Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Jerlamarel

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
843
Reaction score
2,525
Wakati nchi nyingi makampuni ya mawasiliano yakiwa yanaweka kipaumbele sana kwenye usiri wa taarifa za wateja wao, hapa kwetu hali ni tofauti kabisa.

Hilo limethibitishwa leo na Wakili Msomi Fred Kapara, ambaye ni Wakili wa Kampuni ya Tigo, alipoulizwa Mahakamani wakati akitoa ushahidi katika kesi inayomuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA na wenzake wanne, kwamba kati ya Utii kwa mamlaka na Usiri wa taarifa za wateja kipaumbele kwao ni nini, bila kupepesa macho akajibu Utii (Compliance) kwao ndiyo kipaumbele (Priority) zaidi.

Sasa majibu ya kwanini kumekuwepo na uzimaji wa baadhi ya mitandao ya kijamii na kupanda mara dufu kwa gharama za bando za data yameshapatikana. Sababu kubwa ni kwamba huko kwenye hizo social networks zingine kwao Privacy za Wateja ndiyo Priority hivyo mamlaka zitashindwa kupata kile wanakitaka kwa urahisi.

Hii kesi mpaka waje wamalizike mashahidi wote 24 tutakuwa tumeshapata siri nyingi sana ambazo raia wa kawaida tulikuwa tunafichwa.

31B0E624-3D80-4C2F-B612-5CBA00EEE0FB.jpeg


Ushahidi wote, soma Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Mbowe na Wenzake: Shahidi Afred Kapala wa tiGO atoa Ushahidi, Kesi kuendelea, Nov 03, 2021
 
Wakati nchi nyingi makampuni ya mawasiliano yakiwa yanaweka kipaumbele sana kwenye usiri wa taarifa za wateja wao, hapa kwetu hali ni tofauti kabisa.
Unapo anzisha kampuni unapewa vigezo na masharti na regulatory body husika namna ya kuendeha shughuri zako.

Sasa kama kutoa ushahidi/kielelezo kwa jamhuri juu ya no. fulani ya simu n moja ya requirement na ulishakubali unapoanzisha kampuni unazani tigo wafanye nn?

Tatizo sio tigo tatizo n mamlaka zetu ndo za hovyo.

Na watu mnachanganya sna kati ya hizi social networks na Makampuni ya simu. Kungekua na usiri kama mnavodhania watu wasingekua wana lazimika kusajiri laini kila kukicha
 
... Halafu ni barua kutoka polisi isiyoeleza sababu ya kuhitaji taarifa za mteja; akaandaa taarifa yeye, akasaini yeye, akawasilisha yeye, anatoa ushahidi yeye! No separation of duties!

Wataalamu tusadieni kuchambua ushahidi wa leo wa mwanasheria wa tiGO; umebadili mwelekeo wa kesi? Mbowe na washtakiwa wenzie bado wako salama au unawaweka kwenye hali ngumu?
 
Kwa maana hiyo chadema walitaka hata mtu mwovu akitumia mtandao ALINDWE TU NA UOVU kwa kuwa sheria ya usiri na faragha inamlinda.
#Hata ulaya hakuna kitu ya namna hii.
Yani inamaana pamoja na kujinasibu kama watu wanaozijua Sheria, hawakuwa wanajua kama mamalaka zimepewa uwezo huo pale inapolazimu? Na kwa hii kesi ilikuwa ni lazima kuexpose ushahisi wowote unaoweza kurahisha kesi, maana kama ushahidi mzuri wa kuthibitisha makosa ulikuwa unapatikana huko, huwezi kuuacha kwa kigezo cha privacy.

Ningeona wamefaya makosa kama wangefatilia taarifa za siri ambazo hazihusiani kabisa na makosa anayokabiliwa nayo mtuhumiwa, kosa ni kosa tu liwe ni la kifichoni au la wazi.

Nadhani ni kwakua inang'ata kwao ndomaana hawakutaka taarifa za uovu wa jamaa yao zivujishwe.Angekuwa ni Sabaya hapo, ungeona hoja tofauti kabisa kwenye mitandao.
 
Back
Top Bottom