Katika kujadili Maana ya maana ya maana ipo mikabala mingi na nadharia nyingi kuhusiana na Fasili ya neno Maana.
Embu tuone hapo chini. Dhana
ya Semantiki
Etimolojia ya neno
semantiki inatokana na maneno mawili ya Kigiriki yenye maana ya
“sema”= maana na “ticos” = ishara. Hivyo, semantiki ni ishara za maana ama zenye
maana. Kiisimu semantiki ni taaluma inayohusika na maana katika tungo ama maana
za maneno.
a)
Semantiki hutafiti maana za fonimu,
mofimu, maneno na tungo.
b)
Maana hushughulikiwa katika viwango
vyote vya lugha, kama vile sauti, maneno na sentensi.
Maana
ya maana
Hakuna jibu la mkato au
jibu rahisi linaloelezea juu ya maana ya maana, dhana ya maana ni telezi,
kutokana na utelezi huo wanaisimu mbalimbali wameeleza maana ya maana kama
ifuatavyo.
1. Maana kama dhana (Richard
na wenzake, 1925) wanasema maana ni ile dhana na dhana hii ni ya msemaji yaani
msemaji huwa na dhana fulani kabla hajasema.
Udhaifu:
si
rahisi kuwa na dhana inayofanana kati ya msemaji na msikilizaji. Baadhi ya
maneno ya lugha hayana dhana mahususi hadi yatumike na maneno mangine.
Mfano:
pia, na, kadhalika
2. Maana kama mwitiko
(Bloomfield
na C. Morries) wanasema maana ni mwitiko wa msikilizaji. Wao wanatazama tabia
ya binadamu anapoitikia neno fulani linavyotamkwa.
Udhaifu: si
rahisi wasikilizaji zaidi ya mmoja kuitika katika maana moja.
3. Maana ni matumizi :
Wanazuoni
wa msimamo huu wanasema maana ya neno hutokana na matumizi yake katika mfumo wa
lugha. Neno kama lilivyo halina maana kama haliko kwenye matumizi au muktadha.
Maana ya neno inabadilika kulingana na muktadha.
Udhaifu:
lugha
inatazamwa kama kapu lenye maneno mengi yanayotumika kwa wakati mahususi na
kuchukua maana kwa wakati huo. Kitu ambacho si kweli.
4. Maana ni
kitaja/kiwakilishi/kirejelee majumui : Wanaisimu katika
mtazamo huu wanasema maana ya neno ni kile kitu halisi kinachowakilisha kitu
husika. Maana ya neno iwe katika kitu halisi kinachoweza kutambuliwa kupitia
milango ya fahamu (kuona, kuonja, kunusa, kugusa, kushika). Wanazingatia
uhalisi wa umajumui au maisha. Dhima ya lugha ni kupambanua vitu mbalimbali
katika ulimwengu unaomzunguka mtu.
Udhaifu: kuna
maneno yasiyowakilisha kitu katika mazingira yanayotuzunguka. Mathalani, kuwa,
na, pia, katika, wa, n.k. kuna maneno yanarejelea vitaja zaidi ya kimoja.
5. Fasili nyingine za maana ya maana
Kwa mujibu wa TUKI (1990: 39) wanasema
maana ya maana ni fahiwa (sense) ya
neno au kirai ama dhana, matumizi au kitajwa.
v Maana ni
maelezo yanayotumiwa kukitambulisha au kukifafanua kitu
v Maana ni
kusudio au dhamira ya mtu
v Maana ni
ishara au dalili ya jambo
v Maana ni
thamani, umuhimu au nafasi ya kitu au jambo fulani kwa mtu