Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WAKINA MAMA WAJASIRIAMALI WA DODOMA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA FURSA ZA KIUCHUMI
▪️Wajipanga kujiimarisha kiuchumi kwa fursa za kiuchumi kwa fursa zilizopo Dodoma.
▪️Wajipanga kujenga Maduka ya kibiashara na eneo maalum la uwekezaji
▪️Wampa tuzo Mbunge Mavunde kwa mchango wake kwa wakinamama Dodoma
▪️Mbunge Mavunde kukabidhi kiwanda cha kukamua mafuta kwa wakinamama
📍𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀
Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoani Dodoma kwa kauli moja limempongeza Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuweza mazingira mazuri ya ukuaji wa kiuchumi wa wanawake pamoja na kuongeza fursa za kiuchumi mkoani Dodoma ambapo wananwake ni kundi kubwa wanufaika.
Pongezi hizo zimetolewa jana na Mwenyekiti wa Jukwaa Bi. Maryrhobi Mabhaya wakati wa Kongamano la wakina Mama wa Dodoma kumpongeza Mh. Rais Samia kwa namna ambavyo serikali ya awamu ya sita ilivyochochea maendeleo katika Mkoa wa Dodoma na hivyo kutengeneza fursa kubwa ya kiuchumi.
“Dodoma ya leo sio kama ya zamani,maendeleo ya Dodoma ya sasa huwezi kuyasema bila kumtaja Rais Samia.
Hivi sasa kuna fursa lukuki za kiuchumi ambazo wakinamama tukizitumia vizuri zitasaidia kubadilisha uchumi wa wakina mama wa Dodoma.Sisi kama Jukwaa malengo yetu ni kujenga eneo la maduka makubwa“Shopping Mall“ pamoja na kuwa na eneo maalum la biashara ta wakina mama“Alisema Maryrhobi
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mlezi wa Jukwaa Mama Tunu Pinda amesema ni wakati sasa wanawake wa Dodoma kutumia fursa hizi kubwa kiuchumi ambazo Mh. Rais Samia amekuwa kinara wake kuzitengeneza hapa Dodoma ili kujiimarisha na kukua zaidi kiuchumi.
Akiwasilisha hotuba yake,Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema tangu maamuzi ya kuhamishia shughuli za serikali Dodoma,fursa nyingi za kiuchumi zimeongezeka na hivyo serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuliona kundi kubwa la wanawake likinufaika kupitia sheria na sera wezeshi.
Mavunde alieleza kwamba,Mh. Rais Samia amerudisha mikopo ya wakina mama ya 10% na pia Sheria ya Manunuzi ya Umma imefanyiwa marekebisho ili Taasisi nunuzi zitenge 30% ya manunuzi yake kwa ajili ya makundi maalum likiwemo kundi la wakina mama.
“Nitaendelea kuunga mkono jitihada za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa vitendo,na mwaka huu nitakabidhi kwa kikundi cha wakina Mama Ipagala mitambo ya kusafisha mafuta ya Alizeti ambapo ni sehemu ya ahadi yangu ya uanzishwaji wa kiwanda cha kuongeza thamani mazao kila mwaka“Alisema Mavunde
Wanawake wa Dodoma walitumia jukwaa hilo pia kumpa tuzo ya Mh. Anthony Mavunde kwa kutambua mchango wake mkubwa kuwaendeleza wakina mama mkoani Dodoma
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-11-16 at 09.45.45.jpeg89.8 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-11-16 at 09.45.45 (1).jpeg109.3 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-11-16 at 09.45.46.jpeg126.7 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-11-16 at 09.45.46 (1).jpeg102 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-11-16 at 09.45.48.jpeg87 KB · Views: 6