Fikiria tu, kampuni inatumia mabilioni ye fedha kila mwaka ili itengeneze brand yake kwa wananchi. Lengo ikiwa ni wananchi waiamini na waipende ili waendelee kutumia huduma zake ili kampuni iendelee nayo kutengeneza pesa na faida.
Ghafla, anatokea mtu tu ndani ya kampuni, kwa kushindwa kwake kuelewa the value of brand, anajikuta anatia doa na kuharibu kabisa image ya kampuni, ki urahisi rahisi tu ndani ya masaa machache.. just like that!!
Anashindwa tu kutumia akili yake kujibu maswali diplomatically ili kulinda image na brand ya kampuni, kitu ambacho kingewezekana kabisa kufanyika.
Mtu huyu huyu anaamka kesho anaenda kazini kula kiyoyozi kwa mwajiri aliyemchafua??
Technically, ame destroy billions of value just kwa maneno yake. Watu wa branding mtanielewa. Haileti picha nzuri.
Napenda sana binadamu wenzangu, najua ana familia.. ila mi sio muumini wa "uzembe"..
Sitashangazwa mtu kama huyu asipokuwepo kazini tena.
Corporate world nnayoifahamu mimi, haitamuacha huyu mtu.
Akatafute tu ugali pengine.
Over