Jaribu kuelewa concept, usitetee uharibifu kwa sababu tu kwenye jamii wapo. Simamia kweli daima, usisombwe na upepo wa mazoea, angalia msingi wa jambo naw utakuwa salama na kizazi chako, Mwenyezi Mungu akubariki
Siku hizi kumetokea tabia uhalalishaji wa mambo kwasababu tu yanafanyika, hata kama ni jambo ovu utaskia mtu anasema mbona ni kawaida, mbona watu wanafanya..
Jambo kufanyika mara nyingi zaidi linafikia hatua ya kuonekana kama ni acceptable, hata kama linakiuka maadili au linawakosti binadamu wanaoyatenda hayo mambo.
Ni sawa na mtu kukemea tabia ya wizi kwa kueleza athari zake kama kuuliwa kwa kuchomwa moto, halafu mtu anakuja kutetea anasema wizi mbona upo na watu hawachomwi moto, wanajenga maghorofa na wanapeleka watoto English Medium.
wao wanaona kama "you can do what you do as long as you can dodge a bullet"..
bila kujali na bila kujiuliza kwanini hio bullet ilengwe kwako?
na kwanini upoteze muda kujifunza jinsi ya kuikwepa wakati YOU COULD HAVE PUT YOURSELF IN A POSITION WHERE YOU ARE NOT THE TARGET.
baadhi ya single mothers kuolewa haimaanishi kwamba kuwa single mother ni jambo jema.
kuwa single mother inaathiri 95% ya wanawake, ila wanapongezwa 5% ya wanawake ambao wameweza kuzalishwa na "kubahatika" kuolewa.
bila kujali kwamba kwa uwiano wa 95:5 mizani haijabalance na kuna gap kubwa sana. Bado wahanga ni wengi.