Jerlamarel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2021
- 843
- 2,525
Wakati nchi nyingi makampuni ya mawasiliano yakiwa yanaweka kipaumbele sana kwenye usiri wa taarifa za wateja wao, hapa kwetu hali ni tofauti kabisa.
Hilo limethibitishwa leo na Wakili Msomi Fred Kapara, ambaye ni Wakili wa Kampuni ya Tigo, alipoulizwa Mahakamani wakati akitoa ushahidi katika kesi inayomuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA na wenzake wanne, kwamba kati ya Utii kwa mamlaka na Usiri wa taarifa za wateja kipaumbele kwao ni nini, bila kupepesa macho akajibu Utii (Compliance) kwao ndiyo kipaumbele (Priority) zaidi.
Sasa majibu ya kwanini kumekuwepo na uzimaji wa baadhi ya mitandao ya kijamii na kupanda mara dufu kwa gharama za bando za data yameshapatikana. Sababu kubwa ni kwamba huko kwenye hizo social networks zingine kwao Privacy za Wateja ndiyo Priority hivyo mamlaka zitashindwa kupata kile wanakitaka kwa urahisi.
Hii kesi mpaka waje wamalizike mashahidi wote 24 tutakuwa tumeshapata siri nyingi sana ambazo raia wa kawaida tulikuwa tunafichwa.
Ushahidi wote, soma Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Mbowe na Wenzake: Shahidi Afred Kapala wa tiGO atoa Ushahidi, Kesi kuendelea, Nov 03, 2021