Inawezekana, labda tunatofautiana katika itikadi zetu za dini au imani mkuu.
Ila kwa dini yangu, mungu anasema katika maandiko "Unaweza ukapenda sana kitu fulani kwa mapenzi ya dhati, ila kikawa na madhara na si kizuri kwa maisha yako. Na unaweza ukachukia kitu kwa dhati ila kikawa na faida kwa maisha yako. Kila kitu mungu ndio anaojua zaidi".
Hii kauli imebeba kila kitu, kuanzia mahusiano, chakula na mpaka starehe tunazofanya. Unaweza ukamchukia mwanamke kwa kigezo ni single mother, ila akawa ndio bora kwa maisha yako, na unaweza ukampenda kwa dhati mwanamke alie mzuri kimaumbile/bikra ila ndio akawa anamadhara katika maisha yako
Kama hauta kubaliana na mimi kwa hilo, basi naomba nisamehe, tusibishane mkuu.