Avoid hast generalizations!
Pia single fathers sio wengi kama unavyoelezea, jamii kubwa imezungukwa na single mamaz
Hii ipo kisheria zaidi. Mtoto akiwa chini ya miaka 7 baba hana mamlaka ya kisheria kukaa na mtoto. Ukiona mtoto wa chini ya miaka 7 yupo na mama basi kuna uwezekano baba yupo na anasaidia malezi ya mtoto wake, lakini ukiona mtoto wa umri huo yupo na baba ujue mama alimtelekeza mwanae. Suala la kuona single maza wengi haimaanishi kwamba baba mtu katelekeza mtoto, isipokua taratibu za sheria na ustawi wa jamii zinamzuia kukaa na mtoto
ata waliolelewa na hao mama hatushangai kuona wakijikita kuanzisha hizi mada kuwaponda! Nyie kama mnaongelea singo maza ambao ni gen z labda, wamama wengi nilioona wakilea watoto peke yao wanapitia magumu sana!
Hao wamama sio watakatifu kwaiyo usijenge mtazamo kwamba kwenye kila kesi ya single maza, mwanaume ni vilain na mwanamke ni victim.
Mada yako iko financially sana, unataka mtudate na singo maza asiombwe pesa wakati ata ambao wanatoa mimba mnawahonga sana tu! Unataka mwanamke akiachana na mwanamume waliozaa mtoto asimhudumie! Hiyo ni ndoto..
Naona kama haujanielewa. Suala la matunzo ya mtoto ni jukumu la wazazi(baba na mama) kwaiyo single maza anavyoanzisha mahusiano mapya sio sawa kutaka au kuona kwamba huyu mpenzi wake mpya abebe jukumu la gharama za malezi, na hili suala la kubeba gharama za malezi ya mtoto ambae sio wako ni moja ya changamoto inawafanya vijana wasite ku-settle na single mazas
Ifike mahali muandike na chanzo cha hili kundi sio mnaandika kama vile mwanamke anajitia madole ndio anatapa huyo mtoto!
Suala la kushika mimba na kuzaa muamuzi mkuu ni mwanamke. Hakuna kinachoweza kutokea bila mwanamke kuruhusu, vinginevyo awe amebakwa. Na hili kujua kama mwanaume yupo siriaz na wewe ni mpaka pale atakapokuoa rasmi. Mwanaume hajakuoa, kwenu hawamjui, kwao hawakujui wewe umebeba mimba basi hapo hata ukitelekezwa hauna uhalali wa kulalamika wala kuwarushia lawama wanaume, kwa sababu hayo ni matokeo ya maamuzi ya kipumbavu uliyoyafanya wewe mwenyewe. Accountability inawashinda sana wanawake.
Ofcoz ata mi sipigagi cm kwa baba mtoto, nimpigie ili tufanyeje? Nikipiga cm ndio mtoto anafanyaje? Ukipata muda kamuone dogo kama kuna vizawadi unapeleka biashara imeisha eti nipige cm kama mtoto hana changamoto napiga cm kutafuta nini ss kama sio kuanzisha mambo mengine bila sababu za msingi! Tunalazimishaga uzungu wkt wengi wenu maisha mlokulia hayana tofauti na hao watoto wa mzazi mmoja! Mmeigeuza kama ulemavu na mimba mnatutia nyinyi!
Uwe unasoma between the line. Mama mtoto kushindwa "kupiga hata simu" ni mfano tu umetumika kuonyesha kwamba hajali chochote kuhusu mwanae. Kuonyesha kujali sio kupiga simu hata hata kumtembelea shuleni au kumoelekea mtoto zawadi kama ulivyosema ni kujali pia.
Natamani sana kujua umri wa mnaopiga vita hili kundi na bando kutwa kujaza magesti mxiew!!
Tatizo wanawake hamtaki kukubali ukweli kwamba hiki kizazi cha vijana wa sasa hivi sio kile kizazi cha wababa na wazee wetu ambao kimsingi walikua ma-simp, ndio wakaja na misemo ya kioumbavu ya kitanda hakizai haramu, kuchapiwa siri ya ndani n.k Kizazi cha vijana wa sasa ni tofauti, ni kizazi ambacho kimesha-unlock manipulations na cheating code za wanawake. Kwaiyo mwanamke utapokelewa kutokana na nia unayokuja nayo kwenye mahusiano.