Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Unacho sema ni kweli kabisa hasa hiyo no.2
 
Mbona hizi hasira hazionekani Kwa wababa wanaoishi na watoto wao bila Mama yao
 
Hiyo hasa ukute mume anamtenda sana mke hapo hasira zinaishia kwa mtoto na kauli ya "...baba yako ananiumiza kichwa na wewe unanisumbua...pumbavu" hapo mtoto anapewa
 
Nina jirani yangu hapa single mother kila siku anawatukana wanae mapacha matusi ya nguoni..... Tusi alilowapa leo mchana lilinitisha ilibidi nitafute safari ya ziada
 
Hiyo hasa ukute mume anamtenda sana mke hapo hasira zinaishia kwa mtoto na kauli ya "...baba yako ananiumiza kichwa na wewe unanisumbua...pumbavu" hapo mtoto anapewa
Haswa lazima itokee hivyo. Inasemekana mwanamke ana maneno mengi sana ambayo hayo yote yanatakiwa yatuliwe kwa mumewe, hata kama hayana faida lakini madam ameyasema kwake hiyo ni faraja tosha. Akikosa sehemu pa kuyamwaga hata mwanamke mwenzie anakuwa adui.
 
Mbona mi mwanangu hajawahi sikia hata tusi la nyoko toka kwangu hiyo haihusiani na kuwa single mother wala nini ni tabia ya mmama mwenyewe
 
source ikowapi ya huo utafiti wako???
hoja yako ni dhaifu sana mimi ni mmoja nilie lelewa na mama tu lakini alinilea katika misingi mizuri na yenye maadili

mambo ya kuchezea kichapo na kuoga matusi source yake sio u-single mother inategemea na mazingira manayoishi na tabia za wazazi wenyewe lakini sababu sio kuwa single

sikunyingine lete hoja nzito na zenye mashiko alafu kwenye heading yako umeanza “utafiti......" utafiti gani hakuna takwimu yoyote mkuu izo ni hoja zako za kutunga
*virginboy*
 
Sio wote mwanangu nampenda kupitiliza hadi naambiwa na mharibu kumpiga labda unikose maana kumdekeza kumemfanya awe na ka ujeuri flan kumtukana hata siku mmoja zaidi ya kumtania masikio hayo inatagemea umeachwa kwa maxingira yap na baada ya kutendwa na ukatoa msamaha namsamehe huyo utaishi maisha ya raha sana sema wengi bado hawafahamu hili
 
Nikiwa na experience ya kutosha.

Ulichokisema hakina ukweli wowote.
 
Upo sahihi sio single mothers wote, ila ukichukua parcentage ya wastani wa watoto wanaochezea kichapo au/na kukoga matusi asilimia kubwa inaenda kwa watoto wanaolelewa na single mother hasa ktk jamii zetu masikini ambapo mama hana kipato cha uhakika, mara nyingi hasira anapeleka kwa mtoto asiye na hatia
 
Nikiwa na experience ya kutosha.

Ulichokisema hakina ukweli wowote.
Fanya utafiti kidogo tu maeneo unayoishi wakusanye watoto kumi waulize swali mara ya mwisho umepigwa lini na mama yako watakao kujibu wamepigwa au kutukanwa waulize unaishi na nani then angalia uwiano utakuja rekebisha kauli yako hapa
 
Nina jirani yangu hapa single mother kila siku anawatukana wanae mapacha matusi ya nguoni..... Tusi alilowapa leo mchana lilinitisha ilibidi nitafute safari ya ziada
Wakati mwingine anamtukana mwanaye kumbe anajitukana yeye bila kujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…