Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Mnatabia ya kuchambua kamstri kamoja na kukasimamia ili kutafuta uchochoro wa kutokea, bila kusimamia hoja yote niliyoandika.

Kwahiyo hapo umeona wapi nimeandika kutuma 500K ni kosa???

Kutuma 500K sio kosa,swala ni unatuma laki tano ili kifanikisha shughuli gani?? Kama kwenye kesi imesemekana kuwa kuna kiasi kilichotumwa kwaajili ya kitu fulani, kuna ubaya gani mahakama ikithibitusha ili kujua kama ni kweli Mbowe anasingiziwa?
Na wewe jiongeze kidogo! Hivi unapotuma muamala wa fedha Kuna kipengele chochote kinachoonyesha matumizi ya fedha uliyotuma? Kwanini huyo mwanasheria wa tigo aspeculate kuwa muamala huo ulitumwa Kwa kazi fulani ilihali hata barua anayodai ilimtoka polisi haikuainisha sababu Wala kosa lililodhamiriwa na muamala huo? Mwanasheria kilaza TU asiyeweza kureason Bali kuconlude na kujudge! Hastahili hiyo nafasi kwani kaichafua Sana kampuni ya tigo! Afukuzwe kazi mara moja!
 
Mambe alisema huko duniani wakijua Tz taarifa zinapatikana kirahisi namna hii Ni biashara kubwa sana duniani.huo mwanya Ni hatari kwa maaofisa wa serikali kukutumia na kuuza Taarifa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
NGOJA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWAAAA..WATANZANIA ELEWENI TENA NGOJA NIWASHIKE MASIKIO MSIKIE..kwenye haya makampuni ya simu vile vitengo vya makampuni ya simu vinavyohusiania na upatikanani wa taarifa za wateja Kama maongezi ya simu na text .WATU WA KITENGO NYETI WAMO NA KILA SIKU WANAFUATILIA MAONGEZI MBALI MBALI WANAYOAGIZWA.Ni mitandao yote.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna kampuni yoyote duniani yenye wakili. Hakuna. Kampuni inakuwa na mwanasheria; whether huyo mwanasheria ni wakili au solicitor lakini bado ataitwa mwanasheria wa kampuni au taasisi lakini si wakili wa Kampuni. Tigo inekuwaje kuwa na wakili na si mwanasheria?
 
Kinachofanyika Tigo ndicho kinaweza kuwa kinafanyika katika makampuni mengine yote ya simu.
Huyo jamaa naona kaamua kuihujumu tigo maana wateja kina sisi ndiyo tusha hama
 
Je Unaifahamu kampuni ya Apple?

Kwao mteja kwanza, na si vinginevyo.
Unazijua sheria za US ambako ndio Apple imesajiliwa? Kwao kulinda haki na siri za mteja ni takwa la kikatiba wala sio maamuzi ya kampuni. Sisi Tanzania ambako ndio Tigo Tz wamesajiliwa ni takwa la kikatiba kampuni kutoa siri za mtuhumiwa. Sasa unalinganishaje vitu hivi

Apple inaweza kupigwa faini kwa kuvujisha taarifa, Tigo inaweza kupigwa faini au kufungiwa kwa kutoipatia serikali taarifa.

Upuuzi wa sheria na serikali yetu tusiulimbikize zikawa shida za makampuni wanaokuja kuwekeza. Hawa wawekezaji sio wapumbavu wana uwezo mkubwa na ndio maana TTCL inakula matope huku wao wakipiga faida
 
Kama walaji wakiamua kuisusa basi watalia njaa kama uhuru na mzalendo
 
Hebu tujiulize kidogo halafu tuendelee kubishana mpaka kesho....

Zipi ni requirements za serikali haya makampuni yanapoomba leseni kwa serikali..?
Tunaponunua laini kuna fomu ya makubaliano kati yetu na tigo kwa tigo kulinda haki zetu tunajaza na kusign?

JF tukijiunga huwa kuna requirement za JF tunapewa then tuna click agree ~ TUNAZISOMA HIZI REQUIREMENTS.. au tuna agree tu..
Ulizisoma?
 
Mpaka anayetaka siri hizo awe na court order ya kuitaka kampuni husika kutoa siri hizo siyo kienyeji tu. Na kampuni husika inaweza kwenda mahakamani kuipinga court order kuhusu kutoa siri za mteja wao.
Sheria za US zinaruhusu kampuni za simu kutoa siri za wateja, au ndo ushalishwa matango pori lumumba
 
Na wewe jiongeze kidogo! Hivi unapotuma muamala wa fedha Kuna kipengele chochote kinachoonyesha matumizi ya fedha uliyotuma? Kwanini huyo mwanasheria wa tigo aspeculate kuwa muamala huo ulitumwa Kwa kazi fulani ilihali hata barua anayodai ilimtoka polisi haikuainisha sababu Wala kosa lililodhamiriwa na muamala huo? Mwanasheria kilaza TU asiyeweza kureason Bali kuconlude na kujudge! Hastahili hiyo nafasi kwani kaichafua Sana kampuni ya tigo! Afukuzwe kazi mara moja!
Hii kweli ni home of great thinkers😂.

Ikiwa kwenye kesi imethibitika kuwa tarehe fulani kiasi fulani cha fedha kilitumwa (shahid kasema), na hakuna traces zozote kwenye simu ya mtuhumiwa inayoonyesha kuwa alituma hiyo pesa (pengine labda aliifuta), utaupata wapi ushaidi wa kuthibitisha huo muamala kama sio kwenda Tigo kwenywe?

Tigo wapo hapo kufatilia na kuthibitisha kama ni kweli kuna miamala ilifanyika na sio kushuhudia matumizi ya hizo pesa.

Matumizi ya hizo pesa hayaihusu Tigo hata kidogo, matumizi ya hizo pesa yanaihusu Mahakama ambayo inataka kuthibitisha.

Tigo hawana makosa, ilaumuni myanya ya kisheria(katiba) inayoipa mahakama mamlaka ya kupata privacy ya mtu.
 
Nashukuru tigo kwaherini line yenu mwisho Leo kumbe mnajali utii kwa wasiowapa hela sisi tunaowapa hela ni nafasi ya pili.
Hata mimi ndiyo nipo hapa nasajiri line kwa mtandao tofauti
 
Back
Top Bottom