Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

Wakili wa Tigo adai kwao Compliance (Utii) kwa mamlaka ni kipaumbele kuliko Privacy (faragha) za Wateja

But still bado ni brand kubwa.. maana ndo namba mbili baada ya Vodacom kwenye market share..meaning bado ana ushawishi na brand yake ni kubwa
Wateja wa aina gani ndio issue. Sijui kiasi gani hali imebadilika lakini Kwa muda mrefu tigo imekuwa ikiitwa mtandao wa wanafunzi, kwa ujumla cheap and cheerful. Na ndio soko letu lilivyo kwa kiasi kulani hawatofautiani sana. Sio soko linaloelewa na kuthamini data protection kivile.
 
Kwa maana hiyo chadema walitaka hata mtu mwovu akitumia mtandao ALINDWE TU NA UOVU kwa kuwa sheria ya usiri na faragha inamlinda.
#Hata ulaya hakuna kitu ya namna hii.
Hapa wazazi walipoteza rasilimali zao
 
Kapata baraka za mwajiri. Hivi ile ishu ya kususia mtandao wa voda iliishia wapi wanachadema? Maana naona hadi kwenye michango ya chama huwa mnatumia MPESA.
Nani kakudanganya.Tena kwa kiwango gani.Yaani mjinga mmoja anawapoteza wateja maelfu kwa kuwa nyie tigo ni wavujaji wa siri za mteja na kampuni.Wapi security ya mteja.Tigo bye bye.
 
Kuna mtu kaandika humu wanavyotudharau wateja. Sitashangaa wakikaa kimya.

Walitakiwa watoe kauli hata kama ni ya kujikosha ilakukaa kimya ukichanganya na hili tukio itazidi kupoteza mvuto kwa wateja.
 
Hahahahahahaaa!! Kwani ni mara ya kwanza yy kufanya ivyo hii itakua mara ya pili ya kwanza kabisa ni NONDO mambo ya mtandao wa tigo kua jamaa kajiteka.
Na mpk leo alikuwepo kazini na atakuwepo kazi mpk atakapo staff kwa umri tu.
 
Amewatia aibu sana wanasheria, sikutegemea kama mwanasheria anaweza kuwa haelewi umuhimu wa privancy ya mteja
Hawa ni wale wanaingiaga kazini kwa mgongo wa wakubwa sasa sema tu hii kesi imemkuta kwenye nafasi mbaya na imempwaya tayari.
 
Kuna mambo tokea mwaka 2013 hii kampuni ilikuwa ikitumika ovyo sana.

Iligeuzwa na idara fulani sitapenda kuitaja kulinda heshima yao.

Ila mpaka leo inatumia kama utajichanganya ukitumia mtandao huu wa tigo.

Uvujishwaji siri za wateja hupo sana kupitia mtandao huu.

Tena kama mpaka idara fulani kila mtu kuwa na mtu ndani ya mtu kwenye kampuni hiyo kumpa taarifa.

Tabia hii leo imekuja kuthibitika kwa kesi kubwa ambayo shaidi kama wakili wa mtandao huu na kufanya mengine ambayo mwenyewe sio upande wake kabisa.

Kwanini naeleza tatizo hili.

Kampuni hii kiufupi uongozi wa kusimamia mienendo ya mifumo imekuwa na dosari sana.

Kkama

Laini ya simu kusajiliwa mara mbili au kuuzwa bila idhini yako au kutumiwa kwenye mambo mengine.

Uvujaji wa siri za wateja bila kufuata mamlaka husika.

Tracking za simu zisizofuatwa kisheria .na juwa wale waanga wa kununua simu mitandaoni kisha ukaambiwa simu ya wizi.
 
Wateja watigo naona mmepigwa na kitu kizito kisogoni mwenu tena cha ncha Kali..😂
 
Kwa majibu yale yule sio mwajiriwa wa Tigo yule ni mtu wa kitengo kaenda tu pale kwa kivuli cha Tigo huwezi kuwa mwanasheria wa kampuni kisha ujibu kivile.Na kama ni mwajiriwa kweli ni waajiriwa kwa ajili ya kazi maalum
 
Wewe unaongea tu.
unamjua mtu anayeitwa "JAMHURI"
tusiwape tu lawama.
kuna rafiki yangu alikuwa Shahid kwenye kesi ya bangi.
Aliletewa samansi na mbavu mojaaa.
akataka kugoma kwenda nikamwambia watakuja kukuweka ndani.kaongee ulichokiona usiongeze neno Wala kupunguza neno.
Toa ushahidi kulingana na unachokijua
Akaenda akapita salama.
Haya mambo NI mazito.
 
Kwao kulinda haki na siri za mteja ni takwa la kikatiba wala sio maamuzi ya kampuni. Sisi Tanzania ambako ndio Tigo Tz wamesajiliwa ni takwa la kikatiba kampuni kutoa siri za mtuhumiwa.
Nimekuelewa vyema sana.

Ahsante kwa ufafanuzi wa kina
 
Ngoja tuone kama atapona.. ingekuwa management inajua wangetumia diplomasia kama nilivosema..
Tigo haiwezi kumwajibisha yule kamwe, anaeweza kumwajibisha yule ni mteja anaetumia tigo aliyekerwa na kile kitendo, ikiwa familia ya mbowe wenyewe utakuta hadi sasa bado wanatumia tigo vipi kwa raia wa kawaida huko horohoro tanga?
 
Back
Top Bottom