Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Hata baki salama wanaenda kumuondoa mana alicho kiongea leo, ni hatari sana, kwanza aliulizwa amtaje aliye sajili line ya tigo akasema hamji, haya line ilisajiliwa wapi anasema hajui anachotaka kusma ni kwamba tigo haina data za kutosha kuhusu wateja wake na haituni privacy ya wateja wake.
Sioni kama wanamuacha
 
Kwamba police akienda tigo tu kama unatumia huo mtandao anapewa habari zako zote kuanzia miamala yako simu zako na sms zako. Aibu yao
 
Kill nchi inamipango yake kisheria, North Korea sio Iran na Iran sio Tanzanian. Tuheshimu mamlaka iliopo kwa sheria ilio jipangia. Wewe Kama huli nyama ya nguruwe wenzio wanakula hivyo hivyo nyoka na samaki.
 
Kila nchi inamipango yake kisheria, North Korea sio Iran na Iran sio Tanzanian. Tuheshimu mamlaka iliopo kwa sheria ilio jipangia. Wewe Kama huli nyama ya nguruwe wenzio wanakula hivyo hivyo nyoka na samaki.
 
Ukweli lazima useme.Jamaa kazingua kinoma.

Angeweza kujibu maswali vizuri tu Kwa diplomatically kuliko vile Alivyofanya.
Alikuwa Open Sana.

Kiukweli ningekuwa Boss wake Kesho asubuh angeikuta barua mezani.

Tigo wametumia miaka kujibrand, Kwa Wenzetu brand ni kitu cha thaman mno haijalishi upo mahakamani au vipi. Bado Kuna namna ilipaswa ayajibu maswali Kwa namna sahihi Yaani jamaa kazingua Sana.

Mimi ni Mteja wa kudumu wa tigo Ila Kwa ushahidi wa Leo nimefahamu Mambo mengi Hadi nimeogopa. Privacy ya Mteja ni rahisi kuombwa na mtu mwingine pasipo Mteja kujulishwa.
 
Kampein ni kuitupa au kuachana na huduma za tigo zote kwetu sie tunao amini la ku bumba,we kama ni kijani pita hivi
 
Fikiria tu, kampuni inatumia mabilioni ye fedha kila mwaka ili itengeneze brand yake kwa wananchi. Lengo ikiwa ni wananchi waiamini na waipende ili waendelee kutumia huduma zake ili kampuni iendelee nayo kutengeneza pesa na faida.

Ghafla, anatokea mtu tu ndani ya kampuni, kwa kushindwa kwake kuelewa the value of brand, anajikuta anatia doa na kuharibu kabisa image ya kampuni, ki urahisi rahisi tu ndani ya masaa machache.. just like that!!

Anashindwa tu kutumia akili yake kujibu maswali diplomatically ili kulinda image na brand ya kampuni, kitu ambacho kingewezekana kabisa kufanyika.

Mtu huyu huyu anaamka kesho anaenda kazini kula kiyoyozi kwa mwajiri aliyemchafua??

Technically, ame destroy billions of value just kwa maneno yake. Watu wa branding mtanielewa. Haileti picha nzuri.

Napenda sana binadamu wenzangu, najua ana familia.. ila mi sio muumini wa "uzembe"..

Sitashangazwa mtu kama huyu asipokuwepo kazini tena.

Corporate world nnayoifahamu mimi, haitamuacha huyu mtu.

Akatafute tu ugali pengine.

Over
Kampuni zote za mawasiliano,serekali inapoomba details au vyombo chochote cha kiuchunguzi katika kupata muhtaasari fulani wa Jambo fulani kampuni za mawasiliano haziwezi kukataa kuitoa faragha husika kwa tarehe husika
 
Kwa bahati mbaya sidhani kama Tigo ni ya viwango hivyo. Kwa Tanzania labda Vodacom tu ndio ningetegemea ijihold kwenye standards ambazo brand yao inaendana na kulinda faragha za mteja. Na hiyo ni kwa sababu ya kuwa chini ya Vodafone group ambayo kwa kiasi kikubwa inafanya biashara kwenye masoko yenye uelewa ulaya. Tigo ilikotoka na inakouzwa kote ni mazingira ya biashara yale yale. Mkurugenzi wao kashikiliwa passport toka awamu ya tano anapambana kimya kimya
 
Ndo maana nimetumia neno ' Diplomatically' sote tunajua serikali ina mkono mrefu .. ila nnachosema mimi ni kwamba jamaa angechunga ulimi wake kwenye kujibu maswali... sasa angalia alichofanya
 
Kwa bahati mbaya sidhani kama Tigo ni ya viwango hivyo. Kwa Tanzania labda Vodacom tu ndio ningetegemea ijihold kwenye standards ambazo brand yao inaendana na kulinda faragha za mteja. Na hiyo ni kwa sababu ya kuwa chini ya Vodafone group ambayo kwa kiasi kikubwa inafanya biashara kwenye masoko yenye uelewa ulaya. Tigo ilikotoka na inakouzwa kote ni mazingira ya biashara yale yale. Mkurugenzi wao kashikiliwa passport toka awamu ya tano anapambana kimya kimya
But still bado ni brand kubwa.. maana ndo namba mbili baada ya Vodacom kwenye market share..meaning bado ana ushawishi na brand yake ni kubwa
 
Hadi sasa hivi TiGO hawajatoa kauli yoyote kwa umma kuepusha kuendelea kuharibiwa kwa taswira yao kwa wateja?
 
Alivyokuwa akijibu kwa kiburi, naamini ana baraka zote katika sehemu zote alikopita, akiondolewa atakuwa ameondolewa tu na atarudi kazini kwake kwa zamani na probably ni mjengoni maana ndio warudishwapo waovu wote walioharibu sehemu zinazoonekana, wanarudishwa kufichwa huko.
 
Ngoja tuone hiyo kesho.. ila daah jamaa ni bonge la mjinga..
 
Kafanya nini huyu
Jamaa kaharibu leo mahakamani kwenye kesi ya Mbowe, katapika mashudu ya ajabu yenye kuondoa uaminifu wa mtandao Tigo kwa wateja wake.

Kwa kifupi sana, kasema hivi Tigo huwa hailindi siri (Privacy) za wateja wake, wakati wowote Tigo bila sababu yoyote ya msingi inaweza kuchukua siri za wateja wake na kumpatia (share) mtu/taasisi nyingine (hususani serikali) ili wazitumie kwa maslahi yao pasipo hata mteja wa Tigo kujulishwa.
 
Back
Top Bottom