, wahukumiwa kifungo cha Maisha Jela

- Kina Nyundo wakutwa na Kesi ya Kujibu (Sakata la Binti wa Yombo)
 
Kuna uzi nimetoka kusema ile kesi hukumu watatoka hata kama High Court itagoma ila CAT lazima watatoboa tu maana CAT haitakubali kutengeneza precedence ya hovyo itakayoonea wengine.

Watu wanaweza wakashangilia.haya maamuzi lakini watu hawa hawa wanapaswa kufahamu kuwa endapo High Court itabariki maamuzi haya basi hata wao wanaweza wakashtakiwa kwa video au picha zaku download na wakakutwa na hatia bila kujali uhalali wa video na picha hizo.

Watu wanabidi wajifunze sana mifumo yetu ya sheria, haya sio yakuchekelea hata kidogo.
 
Unataka kumaanisha nini? Wameonewa?
Sheria ifuatwe sio mihemko ya umma. Unawezaje kumfunga mtu kwa video ya kudownload na bado kusiwe na kosa la kusambaza picha chafu au hata mtu aliyeshitakiwa kwa kusambaza hizo video. Hujiulizi umma ulizipataje hizo video? Si ni kosa sasa mbona hakuna watuhumiwa?

Ina maana kifaa kilichotumika hakipo. Hapo ndio mzozo ulipo zaidi
 
Kuna uzi nimetoka kusema ile kesi hukumu watatoka hata kama High Court itagoma ila CAT lazima watatoboa tu maana CAT haitakubali kutengeneza precedence ya hovyo itakayoonea wengine...
Bush lawyer at work. Yaani kwamba kwakuwa binti alikuwa kwenye vitisho vya watu kadhaa akiwemo afande ulitegemea alivyoulizwa kwa vitisho kama ame enjoy aseme haja enjoy nini kingefuata?

Huyu wakili kweli kilaz,a anaaibisha mawakili wenye weledi maana huwezi kusema eti kwanini na yeye binti hakushtakiwa.

Yaani aliyetendewa uhalifu awe mshtakiwa? Angefanya kwa hiari yake hapo kweli na yeye angejumuishwa kwenye mashtaka.

Lakini binti alibakwa na wahuni sita huku wakimtisha kumfanyia mabaya zaidi endapo hatokiri na kumuomba msamaha afande.

Nakuhakikishia hata rufaa iende Court of Appeal bado hukumu itakuwa upheld kama first court of instance ilivyoamua.
 
Acha wewe si walikuwa wanajirekodi wenyewe huku wakila tunda kimasihara!?
Je, wameshitakiwa kwa kosa la kusambaza picha chafu mtandaoni?, jelilisahaulika ilo kosa au liliachwa makusudi sababu hakuna ushahidi wa wao kusambaza? Na ushahidi huo ungekuwa ni nini? Je unaweza kuhalalisha video kuwa ni halisi?
 
Sheria ifuatwe sio mihemko ya umma. Unawezaje kumfunga mtu kwa video ya kudownload na bado kusiwe na kosa la kusambaza picha chafu au hata mtu aliyeshitakiwa kwa kusambaza hizo video. Hujiulizi umma ulizipataje hizo video? Si ni kosa sasa mbona hakuna watuhumiwa?

Ina maana kifaa kilichotumika hakipo. Hapo ndio mzozo ulipo zaidi
Mahakama haifanyii kazi kosa ambalo halijapelekwa mahakamani. Mahakama inatoa nafuu ama hukumu kulingana na case at hand na sio kutolea uamuzi jambo ambalo halipo kwenye hati ya mashitaka.

Sio kazi ya mahakama kutengeneza kesi mpya bali kazi ya mahakama ni kupima na kufikia uamuzi jambo lililowasilishwa mbele yake.
 
Wakakate rufaa ni haki yao kwani tatizo nini? Ni haki kushtakiwa na ni haki yao kukata rufaa, Ila wajue tu wametenda jinai na tuko nao sambamba hadi kieleweke.

Kama tu wanadhani kukata rufaa= kushinda kesi.
 
Je, wameshitakiwa kwa kosa la kusambaza picha chafu mtandaoni?, jelilisahaulika ilo kosa au liliachwa makusudi sababu hakuna ushahidi wa wao kusambaza? Na ushahidi huo ungekuwa ni nini? Je unaweza kuhalalisha video kuwa ni halisi?
Ungeenda mahakamani,umshauri wakili wao,Bado hujachelewa nenda na dondoo hizo zitumike kwenye rufaa!Huenda ukawakoa Wala tunda kimasihara.
 
Back
Top Bottom