Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Na watoto wa kike waliolelewa na Single mama wana Over confidenc balaa..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119] Wanahisi wanaweza ishi bila mwanaume kabisaaa...
Hao sijajua kwa kweli.
Ila single mama tu anakuwa na jeuri ya kusema lolote Maana anaplay part ya baba pia.
 
Eeeh swali zuri sanaaa...WANAUME mpaka mtu umemjua tabia yake halisi hasa kwa wanawake jua ameshakutafunaa...!! Huwaga hutuwi really mpaka pale umeshapata unachokitaka hapo ndo makucha yanaanza ndo maana single mother hawaishi na kujua tabia ya mtu hakukufanyi wewe ujue Maovu yake kabisaa maana watu tunabehave tokana na mazingira so wadada wengi mpaka waje kujua tabia halisi na maisha halisi ya wanaume wanaodate nao ni TOO LATE SANA. Kuijua tabia halisi ya Mtu sio Jambo la mwezi never ukute hata wazazi wako hawajui tabia yako halisii hadi leo[emoji23][emoji23] wanakuja kusikia tu umetia mimba mtoto wa watu huko ukamtelekeza.
Nani alikudanganya mwanamke lazima ugawe uchi wake? Mume haombi uchumba gesti. Ukiona hivyo ujue binti naye hajitambui
 
Nanukuu hapo "mkitambua ya kwamba wao ni dhaifu" amewaambia ninyi ndiyo mtambue hivyo lakini yeye Mungu hatambui hivyo sasa kama wewe unadhani upeo wako wa kufikiri uko kama wa Mungu basi una tatizo mahali na unahitaji msaada

Halafu kumbe unajua kuwa mmeambiwa muishi na wake zenu kwa kuwahurumia sasa hiyo huruma mbona hamna matokeo yake mnasababisha single mothers halafu lawama mnawatupia wao maana mngekuwa na huruma msingekuwa mnazalisha na kuacha halafu kwa ujasiri mnakuja kusema kabisa eti "mwanamke asijilinganishe na mwanaume kwa sababu yeye ndiye anayeumia zaidi"
Kwa hiyo sisi tunajua kuliko Yule aliyetufundisha tutambue hilo?
 
Uzi gani huo uliowaambia ukweli wanaume tu mbona sijawahi kuuona?? Hebu siku anzisha uzi unaokemea maovu ya wote wanaume na wanawake bila ubaguzi halafu tuone kama kuna atakayekupinga yaani atakayekupinga mimi nitakula naye sahani moja[emoji16][emoji16]
Hata wewe waweza kufanya hivyo
 
Nani alikudanganya mwanamke lazima ugawe uchi wake? Mume haombi uchumba gesti. Ukiona hivyo ujue binti naye hajitambui
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Unavyosema asigawe uchi utadhani huwaga Huombi nyuchi wewe...!! Wee jamaa punguza unafiki kidogo bhasi... Mwanaume kamili anapokuwa na mwanamke hilo ndo jambo Kubwa liloweza kumfurahisha kwenye mahusiano na demu hawezi sema abane alafu kesho mzee baba kama wewe unaenda kutafuta kwingine... Sasa tatizo unaepewa ndo huna plan zozote nae unakula pekuu..
 
Na watoto wa kike waliolelewa na Single mama wana Over confidenc balaa..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119] Wanahisi wanaweza ishi bila mwanaume kabisaaa...
Hizi comments zinaonyesha mtazamo wako
 
Umenitukania umetuliza.
Maana ni mpambano wa kupigania maadili huu.
Makahaba na maasherati yanatetea na kuubariki ubazazi wao waziwazi, shetwani ana wafuasi wengi sana kuliko tunaowafahamu!

Ujingaujinga 'kabila hiyo' ndiyo chanzo cha watoto wa mitaani wenye baba zao wasio na baba kuongezeka kila uchao!

Tena mada yako inafaa sana kuwa shamba darasa kwa vijana wanaotegemea kuanza maisha ya ndoa ili wasirukie magumegume kwa hadaa ya penzi motomoto. Hizo ni ghilba na wizi wa mapenzi wasiouelewa wengi.

Hakuna kosa kubwa kwa mwanaume kujenga msingi mbovu wa ndoa yako, maana waweza kujuta maisha yako yote hadi kufa na huku umevaa tai shingoni.

Hivi kijina shababi unajisahauje hadi ndoa yako ya kwanza unaanza na single mom!

Yote uliyoeleza mkuu, kijana akiyafuata akaanza nayo, dunia hii ataishi kama yupo ahera kwa ndoa yenye heri na heshima, ingawa vikwazo havikosi.

Nakuomba usikatishwe tamaa na majibu ya watu waliokwisha kukosa maadili tangu wakiwa tumboni mwa mama zao.

Asante sana mkuu, tuungane pamoja kukisema ambacho jamii inakiogopa ingawa ni ukweli unaojenga
 
Basi fahamu haya:

Mwanamke aliyezaa huhamishia mapenzi kwa mwanaye. Hali huwa hivyo hata ndani ya ndoa, kiasi kwamba ndoa nyingi hupoteza mvuto pale tu mtoto anapozaliwa. Kwako wewe kijana unayetaka kujitwika mabomu uoe single mother.

Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu. Lakini kama hata hilo halikutosha kukushawishi, usithubutu kuoa mwanamke ambaye ni single mama, labda kama una uvumilivu usiopimika. Yako mambo kadhaa ambayo yanamfanya single mama asiwe sehemu ya mtarajiwa wa ndoa.

1. Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati. Binti anapojiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa kwa kigezo cha kutafuta kuolewa ni dalili mbaya hata kama ataolewa kweli. Hii inaonyesha kuwa ana udhaifu kwenye eneo la ndoa kiasi kwamba yuko tayari kuutumia mwili wake kama rushwa ili kufanikisha ndoa. Hii haitofautiani na mwanamke aliye ndani ama nje ya ndoa kutumia tigo yake kama kishawishi cha kumshika mwanamume. Unapotumia ngono kama sehemu ya ushawishi, ama kama silaha ya kumteka mwanamume ujue kwamba unaondoa thamani yako na kuingia kwenye kundi la makahaba. Ni kweli uchi wa mwanamke ndio silaha yake kwenye mahusiano, lakini si kwa kuigawa hovyo, bali kwa kuwanyima wanaoitamani ili apatikane mwenye nia thabiti ya ndoa.

Inapotokea binti kajiingiza kwenye mapenzi mpaka kupata mimba, tayari keshapata muunganiko mwingine na mwanamume aliyempa mimba hiyo, tayari wameunganishwa na mtoto huyo, ingawa bado mwanamume aliona huyu mwanamke hafai kuwa mke, alikiwa anamtumia tu kukidhi kiu yake mpaka pale atakapompata mtu sahihi. Sasa wewe ni nani hata ukajiingize kuoa mwanamke wa aina hii?

2. Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo, bali kutakuwa na sharti la mtoto. Kwamba iwapo utamtunza mtoto kama single mama atakavyo basi utapewa mapenzi matamu. Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke apatapo mtoto mapenzi yote huhamia huko, hivyo wewe jiandae kuwa chaguo la pili kwake. Haya sio mapenzi na ujue tu kuwa huwezi kuwa na amani kamwe.

3. Mtoto si wako. Hata kama utampenda na kumhudumia kwa namna yoyote ile, ukweli utabaki kuwa huyo si mwanao, sio damu yako. Ni kwamba umejitwika jukumu la kumhudumia mtoto wa mwanaume mwenzako ambaye ndiye ataendelea kutambulika kama baba mzazi. Siku akikua ataanza kumtafuta aliyechangia mbegu mpaka akaja dunuani, sio aliyechangia ugali. Ikitokea mmeachana na single mama, ujue ndio mwisho wa kuonana na mwanao mpenzi uliyekuwa ukimtunza kwa nguvu zako zote.

4. Utatumia nguvu kubwa kulilinda penzi. Ili ujihakikishie kuwa single mama anatulizana na wewe, utahitaji kuishi maisha ya kumfurahisha yeye, kumpa atakacho ili asije akamkumbuka mume wake wa kwanza. Namna pekee ya kumfurahisha ni kuhakikisha mtoto wa mwanamume mwenzako anapata maatunzo mazuri, nguo nzuri, elimu nzuri n.k. Utalazimika kuwa karibu naye kuliko hata baba mzazi anavyokuwa, yote haya ni kutafuta kumfurahisha single mama. Utaishi maisha ya kujipendekeza, yenye stress nyingi.

5. Huna sauti juu ya mtoto. Hata kama utataka umchujue mtoto huyu kuwa mwanao kamili, umpe malezi halisi ya mzazi, kuna mahali utakwama tu. Huwezi kumwadabisha kwa mikono miwili, lazima mmoja utakuwa nyuma na mwingine utakuwa mbele. Mara zote utakaa ukijiuliza, labda nikimfanya hivi mama yake atadhani namchukia, jamii nayo itanifikiria vingine. Utajikuta wewe mwenyewe unajiwekea mipaka hata kabla pilato hajakuhukumu kwa kuvuka mstari!! Pigo kubwa zaidi ni pale single mama atakapokutamkia kuwa unamtendea hivyo kwa sababu mtoto sio wako. Hapo utabaki kama mjinga fulani aliyepigwa bumbuwazi asijue aukabili vipi ukweli huu mchungu.

6. Chanzo cha vurugu kwenye familia. Hata ikitokea mmezaa watoto wengine, bado mapenzi hayawezi kuwa sawa. Single mama wana kawaida ya kuwaandalia mazingira watoto wa baba wengine tofauti hao wa baba waliye naye wakati huo. Hufanya hivyo kwa hofu kuwa watoto hawa mara nyingi hawana urrithi kwa baba aliyewalea. Hii huleta mgawanyiko mkubwa kwenye familia kiasi cha watoto wenyewe kuchukiana. Hata ndugu wa mwanamume hawawezi kamwe kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya familia kwa sabubu sio damu yao na anao ukoo mwingine kabisa. Hawezi kujitambulisha kwa jina la baba wa kambo kwa sabubu hana muunganiko wowote naye. Hata ikitokea baba mlezi amekufa, ukoo wake hauwezi kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya urithi. Tunajifunza kwa wanyama wengine pia kama simba, ambapo anapoinuka dume mwingine kuongoza majike, huua watoto wote àliowakuta kisha huanza upya kusaka watoto wake. Sasa sisi hatuwezi kuua, bali tunaweza kuepuka taabu hii kwa kutokuoa mwanamke mwenye watoto.

7. Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo. Kwa kawaida mwanamke akishazaa na mwanamume, ule muunganiko huwa haufi. Tayari ni mzazi mwenza na hana cha khmficha tena, hivyo kupasha kiporo ni jambo la kawaida tu. Pia mama atataka mtoto amjue baba yake halisi kwa ajili ya siku zijazo, hivyo hawezi kujiweka mbali na mzazi mwenzake. Sasa mzazi mwenza ni juu yake kuamua kuendelea kumla ama la, kwani hakuna kutongozana tena, ni kupanga miadi tu na kukutana kuserebuka. Kidume wewe utageuzwa baba mlishi huku haki nyingine zote zikielekezwa kwa mwenye mwanaye.

Ukweli ni kuwa single mama anapopata mume, focus yake sio ndoa bali ni malezi ya mwanaye. Anataka uhakika tu kuwa mwanae ataishi na atapata matunzo bora ili siku za usoni aje kumsaidia yeye.

Ewe kijana, usijiingize kwenye mtego utakaoharibu maisha yako. Tafuta bikira atakayefunga kiapo nawe, achana na wanawake waliozaa hovyo kwa kukosa mwelekeo.

Hapa sijazungumza juu ya walioolewa kisha waume zao kufariki, kwani kwao hawa yako mambo mengi pia nyuma ya pazia ya kuchunguza.
The Bitter Truth!
 
Dada zetu na mama zetu wanaishi maisha ya taabu sana kweli hili bara la giza. Huu ujinga wa kuwasemasema single moms lazima ukomeshwe.

Kulingana na mila NA desturi za mwafrika, suala LA kuwasemasema single moms haliwezi kukoma wala kukomeshwa KWA sababu ktk jamii zetu inaonekana dhahiri hao single moms tayari wamejikomesha wenyewe kwa kutaka balaa LA kuandamwa NA stigma hii kutokana na kuzaa nje ya ndoa, tena bila ya mpango au utaratibu.
 
Madada zetu,jitunzeni jamani.Binafsi,kwa mtazamo wangu na kwa niliyoyashuhudia hapa chini ya jua kuoa single mother kuna changamoto in many cases,few of them ni watulivu.Ila kwa walio wengi kwakweli siyo.Vinginevyo mkutane wote mmeshakuwa na watoto tayari,labda itasaidia kidogo
 
Wengine wanatafuta nyie mnawakataaa...
Screenshot_20190911-182257.jpeg
 
Back
Top Bottom