Nina mwanamke ambae tuna mtoto, ila hatukuweza kuoana kutokana matatizo yaliyojitokeza wakati huo. Baadae alioolewa na sasa ni zaidi ya miaka mitano tangu aolewe, mtoto alimwaacha nyumbani kwao, nilimuomba baada ya kuolewa tukatishe mawasiliano kwa afya ya mahusiano yetu, tukawa hatusiwasiliani tena, mawasiliano pekee yakabaki kwa mamaake mzazi na mdogo wake wa kike.
Baadae nilimchukua mtoto nikampeleka Kenya [emoji1139] kusoma, ikawa wakati wa likizo nampeleka kwa bibi yake maana ndiko alikokuzoea, sasa hivi karibuni nilimfuata mtoto nimpeleke shule, nikamkuta huyu mzazi mwenzangu yupo kwao, akaniambia kuwa alikuwa ananisubiria mimi ana mambo muhimu ya kuniambia. Akasema mazungumzo hayo yatafanyika mjini na vile vile alitaka kumfanyia mtoto wake shopping, tukaondoka mpaka mjini, lakini cha ajabu alitupeleka kwenye nyumba ambayo amejenga akasema amemjengea akanipa na documents zote, baadae akanionesha dukani ambalo amefungua na faida ataiweka kwenye akaunti ya mtoto.
Baadae tukaenda kupata chakula ili tuendelee na safari ya shule, tukiwa kwenye chakula nilimuuliza amewezaje kujenga na kufungua duka kubwa vile, akaniambia anamuibia mme wake, kwamba yeye ndie msimamizi wa biashara za mme wake na pesa zote anachukua, alinionesha akaunti yake imenona.
Mbaya zaidi kilichonifanya niandike hapa aliniomba usiku huo tuwe pamoja na kesho yake ndio tuendelee na safari, baada ya ombi hilo, nikamfikria jamaangu (simfahamu) jinsi anavyoibiwa na huyu mwanamke halafu na mimi nimuibie? Nikaona nikikataa moja kwa moja angejisikia vibaya, nikamdanganya nimeisha kanyaga miwaya, akaishia kunishukru na kunipongeza kwa kumuokoa.
Baada ya hapo nimefikria sana kuhusu hawa single mothers, hivi wanakwama wapi? Wanakumbuka nini kwa wanaume waliowazalisha?