Uzembe wa hali ya juu kivipi? Nauliza wakati mnakojoa huwa hamjui kama mnapanda mbegu na kwamba inaweza ikaota au isiote?
Marianah; Mnapokojoa huwa hamjui kama mnapanda mbegu ambayo inaweza iote au isiote?
Jokajeusi; Mwanamke asiye wa ndoa hatuwezi fikiri jambo hilo.
Marianah; Ila.
JokaJeusi; Hizo zinaitwa mbegu zilizoangukia barabarani. Hazijapandwa. Tofautisha kupandwa na kuangukia barabarani. Mbegu zilizopandwa hupandwa kwa mke. Lakini zilizoanguka barabarani ni hao michepuko. Mchepuko ni kama barabara tuu mtu yeyote huweza kuipitia. Hata magari hupitia.
Marianah; Acha dharau na kejeli. Isikute hata wewe mbegu yako ilianguka barabarani.
JokaJeusi; Haiondoi Ukweli.
Marianah; Nyie wanaume ndio Sababu ya Sisi kuwa single mother.
JokaJeusi; Upo sahihi. Ninyi mlijigeuza Barabara unafikiri tungepita wapi. Matokeo yake tulipopita tuliangusha Mbegu zikaota.
Marianah; Msitulaumu basi. Kubalini kutuoa.
JokaJeusi; Barabara ikizoea kupitwa na Watu haiwezi ota majani.
Marianah; Unamaanisha nini?
JokaJeusi; Nilipaswa kukuuliza wewe swali hilo kuwa ulimaanisha nini kujigeuza barabara. Matokeo yake watu wanaangusha mbegu, Ng'ombe na mbuzi wanaacha vinyesi vyao. Labda ungejibu swali hilo ningejibu swali lako.
Marianah; Shida mnawalaumu wanawake pekee yao.
JokaJeusi; Sio tunawalaumu wanawake. Bali ni kuwa hatuwezi kuwaoa.
Marianah; Kwa nini msituoe wakati mmetuzalisha?
JokaJeusi; Uliona wapi mtu akijenga Nyumba Barabarani?
Marianah; Mmmmh!
JokaJeusi; Ndio hivyo. Hukumbuki bomoa bomoa ya JPM kipindi kile.
Marianah; Inatosha. Naona umeamua kunitukana.
JokaJeusi; Sorry kama nimekuudhi. Ila ukweli ni kuwa Kuoa single mother ni sawa na kujenga nyumba barabarani. Bomoa bomoa ikija nyumba inabomolewa.